Uchaguzi 2020 Lissu akishinda urais, nchi italipuka kwa shangwe isiyo ya kawaida

Hata asiposhinda tumefurahi tu kusikia akisema yale yalikuwa adimu kusikia- yaani ukweli kama ukweli
Well said, hata asipotangazwa kuwa ameshinda ila atakuwa ametoa fundisho. Labda dharau kwa wananchi ambao mamlaka yote yanatoka kwao itapungua kama siyo kuisha.
 
Mkuu 2015 na miak 5 baada ya utawala wa JPM ni tofauti sana. Watu wamefanyiwa ubabe uliopitiliza. Nchi imetawaliwa kwa matamko wa mtu sio sheria. Watu Kimara walivunjiwa nyumba zao wakati kuna zuio la mahakama kuu. Mahakama ikapuuzwa, nyavu sikachomwa moto na zimenunuliwa ndan ya nchi hii hii. Sas hivi watu wanamjua vzr. 2015 hawakumujua qalimjua JK. Hana kipya cha kiwadanganyia, asubili alichopanda kama Bukoba alivyofanywa
 
Nilitaka kuja na uzi wenye heading hii hii, hakika kumbe kuna wakati tunakuwa na mitizamo inayofanana, mkuu ahsante kwa bandiko! ni ukweli usiopingika kutakuwa shangwe ambalo halijapata kushuhudiwa ktk historia ya nchi hii.
 
Mkuu natamani sana kupata clip na kushuhudia kilichomkuta His Execelency huko bukoba
 
Wala Rushwa na wanyang'anyi watalipuka
 
 
Safari kuiba kura ngumu ndugu yangu, wewe mpigie jiwe lakini kawaambie na rafiki zako wizi wa kura safari hii ngoma nzito. Wasipotaka kutoka watatolewa kwa nguvu.
 
Yaani nitafanya kila njia nikampe mkono Mh Rais Tundu Lisu, Nitapanga safari ya kwenda Ikulu kama watanikamata poa tu, kama watanipiga basi yatakuwa maumivu ya raha maana napigwa huku namshangilia rais, Kama wataniua basi naamini ntakufa huku natabasamu, nafsi yangu italala kwa amaniiiiiiiii!
 
Itakuwa siku ambayo hata Mungu atalifuta giza kwa muda ili kila mtu amtukuze kupitia Lissu
 
Maalim akiapishwa kuwa rais Zanzibar, tunatangaza tarehe mpya ya uhuru, tunaachana na ile ya 1963/64... itakuwa 2020 October 29th 😀

Walioko bara nauli yenu tu, Zanzibar kila chochoro mtasikia harufu ya biriani, pilau na makeki kwa ajili ya kila mtu kufaidi.
 
Du umeongea maneno mazito Sana. MUNGU akupe haja ya Moyo wako bila kupigwa wala kuuawa.
 
Du umeongea maneno mazito Sana. MUNGU akupe haja ya Moyo wako bila kupigwa wala kuuawa.
Kweli kabisa, yaani kunawatu Mungu angeniwezesha japo nikasalimiana nao ningefurahi sana.

Kidunia- Baraka Obama
Afrika - PL Lumumba
Tanzania- Tundu Lisu.

Hao watatu tu Mungu angenikutanisha nao tu japo niwasalimie
 
Nishaiweka karibu ile nyimbo (pambio) “TUMEUOOONA, MKONO WAKO BWANA, UMETUTOA MBAAAALI, UMETUSHIKA MKOOONO”.. mtaa mzima naona watanijoin hapa nyumbani tuuimbe weee mpaka tuchoke. Na chakula itakuwa pilau tu wiki nzima. Tushereheke na majirani halafu tutajumuika kumtolea Mungu sadaka ya pamoja, maana wote tumejiapiza Lissu lazima awe Rais wetu Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…