Lissu ameisha upepo upo kwa Makonda, Makonda anafanya siasa zinazogusa jamii moja kwa moja tofauti na Lissu Ndio Maana anagain popularity siku zinavyozidi kwenda
Umeandika mambo makubwa sana ama kwa kuelewa ama kwa kutoelewa.
Ni kweli kabisa kuwa Nchi yetu inaongozwa kwa UPEPO, tena UPEPO WA USANII.
Na hii ni aibu kubwa sana kwa Taifa letu.
Jamii ijiulize, hizo KERO zinazotajwa kwenye Majukwaa kwa kupigia simu Mawaziri zimeletwa na CHAMA KIPI hapa Tanzania?
Upuuzi unaofanyika wa kuwapigia simu Mawaziri, na Mawaziri wanavyo jinyenyekeza (kwenye simu), kunatatuaje KERO zilizoletwa na CCM?
Kwa nini CCM inafikiri kwamba Watanzania ni Wapumbavu wasioweza kutofautisha USANII na Utatuzi wa KERO zao?
Kama CHADEMA wataenda kushughulikia Vyeti (vya kughushi) vya mtu mmoja, watakuwa wamefeli sana.
Chadema wanatakiwa wamtumie huyo mwenye Vyeti vya kughushi kuwathibitishia Watanzania kuwa CCM IMESHINDWA KUONGOZA NCHI YETU, kiasi kwamba, hata mwenye VYETI VYA KUGHUSHI ameona hayo mapungufu makubwa, na Mawaziri, tena Mawaziri wasomi wanakiri hadharani kila wanapopigiwa simu.