Pre GE2025 Lissu amjibu Wenje, asema aliudanganya umma kuhusu suala la Abdul

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu kwa mara ya kwanza kabisa wakati anaongelea suaka hili la Abdul alisema: ' nilimwambia mwambie mama yako anilipe pesa zangu za matibabu'. Abdul alipojibu kuwa amelipwa yeye Lissu alisisitizz kuwa hajalipwa na kumpa nakala yake ya barua ya madai ili ampelekee Mama Abdul ili alipwe kama kweli ana nia ya kusaidia.

Sasa Lissu anaporuka kuwa hawakuzungumzia kuhusu hela za matibabu wala hakumtuma Abdul basi Lissu anadanganya.
 
Nenda uko mtu akiwa msema kweli kuwa kuna pesa chafu zinaingia ndani ya chama basi afukuzwe uwanachama
Kakwambia shilingi ngapi zimeingia? Kakwambia zimeanza kuingia leo? Mwaka 2010 wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu gazeti la Raia Mwema (sikumbuki toleo) lilitoa taarifa ya kuhamisha miamala ya pesa ya mamia ya mamilioni kutoka kwenye akaunti za Mbowe za Mbowe kwenda kwenye akaunti zake za nje ya nchi.

Just imagine kwenye kipindi cha kampeni Mbowe anahifadhi fedha nje ya nchi!! Lissu huyu huyu na Wana Chadema kibao walimtetea Mbowe kuwa ni bilionea na ana haki ya kuwa na fedha na kuziweka popote anapotaka! Leo amekuwa mtu wa pesa chafu? Ahahahahaha!!!
 

Toeni video ya kikao cha kamati kuu , acheni longolongo
 
Nenda uko mtu akiwa msema kweli kuwa kuna pesa chafu zinaingia ndani ya chama basi afukuzwe uwanachama
Ndivyo ilivyo Bongoland !
Huwa tunafunzwa kusema uongo tangu tukiwa watoto !
Kwa mfano unawaambia wanao Yule anayenidai akija mwambieni nimesafiri !
Kisha mzee anaingia chumbani kulala !
 
Mmmh ! Bongoland, Bongolala !
Chochote kinawezekana !
 
Hicho chama kili survive kwa kuwa Mwenyekiti alikuwepo, tabia yake ya kukimbia kimbia nje ya nchi kila akipata changamoto kidogo, kuna siku chama kitakosa mwenyekiti kwa muda usiojulikana.
 
Kwa wana-Mwanza tunakumbuka vizuri uchaguzi mkuu wa 2010. Kama sio nguvu ya watu kushinikiza matokeo yatangazwe, Wenje alikuwa ameshakubali kupokea mlungula kutoka kwa Lau Masha. Kwa hiyo sishangai Wenje kuhusika na tuhuma za rushwa namna hii.
 
Mbona jana amefafanua vizuri tu kuwa hajakana kumpa Abdul documents zake alichokuwa anakataa ni kauli ya Wenje kuwa motive ya safari yao na Abdu kwenda nyumbani kwa Lissu ilikuwa kumsaidia kulipwa fedh anazoidaia Serikali. Nia ya safari ya Wenje na Abdul kwenda kwa Lissu ilikuwa kumhonga ili asiebdelee kumsema vibaya kwenye majukwaa na Lissu alimtolea nje Abdul kwa kumwambia hiyo hela yake (Abdul) haitaki laikini kama anataka kumsiadia amwambie mama yake amlipe hela anayoidai Serikali,Abdul.alimjibu kuwa Samia anasema bado hajapata nyaraka za madai hayo ndipo akampa nyaraka hizo. Mbona maelezo haya yamenyooka vizuri tu.
 
Ndugu yangu hela ya Abdul hawezi kukusaidia ukatoe sadaka kwenye nyumba za ibada ama vituo vya mayatima ipo kwa ajili ya wanasiasa na waandishi wa habari wampambe vizuri mama yake azidi kumega mkate wa Tanganyika.. ukitaka hela ni simple tu toboa/ kata uzio wa mgodini Mwadui uingie "Bubeshi" ukachote ng'ana.. utakuwa tajiri ununue Nyankole nyingi.
 
Umetisha ndugu Hahaha 🤣
 
Mimi nafikiri salama ya Chadema kama chama Cha siasa ni KUMFUKUZA LISSU uwanachama aidha kabla ya uchaguzi ili asiwaharibie chama au baada ya uchaguzi ili wabaki salama baada ya uchaguzi. Sababu Kuu ni kwamba "Mtu mstaarabu haropokiropoki!".
Anayetakiwa kufukuzwa au kusimamishwa ni Wenje, kwa chama makini na kwa mtu makini anayehubiri uwajibikaji kwanza anatakiwa hata ajiondoe kwenye kinyang'anyiro cha Umakamu M/kiti maana akiendelea na akishinda inamaana chama wamekiuza kwa wapenda Rushwa. Na Mh Lissu ameweka wazi taarifa hizi ili wanachadema waamue kama wana mkabidhi chama mla rushwa au wanamkataa, na kama kiongozi yeyote wa juu anamsapport inamaana Lao ni Moja.
 
Siwezi kuwa Mwana CCM halafu nikawa nyumbu. Nyumbu ni ninyi Chadema. Mlimfanya Mbowe kama Mungumtu leo mnamshangaa kujiona Mungumtu! Ahahahahaha!!!
Sijawahi kuwa chadema Wala CCM ila machawa hasa wa kiume mnajudharilisha sana
 
Mimi nafikiri salama ya Chadema kama chama Cha siasa ni KUMFUKUZA LISSU uwanachama aidha kabla ya uchaguzi ili asiwaharibie chama au baada ya uchaguzi ili wabaki salama baada ya uchaguzi. Sababu Kuu ni kwamba "Mtu mstaarabu haropokiropoki!".
Kwahiyo hamtaki watu wakweli wawepo?, haya ni matokeo ya kukuzwa kiwiziwizi
 
Mnajua kujitoa ufahamu nyie watu, au kama sivyo basi una uelewa mdogo na akili ndogo sana
 
Hayo yote kayazungumza kwenye hizo audio. Tatizo hujasikiliza audio.
 
Lisu Domo kwabwa lzma awe na njaa zaid ya kiongozi yyte ndani ya Chadema tatizo ajapata njia za kuchukua iyo mifeza kaona Wenje pengine atajua yeye akitaka cake kubwa zaid ndio akaona Asuse akidhani atatafutwa pekeyake. Kaona kimya ndio kaona amwage mboga!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…