Pre GE2025 Lissu aishangaa CHADEMA ilimpokeaje Nyalandu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Utaratibu wa kutetea kila maamuzi ya viongozi wa chama bila kuangalia faida au hasara zake ni mbaya sana.
Wapinzani wakifanya hivyo wanakuwa hawana tofauti na wanachama wa CCM.

Kuna kipindi mlikuwa mnatetea akina Mbowe kila kitu. Nikasema siwezi kuwa na chama kamwe. Siwezi kuwa katika kapu moja la 'collective imbecile' na kuburuzwa kama nyumbu.
 
Lisu ana tatizo la afya ya akili toka alipojeruhiwa chadema wawe makini kabla hawajampa madaraka makubwa
 
Ipo siku atashangaa pia Mbowe kuwa Mwenyekiti wa kudumu.

Ndivyo walivyo wanafiki.
 
Kichwa na habari ni tofauti na alichokisema Lissu.

"Lissu aishangaa Chadema ilimpokeaje Nyalandu",​

ISOMEKE, "SIJUI TULIMPOKEAJE NYALANDU" akiwa na maana naye alishiriki kwenye uamuzi, kama haujui kiswahili omba msaada.
Naona pia wengi walioandika hawajui kiswahili.
 
Chawa bhn, ukisoma hiyo habari imeandikwa 'Lisu ashangaa CHADEMA tulimpokeaji Nyalandu' kwamba na yeye Lissu alihusika ktk kumkaribisha Nyalandu hivyo kama ni kufanya makosa naye alihusika.
Ila chawa nyie mnatuambia Lissu aishangaa CHADEMA kumkabisha Nyalandu, kwamba yeye hakuhusika ktk uamuzi huo bila shaka ilikuwa ni uamuzi wa MBOWE🤣🤣🤣 ili kunogesha habari yenu na malengo yawe yametimia!.
 
Kwa hili Lisu nampiga, Nyalandu alifanya kazi kubwa sn kipindi yeye akiwa mgonjwa, mchango wake ni mkubwa sn kwa CHADEMA.
Lissu ndio kagoma sasa,ufisadi wa chadema unamkera sana lissu,Lissu aseme wazi sasa anagombea ucheaman ili aungwe mkono na mamilioni ya wapenda haki.
 
Hapo Lisu nakukatalia. Nyarandu by that time was to his senses! Aliacha ubunge kwa kupinga matendo ya Magufuli. Alikwenda Nairobi kukuona defying instructions from Magufuli!
Majira hubailika! Baadaye alirudi CCM , akakengeuka kama wanavyokengeuka wengi. hata CCM ikitoka madarakani, utaona uhalisia wa hao wanaojiita wana CCM kindakinda. Erythrocyte
 
Kutarajia mwanasiasa awe shabini (consistent) katika maneno na maamuzi yake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Siasa ni sanaa na sayansi inayotegemea upepo wa mawazo ya umma na vipaumbele kadha wa kadha ili kufanya mabadiliko hususan ya kitawala na uchumi na kijamii.

Kwenye akili ya mwanasiasa, matokeo ndiyo yanahalalisha mbinu iliyotumika (iwe chafu au safi).

Kwa mantiki hiyo, si ajabu wachache wakatolewa kafara kwa manufaa ya wengi.
 
Kwa hili Lisu nampiga, Nyalandu alifanya kazi kubwa sn kipindi yeye akiwa mgonjwa, mchango wake ni mkubwa sn kwa CHADEMA.
Nasikia kwenye kura za kupata mgombea wa cdm kwenye urais Nyalandu akimgaragaza vibaya Lissu. Lakin wakaamua kugeuza na kumpitisha tu Lissu. Lissu ana chuki na wivu.
 


Mbowe ndio Chadema hawezi ondoka, akiondoka chama kinakufa.
 
Reactions: Tui
KWA KAULI HIZI, MAANA YAKE CHADEMA HAKUPO SHWARI TENA, INASUBIRIWA TU MUDA UFIKE, KILA MMOJA AOKOTE MBAO ZAKE ASEPE!
-Mwenyekiti, acha waende, kama wengi tu, walivyoondoka, uimara wa chadema unabakia pale pale, chama makini hakiwezi kushikwa aidha kuongozwa na mtu mmoja mroho wa madaraka, anayejiona yeye pekee ndiye mwenye akili kubwa chamani, chama ni wanachama, chama ni majadiliano, chama ni mikutano ya ndani katika Kujadili mitafaruku ndani ya Chama, chadema watakuwa wajinga sana endapo wataruhusu miungu watu wenye ubinafsi, ""LISSU ONDOKA CHAMA KINUSURIKE INATOSHA SASA""
 
Umejiunga hapa jukwaani 2017 miaka miwili baada ya hiyo gia ya angani. Ulimzodoa nani miaka miwili baada ya gia ya angani? Mimi nimepinga tena humu humu toka Lowassa kapokelewa na kupewa nafasi ya kugombea urais kwa njia ya Vodafasta, pitia post zangu za nyuma ndio uje na maelezo haya.

Wapiga kura watakuwa wachache sana sio kwa sababu ya Mbowe kung'ang'ania madarakani, bali ni kwasababu ya chaguzi zetu za kishenzi ambapo kura zao haziheshimiwi.

Suala la kuanzisha chama kingine Cha siasa huo ni mpango wa muda mrefu wa Tiss. Lengo ni kuendelea kucheza na akili za wananchi Ili ccm iendelee kusalia madarakani kwa shuruti. Unaweza hata ww kuanzisha chama Cha siasa kama unaona vipi, au ww unasubiriwi kuanzishiwa chama tu?
 
Kwani hapa amezungumzia uginjwa wake au Nyalandu kujiunga / kupokelewa Cdm?!
Hakuna mtu alipokelewa Chadema Bila kikao kumsukumizia yote Mbowe sio sahihi

Lisu Vizuri aheshimu maamuzi ya Chama badala ya kuelekeza personal atlacks Kwa Mbowe
 
Mbowe alikuwa anataka kuongeza idadi ya wabunge tu bila kujali anamkubali nani kwenye chama, ndiyo maana kina Shibuda walikuja kuleta tabu sana CHADEMA.
Shibuda alikuja kabla ya ule upuuzi wa 2015, maana yeye aliingia 2010. Nilidhani cdm walijifunza kutokana na mwenendo wa Shibuda ndani ya cdm, maana Shibuda alikuwa mbunge kwa ticket ya cdm, lakini akabaki mwanaccm mtiifu. Ilifikia hatua hadi cdm wakamtenga Shibuda. Lakini 2015 wakafanya maamuzi ya kipuuzi kabisa kuliko ya huyo Shibuda.

Hata ukitazama kundi kubwa la viongozi wa cdm waliorejea ccm wakati wa dhalimu magu kwenye kampeni ya kuunga mkononi juhudi, ni wale waluokuja muda mfupi Kabla ya uchaguzi wa 2015, na kupewa nafasi kama Lowassa. Na mmoja kati ya waliorejea ccm ni huyo Lowassa. Nilisangaa sana Mbowe kupata ujasiri wa kugombea uenyekiti tena baada ya ile political blunder ya 2015! Mbowe alitakiwa kujiuzulu muda mrefu baada ya kete ya Lowassa kushindwa kuchukua urais.
 
Nitag kwenye post Mojawapo niliyounga mkono ule upuuzi boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…