Kwa jamii nyingi kijana akishapata umri basi anaonekana ameshakuwa mkubwa na hastahili tena kuwepo hapo kwako mzazi na mara ingine kama ataendelea kuwepo, basi atakereshwa almradi aondoke akaanze kujitegemea na s'tyms haya yanafanyika bila hata kujali kama mhusika ana ajira au la.
Wengi wanadai kumwondoa kijana kunaichangamsha akili yake kumfanya kijana ajitambue zaidi aache kujibweteka aongeze juhudi za kupambania maisha n.k.
Hii ni tofauti kwa jamii zingine hasa za kimwambao. Wao kijana hakui kwa mzazi. Mandhari mzazi yu hai basi mtoto atabaki kuwa mtoto tu, maisha yake yote. Huko kijana anaweza kuishi na wazazi hadi akapata wajukuu na pengine hata kuzeekea na hata kufia akiwa
hapohapo kwa wazazi.
Haya mambo wakuu yamekaaje?
Je, ungependa kumwona kijana wako katika taswira ipi kati ya izo mbili hapo juu?