Mbona hizi habari za chadema zimeshika kasi humu... kwani kunanini?!
Tena zikiwalenga Tundu Lissu (M/M/Kiti) na Freeman Mbowe (M/Kiti).
Hawa wengine kina Msigwa, Sugu, Lema, Heche and others wanaingizwa katikati hawa wabaya wao wakiota kuwa propaganda zao zinaweza kuaminiwa na kuwagawa CHADEMA.!
Hii kitu miaka yote imefeli. Sijui ni kitu gani kinawafanya CCM waamini kuwa ujinga na upumbavu huu wanaoufanyaga miaka yote unaweza kufanikiwa kufarakanisha viongozi wakuu wa CHADEMA na mwisho kukisambaratisha chama kama walivyofanya kwenye vyama vingine NCCR - Mageuzi, TLP na CUF miaka hiyo
Kwa hiyo hii isikushangaze. Haya ma-CCM yanakuwaga hivyo miaka yote kila msimu wa chaguzi ndani ya chama na chaguzi zingine za kitaifa unapofika ikiwa ni jitahada zao kuleta mafarakano kisha ikibidi chama kipate viongozi mamluki wa CCM na wao wafanikishe malengo yao ya kutosumbuliwa na nondo za kina Tundu Lissu.
Asante kwa Freeman Mbowe. Huyu jamaa siku zote yuko very strong. Angekuwaga anataka mabilioni ya CCM, angeshayachuaga miaka mingi iliyopita, akawekeza kwenye biashara zake na kuiacha CHADEMA mikononi mwa mamluki wa CCM. Huyu jamaa ndiye patriot halisi huyu. Yuko tayari kupoteza vyake kwa ajili ya wengi.
Na bahati mbaya kuwa ma - CCM hawajui tu jinsi ambavyo Tundu Lissu na Freeman Mbowe zinaiva na kwamba, hakuna anayeweza kuwagombanisha au kuwatenganisha. Na bahati nyingine kuwa ma - CCM hayamjui vyema Tundu Lissu!!