Lipi ni sawa, kumfukuza kijana wako hapo kwako ili akaanze maisha yake au kumwacha azeekee hapo kwako?

Lipi ni sawa, kumfukuza kijana wako hapo kwako ili akaanze maisha yake au kumwacha azeekee hapo kwako?

Kwa maisha magumu na heka heka za kutokua na kazi maalum niliopitia baada ya kufukuzwa ,na Mzee kwangu nitakua tofauti sana, mwanangu wa kiume akae tu home hata akipata na vitukuu hapa sawa
Maisha ya kujitegemea bila kua na msaada au support yeyote kwa ndg mabaya sana unaweza kujikuta kibaka bila kupenda

Napenda sana mfumo wanaoutumia baadhi ya kabila kama wairaq kwao mtoto wa kiume akifikisha umri wa kuoa anakatiwa ngombe za kutosha then anaenda kujitafuta
Mwakani dogo mtoto wa sister namtimua kwangu akajitegemee. Anapata hela lakini ameshindwa kujitambua kwa vile ana mahali pa kulala na kula! Hela anayopata anatumia ovyo ovyo tu! Naamini akiwa na kwake atafanya vizuri! Wazazi tuwe wakali kwa watoto wetu kijana miaka 30+ bado linaninginiza makend... home kufanya nini? Fukuza huo mfugo!
 
Kwa maisha magumu na heka heka za kutokua na kazi maalum niliopitia baada ya kufukuzwa ,na Mzee kwangu nitakua tofauti sana, mwanangu wa kiume akae tu home hata akipata na vitukuu hapa sawa
Maisha ya kujitegemea bila kua na msaada au support yeyote kwa ndg mabaya sana unaweza kujikuta kibaka bila kupenda

Napenda sana mfumo wanaoutumia baadhi ya kabila kama wairaq kwao mtoto wa kiume akifikisha umri wa kuoa anakatiwa ngombe za kutosha then anaenda kujitafuta
Kumfukuza kijana ili akajitegemee bila ya kumwandalia vianzio ni unyanyasaji wa kijinsia.

Kuingia kichwa kichwa mitaani kuanza maisha kunaweza kuhatarisha maisha ya mwanao juu ya usalama wa maisha yake na kupelekea kipato atakachokipata kwenye mihangaiko yake kisimsaidie lolote.

Faida za kijana kubakia nyumbani wakati akijitafuta ni kuserv gharama za mapango na chakula kwa ajili ya kujiandaa kujitemea bila ya kuwa na pressure.

Siwezi mfukuza kijana mwenye nidhamu zake akajitegemee kwa kigezo cha umri huku akiwa hana mbele wala nyuma, ataendelea kubakia nyumbani infinitively.

Kijana ninayeweza kumfukuza nyumbani ni yule atakayezalia nyumbani bila kujali jinsia ya kike wala kiume.

Ukiwa hauna msimamo wa kusimamia nidhamu na adabu nyumbani kwako, makazi yatageuzwa gheto la wahuni ama danguro na vyumba ulivyovitenga kuishi wanao vitajazwa wajukuu na majukumu ya kulea mimba na vichanga vya wanao utayabeba wewe mzazi.

Hivyo kijana ama msichana atakayezalia nyumbani nitamfukuza akabebe majukumu ya kulea akiwa huko nje ya uangalizi wangu anakokujua mwenyewe maana huyo sasa atakuwa amekua kwa maana ya kukua na akili zake zimekomaa kwa majukumu ya kulea familia yake na kujitegemea na kwa hilo sina excuse.
 
Back
Top Bottom