View attachment 2991772
Tundu Lissu amejibu tuhuma zilitolewa dhidi yake kwamba anayoyasema kuhusu Rais Samia na mtoto wake Abdul kutoa pesa ili kuvuruga uchaguzi ndani ya CHADEMA.
Majibu hayo yamekuja baada ya member wa JamiiForums.com kuandika andiko likiwa na madai hayo
Pia soma: Inadaiwa hasira za Lissu zinatokana na kunyimwa gari na Rais Samia
Lissu amejibu baada ya kutafutwa na JamiiForums, ambapo amesema:
"Mimi sijawahi kuomba favour yoyote, narudia, yoyote, iwe ya gari au kitu kingine chochote kutoka kwa Rais Samia.
"Kitu pekee ambacho nimekidai kwake ni haki zangu za:
(a) Kupatiwa passport nyingine baada ya mwanzo kuibiwa;
(b) Kulipwa kiinua mgongo kwa muda niliofanya kazi ya Ubunge,
(c) Kulipwa stahiki za matibabu yangu baada ya shambulio la Sept 2017.
"Katika madai hayo, (a) na (b) yalitekelezwa kabla ya mimi kurudi nchini mapema mwaka jana, na nilisema hivyo hadharani. Madai ya fidia ya matibabu hayajalipwa hadi hivi sasa na nimesema hivyo hadharani mara nyingi.
"Tuhuma za rushwa hazina uhusiano wowote na kuvunjika kwa maridhiano. Mimi binafsi nimeanza kuzungumzia hadharani juu ya kukwama kwa maridhiano mapema kabisa ya mwaka jana.
"Nimezungumzia rushwa za Abduli na mama yake wiki mbili zilizopita. Wanaoamini kuna uhusiano wowote kati ya masuala haya hawajatumia vichwa vyao sawa sawa.
"Kuhusu ushahidi wa rushwa za Abduli na mama yake, ijapokuwa rushwa huwa haitolewi risiti, kuna ushahidi wa kutosha wa uwepo wa rushwa na mwenye macho haambiwi tazama!"
=====
Pia soma:
-
Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul
CHADEMA WAMKALIA KOONI LISSU NI MNAFIKI AOMBE RADHI - ASIJITOE AKILI
Kamati kuu CHADEMA imemuhoji Makamu Mwenyekiti na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Tundu Lissu kwa kuudanganya Umma kuwa haku kukubaliana na uamuzi wa kumwalika Rais Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika tarehe 8 Machi mwaka 2023.
Wakati Mwaliko huo kutoka CHADEMA kwenda kwa Mheshimiwa Rais ulijadiliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA na Lissu akiwa mjumbe alibariki ujio wa Samia kamati kuu.
Lissu ameulizwa na wana kamati Tarehe 6 Machi, 2023 wakati akihutubia kwenye mtandao wa Clubhouse alipongeza na kusifia kitendo cha BAWACHA kumualika Rais Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho yao ya Siku ya Wanawake Dunian.
Katika mahojiano hayo Tundu Lissu alienda mbali kupongeza kitendo cha Rais Samia kukubali mualiko kwa kusema, “Sikumbuki ni lini mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, ambae siku zote ni rais wa nchi, amewahi kushiriki katika shughuli rasmi ilioandaliwa na chama cha upinzani. Hasa chama kikuu cha upinzani. Wanakamati wanauliza je alikuwa amelewa..?
Tumewasilisha hapa Mawasiliano mbalimbali ya CHADEMA ambayo yamewekwa wazi yanaonyesha kuwa wajumbe pekee wa Kamati Kuu waliopinga rais kupewa mwaliko huo walikuwa John Heche na Godbless Lema.
Tundu Lissu alikuwa katika kundi la wanaokubaliana, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe. Hivyo wajumbe wameshangaa leo hii Tundu Lissu akitoka hadharani na kudai ya kwamba hakuafiki uamuzi huo. (Ni Mnafiki)
Wajumbe wamehoji Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi ambayo ilimpeleka hadi Brussels, Ubelgiji, ambapo wakati huo Tundu Lissu alikuwa akipatiwa matibabu zaidi na alifanya kikao na Tundu Lissu kwa ajili ya mazungumzo.
Kikao hicho kilikuwa cha faragha, lakini baada ya mazungumzo yao, Tundu Lissu aliingia kwenye mtandao wa kijamii Twitter na kuelezea mambo sita waliyozungumza na Rais Samia.
Kati ya hayo sita, viwili vilikuwa pamoja na Rais kuhakikisha kwamba Tundu Lissu anapata stahiki zake, kitu ambacho baadaye Tundu Lissu mwenyewe alikiri kilitendeka, pamoja na Rais kuhakikisha usalama wake pale atakaporejea nchini, jambo ambalo sote tumeona likitokea.
Wajumbe wamerejea historia Lengo ni kuweka rekodi sawa na kudhihirisha kwamba Rais Samia Suluhu Hassan hajawahi kuwa na migogoro binafsi na Tundu Lissu.
Tundu Lissu naye hakuwa na matatizo na Rais wakati ambapo rais alikuwa akijibu maombi yake mbalimbali. Hivyo, si ajabu kuona kwamba hadi mwaka jana, wakati CHADEMA ilipokuwa ikijadili kumwalika Rais, hawakuwa na shida yoyote kati yao.
Kilichotokea katikati ambapo Tundu Lissu alianza kumshambulia rais kibinafsi, Jambo ambalo limesemwa jana kuwa alinyimwa gari aina ya Nissan Y62 aliloliomba. (Chuki binafsi)
Tukirejea sasa swala la Tundu Lissu kudanganya umma na kudai kuwa hakuafiki Rais Samia Suluhu Hassan kualikwa kwenye sherehe zile, kwenye uongozi wa taasisi yoyote iwe ya serikali, chama au kampuni binafsi kuna kitu kinaitwa collective responsibility.
Maana ya collective responsibility ni kuwajibika kwa pamoja kwa maana ya kwamba jambo likisha jadiliwa na kukubaliwa kwenye vikao basi wote mnatoka na kauli moja inakuwaje Lissu atoke hadharani aseme hakubaliani walihoji baadhi ya wajumbe.
Uwajibikaji huu wa pamoja ndio sababu ambayo John Heche na Godbless Lema, ambao walikuwa wanapinga rais kualikwa, hawajawahi kutoka hadharani na kukosoa uamuzi huo.
Sasa pale ambapo Tundu Lissu, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya chama, na mtu mwenye ndoto za kuwa rais wa nchi hii, haielewi maana ya uwajibikaji wa pamoja, inatia wasiwasi ni aina gani ya rais angekuwa kama angepata ushindi katika uchaguzi wa 2020.
Na utovu huu wa kinidhamu na kuto kuheshimu taasisi ambayo yeye ni kiongozi muandamizi sio tu kwenye swala la mualiko wa rais.
Wanakamati kwa kauli moja wamemtaka Lissu kuandika barua ndani ya masaa 72 ya kuomba radhi.