Idadi ya wagombea wa CCM inashinda hao wanayo vumisha, Maelfu wampokea Lissu. Lakini kitendo cha CCM kujivunia jezi zao mtaani ni ishara nyingine awamu ya 5 kazi ccm wameifanya. Odinga hapo Kenya kuna picha ya mtandaoni kavaa shati la jezi ya CCM.
Lissu anajitahidi sana kuongea maneno ya kukera na kuudhi dhidi ya Rais Magufili, lakini kasahau JPM ni master of human psychology, anamuangalia kamchunia. Lissu anabakia kuteseka nini kinachopikwa. Hanabudi kusubiri mpaka muda ukifika atapakuliwa.
Lissu anamadhaifu mengi mno katika hizi kauli zake za upayukaji na ndio maana ukitulia na ukawa makini kumtuliza ni rahisi sana.
Lakini ni muhimu wakati ukifika Lissu na umeshafika ni sasa aambiwe ukweli, wala msimdanganye hamna namna ataweza shinda uchaguzi huu. Hilo haliko, asiachiwe tu uwanja na kuangaliwa tu akiulaghai umma na mataifa mengine ya nje kuwa anakubalija na kesha shinda. Wakati wa kura akishashindwa kihalali ataleta matatizo yale ambayo wameshapanga na mabeberu ya kuitisha maandamano ya kuhamasisha uasi.
Kwangu mimi naona si sawa huyu aachiwe kuongea kila anachojisikia kuongea na kila anachotaka kuwaaminisha wale wanao msikiliza hata kama ni uongo na upotoshaji. Uongo ukaachwa kukanushwa na ukaendelea kuongelewa kwa kurudiwa rudiwa hugeuka na kuonekana ndio ukweli huo. Hivyo ni vizuri mbinu za kukabiliana na huyu anaye ongea kauli za kuandaa waasi watarajiwa akabiliwe mapema kabla ya kuanza kukumbuka shuka wakati kumesha kucha. Makosa haya yalifanyika awamu iliyopita kukatokea mapinduzi ya kutumia pambio la chama ingawa baadaye yalizimwa. Lissu si wakumchekea.