Pre GE2025 Lissu ajibu tuhuma za kunyimwa gari pamoja na fedha na Rais Samia, asema hajawahi kuomba 'favour' yoyote kutoka kwake

Pre GE2025 Lissu ajibu tuhuma za kunyimwa gari pamoja na fedha na Rais Samia, asema hajawahi kuomba 'favour' yoyote kutoka kwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katika hili nimeanza kumuelewa Lissu amenyooka sana na katika hili atakuwa na maadui wengi ndani ya chama chake kuliko nje ya chama!

Mimi sio shabiki wa Lissu lakini kamwe awezi kuchukua rushwa!
 
Katika hili nimeanza kumuelewa Lissu amenyooka sana na katika hili atakuwa na maadui wengi ndani ya chama chake kuliko nje ya chama!

Mimi sio shabiki wa Lissu lakini kamwe awezi kuchukua rushwa!
Kwa hiyo gari aliyoomba sio kutaka rushwa?
 
Mimi nilitegemea kama Polisi wangemkamata Lissu kwa kuwatuhumu Abdul na Mama yake kutoa rushwa bila ushahidi!
Nadhani Polisi wakifikiria Mama na Abdul ni akina nani wanakwama!
Maana akina Abdul ni wengi mno!
 
Kumekucha 🐼🔥

Yawezekana Chadema tatizo ni Kubwa kuliko tunavyofikiri

Hasa nikikumbuka Polepole alivyomlipia faini Katibu mkuu wa Chadema by then Dr Mashinji

Na Shujaa akamlipia mchungaji Msigwa 😂
Kumbukumbu nzuri. Lakini, pamoja na hayo, kwa nini Mchungaji anachanganya akili? Sugu, anachanganya akili?
Nimesoma chizi mmoja anasema HECHE naye?

Mbowe alichanganya akili siku nyiki kwenye maridhiano, hili linajulikana.

Ndiyo maana sisi wengine toka mwanzo tukasema, "MTINDO" anaoutumia Samia kuwamaliza CHADEMA ni 'lethal' (sumu kali zaidi); kuliko ule aliokuwa akitumia Magufuli. Samia anabembeleza, anatumia sauti nyororo; "lugha za kistaarabu" huku akikunyonga na wewe unachekelea.
Kuna wengi sana ndani ya CHADEMA waliochotwa akili zote na mtindo wa huyu mama.

Natumaini kuna waliostuka mapema ndani ya chama hicho ili kukinusuru na sumu hii.
 
Lissu hana cha kupoteza hivi sasa anajua likiharibika ana kwenda kuishi mabanda ya maskini ubelgiji!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

Mlale Unono 😀😀
This is nonsense. mtu kakuibia shati lako, unamdai akupe shati lako, kwa vile ni mbabe anakataa. Unafika wakati shetani wake anapata upako wa Mungu kidogo, anakupa shati lako. Unamshukuru kwa lipi? yeye ndiye akushukuru kwa wewe kukubali kumsamehe na kupokea shati lako
 
Lissu hana cha kupoteza. Watoto wake ni raia wa Marekani huku yeye akiwa na hifadhi ya kudumu Ubelgiji. Watu kama kina Mdude ndo wataendelea kuteseka.
 
Tundu Lissu amejibu tuhuma zilitolewa dhidi yake kwamba anayoyasema kuhusu Rais Samia na mtoto wake Abdul kutoa pesa ili kuvuruga uchaguzi ndani ya CHADEMA.

Majibu hayo yamekuja baada ya member wa JamiiForums.com kuandika andiko likiwa na madai hayo

Pia soma: Inadaiwa hasira za Lissu zinatokana na kunyimwa gari na Rais Samia

Lissu amejibu baada ya kutafutwa na JamiiForums, ambapo amesema:

"Mimi sijawahi kuomba favour yoyote, narudia, yoyote, iwe ya gari au kitu kingine chochote kutoka kwa Rais Samia.

"Kitu pekee ambacho nimekidai kwake ni haki zangu za:
(a) Kupatiwa passport nyingine baada ya mwanzo kuibiwa;
(b) Kulipwa kiinua mgongo kwa muda niliofanya kazi ya Ubunge,
(c) Kulipwa stahiki za matibabu yangu baada ya shambulio la Sept 2017.

"Katika madai hayo, (a) na (b) yalitekelezwa kabla ya mimi kurudi nchini mapema mwaka jana, na nilisema hivyo hadharani. Madai ya fidia ya matibabu hayajalipwa hadi hivi sasa na nimesema hivyo hadharani mara nyingi.

"Tuhuma za rushwa hazina uhusiano wowote na kuvunjika kwa maridhiano. Mimi binafsi nimeanza kuzungumzia hadharani juu ya kukwama kwa maridhiano mapema kabisa ya mwaka jana.

"Nimezungumzia rushwa za Abduli na mama yake wiki mbili zilizopita. Wanaoamini kuna uhusiano wowote kati ya masuala haya hawajatumia vichwa vyao sawa sawa.

"Kuhusu ushahidi wa rushwa za Abduli na mama yake, ijapokuwa rushwa huwa haitolewi risiti, kuna ushahidi wa kutosha wa uwepo wa rushwa na mwenye macho haambiwi tazama!"

=====
Pia soma:
- Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul
Huyu jamaa anaendekeza tamaa na sio kingine ikumbukwe alimsifia Sana mama samia kipindi kamrudisha nchini na kumpa fidia zote ni mshamba na sio mtu wa kumkaribisha
 
Back
Top Bottom