LGE2024 Lissu Alitaka CHADEMA Ishinde uchaguzi Kupitia Kura ya Nani Wakati yeye Mwenyewe Hakupiga Kura?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hata CHADEMA wenyewe wanajua kabisa kuwa wameshindwa kihalali kabisa kutokana na kutofanya maandalizi
2020 Chadema ilishiriki uchaguzi mkuu wa Raisi,Wabunge na madiwani bila tume huru wakilenga maslahi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa hakuna maslahi japo msingi ni serikali za mitaa.
Maandalizi yangeanzia kwenye mitaa ndio chimbuko letu sote.
 
2020 Chadema ilishiriki uchaguzi mkuu wa Raisi,Wabunge na madiwani bila tume huru wakilenga maslahi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa hakuna maslahi japo msingi ni serikali za mitaa.
Maandalizi yangeanzia kwenye mitaa ndio chimbuko letu sote.
Mkuu hakuna tume huru hapa tume inakuwaje huru iko chini ya chama
 
Mkuu hakuna tume huru hapa tume inakuwaje huru iko chini ya chama
Ni nadra kumkuta mtu mwenye madaraka atake na wewe mgawane huo ulaji.
Ni jukumu la yule myonge nae kuchachamaa kudai kitumbua chake.
Wanyonge hao watakapopaza sauti kwa umoja wao ndio bwana mkubwa yule atafungua milango ya riziki kwa wasio na kitu sababu ya shindikizo.
Bila kushiriki uchaguzi ukapambana kisawasawa ndani ya michakato ya uchaguzi,ukabaki kulalamikia nje ya ulingo utachelewa sana.
Na kama anaekuchelewesha kupata haki yako ni chama chako vunja uongozi huo simika uongozi mpya,KUFA KWA DEREVA KUFA KWA MAKANGA usemi wa Kenya.
 
Hapa sululisho ni KATIBA MPYA
 
Hapa sululisho ni KATIBA MPYA
Katiba mpya hailetwi mezani kama tuzo la Miss Tanzania.
Katiba mpya inapiganiwa kushoto kulia,fang fang hadi kieleweke,mchakato wake hauna mapumziko.
Katiba mpya haitokani na utashi wa watawala bali watawaliwa.
Katiba mpya sio kama shule za wenye nazo,unafuliwa hadi nguo za ndani,mchakato wa katiba mpya ni sawa sawa na kuku wakienyeji anavyolinda na kulisha vifaraga vyake hadi viweze kujitegemea.

Yawezekana wananchi wengine hawajui kuwa bila class struggle hatuwezi kusogeza demokrasia kwa wananchi walio wengi.Kila jambo lina mwanzo.
 
Acha usukule
 
Luca,acha kuandika vitu usivyovijua na wala siyo upunguze.Hivi,huwa unawachukuliaje watu wewe hasa humu JF?Kwa hiyo CCM imeshinda,siyo?
 
Luca,acha kuandika vitu usivyovijua na wala siyo upunguze.Hivi,huwa unawachukuliaje watu wewe hasa humu JF?Kwa hiyo CCM imeshinda,siyo?
CCM Imeshinda na ndio maana imetangazwa kuwa mshindi na kuwafanya watu kulipuka kwa shangwe huku wakibubujikwa na machozi ya furaha
 
Mkuu hakuna cha kujifunza,tujifunze nn figisu au,naamini kama ww ni MTANZANIA kabisa tukiweka pembeni uchama yanayoendelea mwenyewe unaona
Naona kuendelea kupotea kwa vyama vya upinzani.kutokana na kukosa sera na ajenda zenye kugusa Maisha ya watu
 
Tatizo CCM hawataki Katiba mpya kwa vile ndiyo itakuwa mwisho wao kutawala wanatumia mabavu ya vyombo vya dola kuzuia upatikanaji wa Katiba mpya. Suluhisho ni Mapinduzi ya kijeshi tu.
Naona umevurugwa na kuanza kuropoka ropoka tu hapa kama mlevi wa gongo. Utapinduliwa wewe kichwa chako ili kikae sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…