Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Utaratibu wa kutetea kila maamuzi ya viongozi wa chama bila kuangalia faida au hasara zake ni mbaya sana.Kama Kuna kosa kubwa walifanya uongozi wa cdm ni kuwapokea wanasiasa maslahi wa ccm, the likes of Lowassa, Nyalandu, Msindai na takataka za aina hiyo. Mbowe angekuwa anajali uwajibikaji alipaswa kijiuzulu uenyekiti na kukiri kufanya makosa kwa kupokea hao wahuni, na kuwapa nafasi adhimu huko cdm.
Wapinzani wakifanya hivyo wanakuwa hawana tofauti na wanachama wa CCM.
Kuna kipindi mlikuwa mnatetea akina Mbowe kila kitu. Nikasema siwezi kuwa na chama kamwe. Siwezi kuwa katika kapu moja la 'collective imbecile' na kuburuzwa kama nyumbu.