Pre GE2025 Lissu: Aliyeshika chupa ya damu nikipelekwa Nairobi ni Msigwa (sio Mbowe)

Pre GE2025 Lissu: Aliyeshika chupa ya damu nikipelekwa Nairobi ni Msigwa (sio Mbowe)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hizi habari za chadema zimeshika kasi humu... kwani kunanini?!
Chadema inapendwa sana. Kwahiyo muda wote iwe makini sana ktk harakati na kazi zake. Kosa dogo tu linageuka kuwa nongwa kwa wananchi. Watu wameichoka ccm hivyo matumaini yao yako chadema, hivyo ikizingua inaumiza watu wengi sana
 
😂 😂 😂
Kwani Mbowe alishwahi kusema yeye ndio aliyeshika CHUPA?
Halafu harakati za Lissu sasa hivi anazifanya kwa kivuli cha chama gani?
Hebu wana JF muwe na Fikra pevu basi.
Aliyesema hivyo ni Godbless Lema
 
Wacha wagawane mbao. Hizi siasa siyo za kuzishabikia sana. Ni vitengo tu vya watu kujipatia riziki.
Siku si nyingi lile swali la kila mtanzania kuhusu upotevu wa mabillion ya join the chain litapata jawabu
 
Siasa sasa zimehamia kwenye chupa ya damu!!!
 
Chadema mlisha toana uhai na bado mnataka kushambuliana tena, hivi kugombea Uenyekiti Chadema Taifa kumbe ni kosa la jinai? Mbowe amekuwa Mungu mtu huko kwenu? Aiseee, hiki ni chama au kampuni ya biashara? Mnatia aibu sana, eti chama cha demokrasia? Hivi mnajua hata demokrasia ni nini?
 
Hujaelewa hoja yangu na umekurupuka kunipa quote, nimeuliza hivi Kwani Mbowe alishawahi kusema Yeye ndiye aliyeshika CHUPA ya damu?
Mjomba wake Lema ndio anaesem hivyo na Mbowe hakuwahi kukabusha
 
😂 😂 😂
Kwani Mbowe alishwahi kusema yeye ndio aliyeshika CHUPA?
Halafu harakati za Lissu sasa hivi anazifanya kwa kivuli cha chama gani?
Hebu wana JF muwe na Fikra pevu basi.
Kwa mara ya kwanza naanza kupata wasiwasi na uwezo wa Mheshimiwa Lissu katika namna kuendesha siasa zake.

Ni wazi tena pasipo shaka Lissu hadi kesho ni mgombea uRais wa Chadema lakini njia anayoitumia hakika hatofika mbali wala hawezi kushinda uRais iwapo atakuwa sehemu ya vurugu ndani ya chama chake.

Kumbe Lissu ni mjinga sana.Katika siasa huwezi kusonga mbele kama unajiweka ktk eneo la vurugu ndani ya base yako mwenyewe.
 
Mbona hizi habari za chadema zimeshika kasi humu... kwani kunanini?!
Tena zikiwalenga Tundu Lissu (M/M/Kiti) na Freeman Mbowe (M/Kiti).

Hawa wengine kina Msigwa, Sugu, Lema, Heche and others wanaingizwa katikati hawa wabaya wao wakiota kuwa propaganda zao zinaweza kuaminiwa na kuwagawa CHADEMA.!

Hii kitu miaka yote imefeli. Sijui ni kitu gani kinawafanya CCM waamini kuwa ujinga na upumbavu huu wanaoufanyaga miaka yote unaweza kufanikiwa kufarakanisha viongozi wakuu wa CHADEMA na mwisho kukisambaratisha chama kama walivyofanya kwenye vyama vingine NCCR - Mageuzi, TLP na CUF miaka hiyo

Kwa hiyo hii isikushangaze. Haya ma-CCM yanakuwaga hivyo miaka yote kila msimu wa chaguzi ndani ya chama na chaguzi zingine za kitaifa unapofika ikiwa ni jitahada zao kuleta mafarakano kisha ikibidi chama kipate viongozi mamluki wa CCM na wao wafanikishe malengo yao ya kutosumbuliwa na nondo za kina Tundu Lissu.

Asante kwa Freeman Mbowe. Huyu jamaa siku zote yuko very strong. Angekuwaga anataka mabilioni ya CCM, angeshayachuaga miaka mingi iliyopita, akawekeza kwenye biashara zake na kuiacha CHADEMA mikononi mwa mamluki wa CCM. Huyu jamaa ndiye patriot halisi huyu. Yuko tayari kupoteza vyake kwa ajili ya wengi.

Na bahati mbaya kuwa ma - CCM hawajui tu jinsi ambavyo Tundu Lissu na Freeman Mbowe zinaiva na kwamba, hakuna anayeweza kuwagombanisha au kuwatenganisha. Na bahati nyingine kuwa ma - CCM hayamjui vyema Tundu Lissu!!
 
Kumbe Lissu ni mjinga sana.Katika siasa huwezi kusonga mbele kama unajiweka ktk eneo la vurugu ndani ya base yako mwenyewe.
Ujinga wake ni nini? Unaweza kufafanua ukitaka na kama unaujua kweli===

Yaani wewe unaweza kulinganisha ujinga wako na wa Tundu Lissu kiasi cha ku - conclude kuwa yeye (TL) ni mjinga kuliko wewe? Really?

Ooh, wewe Ngongo wewe........Kweli??
 
Nafikiri ulimaanisha Lema anasema uongo ni muongo, uzuri Lissu ameshaweka clear kila kitu.
Lissu hakuwa na fahamu,Mbowe kaweka kila kitu wazi sijui kwanini unapenda ligi.

Mtoa mada kapotosha.Mod ikiwapendeza pandishe clip ya Jokakuu kuondoa sintofahamu.
 
Back
Top Bottom