Wakuu,
Wanatumia mbinu zile zile, kila jambo kubwa (lenye maana) likitokea lazima kizuke kitu, Makala alipotoa boko la kutishia usalama wa taifa na Ebola huku la Siglada likazuka, likapelekwa hadi muda wa ripoti ya CAG. Jana Lissu amekamatwa chaaaap saga la Manara na twiga wake likawa motooooo!
Vile vile wakati Mashehe walipoachiwa na kukamatwa tena, CHADEMA wakiwa moto na No Reforms No Election, na Dkt. Slaa ndio alikuwa ameachiliwa na kuongelea na kungelea kuhusu Reforms za CHADEMA hapo ndipo swala la Nicole Joeberry likapamba moto.
FOCUS! FOCUS Watanzania, turudi kwenye mambo ya maana yanayoathiri maisha yetu, uhuru wetu na uchumi wetu. Kunapotokea uonevu Watanzania bila kijali chama chako, ama kama wengine wenye hatuna chama piga kelele, kemea unyanyasaji na dhuluma inayofanywa kwa wananchi.
Leo inatokea kwa Lissu kesho anashikwa mtu wako wa karibu au worse wewe mwenyewe, muda wa kupiga kelele ni sasa. Huo umbea weka pembeni kwa sasa. Tusisahau ripoti ya CAG itaenda bungeni soon, ni muda wa kupigania maslahi yetu, muda wa kuonesha nguvu ya umma.
Pia soma >
Pre GE2025 - Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma