LGE2024 Lissu Alitaka CHADEMA Ishinde uchaguzi Kupitia Kura ya Nani Wakati yeye Mwenyewe Hakupiga Kura?

LGE2024 Lissu Alitaka CHADEMA Ishinde uchaguzi Kupitia Kura ya Nani Wakati yeye Mwenyewe Hakupiga Kura?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ndugu zangu Watanzania,

Unajua kuna watu na wanasiasa hapa Nchini wanaweza kufikiri watu wote ni wajinga kama wao au watu hawana akili au watu hawajitambui au watu ni Manyumbu au kufikiria labda watanzania ni vichaa na mambumbumbu.

Hivi inaingia vipi akilini kwa mtu mwenye akili Timamu na anayejitambua vyema akamsikikiza lissu na malalamiko yake juu ya uchaguzi au kusikiliza kauli za kilaghai za watu aina ya lissu akiwadanganya wafuasi wake kuwa atashinda uchaguzi? Chama kitashinda vipi uchaguzi wakati viongozi aina ya lissu ndio wakwanza kutokupiga kura?

Nani atakipa kura chama ili kishinde? CHADEMA itashindana vipi na CCM iliyo fanya hamasa kubwa ya kuwataka wanachama,wafuasi na wakereketwa wake wakajiandikishe kwenye daftari la mpiga kura na kuipigia kura CCM katika sanduku la kura?

CHADEMA hii ya lissu itashindana vipi na CCM ambayo wanachama wake walikuwa wakipitiana majumbani kupelekana vituoni kwenda kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi? Vipi CHADEMA inaweza ishinda CCM hii ambayo muda wote ilikuwa ikizunguka kwa wananchi kusikiliza kero zao,kutoa majibu na kutatua kero zao?

Vipi CHADEMA hii ya lissu asiyepiga kura ikapata ushindi mbele ya CCM ambayo wanachama wake waliinuka kwa wingi kwenda kupiga kura asubuhi na Mapema wakati yeye Lissu amelala zake nyumbani kwake? Huo ushindi kwa CHADEMA utatoka wapi? Kwa miujiza ipi?

CHADEMA hii ya lissu iliyokuwa ikiokoteza wagombea dhaifu inaweza vipi ishinda CCM ambayo ilikuwa na maelfu ya wagombea waliojiandaa kisawasawa na kwa sera nzito nzito kuomba uteuzi wa chama? CHADEMA hii ambayo ilikuwa haina uwezo hata wa kupiga kampeni nchi nzima inaanzia wapi kuishinda CCM katika sanduku la kura hata kama ingetokea tume ya uchaguzi kutoka Marekani kuja kusimamia uchaguzi huu?

CHADEMA hii isiyo na viongozi wala ofisi wala uongozi ngazi za chini huko inaweza vipi ishinda CCM yeye mtandao wa uongozi mpaka huko vitongojini?

Halafu bila aibu wala hata unaona mtu anajibetua mdomo wake na kusema kuwa CCM imeiba uchaguzi imeiba kutoka wapi wakati hata kura huna? Hapo hapo mtu kama zito aliyefirisika kisiasa anasema eti wawasusie viongozi hawa waliochaguliwa .

Unaweza vipi msusa mwenyekiti wa mtaa? Utapata wapi barua ya utambulisho unapotaka barua yoyote ile kwa mtendaji wa kata au mtaa wako?utapata wapi barua ya utambulisho unapotaka kumwekea mdhamana ndugu yako huko polisi ambapo ukienda kwa mtendaji wa mtaa atakutaka uwe na barua ya utambulisho? Utapata wapi barua ya utambulisho ukitaka kufanya biashara yoyote ile wakati unafuatilia leseni yako halmashauri? Ukienda kwa mtendaji wa mtaa ni lazima uwe kwanza na barua ya utambulisho mkononi mwako.

Sasa utawasusa vipi watu hawa? Kwa ufupi ni kuwa viongozi wetu hawa wa mitaa na vijiji ni kama Maji usipoyanywa utayaoga tuuu.

CCM ni Mbele kwa mbeleeeee.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Halafu wewe bwabwa siku ya siku lazima tuzae na wewe jichetue unajiona wewe ni CCM zaidi kuliko hata CCM yenyewe.
 
Lucas Kuna wakati Unapeleka Wapi Akili?
Kwahyi Lissu Alikuwa Na Ruhusa ya Kupiga Kura Tanzania Nzima Kila Kitongoji??

Au Alikuwa Na Kura Ya Veto Nchi nzima??
Ndio akili zenu hizo CHADEMA? Kwa hiyo hamtambui umuhimu wa kura? Vipi kama wafuasi wa CHADEMA waliamua kufuata mfano wa Lissu wakutokwenda kupiga kura? Lissu kama kiongozi ametoa mfano gani na taswira ipi kwa kutokupiga kura?
 
Mimi nilijiandikisha, ila katka kijiji changu hakukuwa na mgombea wa chama chochote kile tofauti na ccm. Sikupiga kura na kutokana na hakuna umaana wa kachangua mtu ambaye ni mmoja.
 
Wewe sasa na luca ndio mnao hitajiwa zaidi na chadema kama alivyohitajika mchungaji,akina mwita na slaa ,sasa karibuni upande wa pili iwapo kweli mna nia ya ujenzi wa kweli wa taifa letu.
Kujenga Taifa ni wajibu wa Kila raia awe mwanachama au hapana ,hakuna haja ya kuwa Chadema.

Hoja ya Zito izingatiwe,CCM wasiwasogeze vyombo vya Dola kwenye siasa wakionja utamu watakuja kuigeuka na CCM na kuitumbukiza Nchi kwenye Tawala za Kijeshi ambazo Huwa hazijali na Wala huwezi kuzikosoa.
 
Embu kaa kwa kutulia huko.
Wewe jifanye ni CCM kuliko CCM yenyewe ipo siku yako. Uchaguzi umevurugwa na ndugu zetu wameuwawa halafu unaleta kejeli shauri yako unafikiri kuna mtu atakuja kukutetea siku ukibananishwa. Wenyewe wenye CCM yao wametulia wanajua ushenzi waliofanya maana yake ni nini wewe kidampa ndiyo unajitia kifua mbele shauri yako watu wana machungu.
 
Wewe jifanye ni CCM kuliko CCM yenyewe ipo siku yako. Uchaguzi umevurugwa na ndugu zetu wameuwawa halafu unaleta kejeli shauri yako unafikiri kuna mtu atakuja kukutetea siku ukibananishwa. Wenyewe wenye CCM yao wametulia wanajua ushenzi waliofanya maana yake ni nini wewe kidampa ndiyo unajitia kifua mbele shauri yako watu wana machungu.
Wala usinitishe kitu .ungekuwa unajiamini ungekuwa unaongea na mimi ukiwa kwenye majina yako halisi.lakini una piga mayowe ukiwa kwenye fake Id.Naona mmezoea kufanyiana uhuni na umafia ndio maana unataka kunitisha na mimi ukifikiria ni mjinga jinga kama wewe
 
Wala usinitishe kitu .ungekuwa unajiamini ungekuwa unaongea na mimi ukiwa kwenye majina yako halisi.lakini una piga mayowe ukiwa kwenye fake Id.Naona mmezoea kufanyiana uhuni na umafia ndio maana unataka kunitisha na mimi ulifikiria ni mjinga jinga kama wewe
Sikutishi nakuonya tu wenzako wana ulinzi 24/7 na haweleti nyodo kama wewe shauri yako.
 
Sikutishi nakuonya tu wenzako wana ulinzi 24/7 na haweleti nyodo kama wewe shauri yako.
Huna lolote lile dogo.ujinga tu ndio unakusumbua hapa. Kama unajiamini ungetikeza kwa jina lako halisi. Naona huko upinzani mmezoea kumalizana na kutishiana mpaka sasa umenogewa na kujifanya unataka utishe na watu wasiotishika kama mimi.huna akili kabisa.
 
Back
Top Bottom