Pre GE2025 Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'

Pre GE2025 Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Baada ya kupitia maoni mbalimbali kumhusu yeye, nahitimisha kusema kwamba, Mh Tundu lissu, hafai kuaminiwa na wanachi katika nafasi ya Urais
Baada ya kusoma yote huko juu, hadi kwenye mstari huu,; nami nime jiridhisha kwamba ulipo jiandaa kuandika mada hii, tayari nawe ulikuwa umejihesabu kwenye hao "mahiri" wenzako ulio wataja. Hapakuwa na sababu yoyote ya kuja hapa na kudanganya wasomaji kuhusu msimamo wa "mahiri" nyinyi.

Mahiri, ni akina nani hao akina Yericko? Kipimo chako cha umahiri ni hafifu sana, bila shaka ndio sababu na wewe unaonekana kuwa hafifu sana.

Sasa ngoja nikamalizie sehemu ya pili ya andiko bovu ulilo weka hapa tulijadili..
BTW: sina kumbu kumbu ya kukusoma popote ndani ya JF kabla ya hili bandiko lako la leo. Sijaona lolote la kunifanya nione umahiri kwako.
 
Kama hafai kuongoza chama chenu kwa kuwa hana hekima.

Mbona mlitaka aongoze NCHI nzima? Kipi kikubwa NCHI au chama? Kipi kina hitaji busara zaidi?

Je mko tayari kuliomba taifa radhi kwa kosa hilo?
 
Kwa lugha zinazotolewa na wafuasi wa mbowe SI za kuijenga umoja ndani ya chama kamwe, mbowe ni vizuri akakaa nao.Kumdhihaki lissu kisa kugombea nafasi ya mwenyekiti sio sawa
 
Mh Tundu lisu ni JPM aliyechangamka aishie kwenye nafasi aliyopo na akienda sana, aishie kwenye kuongoza Wizara tu
Kwa hiyo "unguli" wenu unaishia hapa!
Sijaona hoja hata moja katika mada uliyo leta hapa inayo stahili kujibiwa Huo "unguli na umahiri" mnao jivalisha ni wazi hamna sifa hizo, wewe pamoja na hao ulio wataja. Ni watu wenye njaa tu mnao hangaikia milo ya kila siku.
Nchi hii mmeigeuza kuwa ya kijuha sana; ndiyo sababu hata watu wa aina yenu sasa mnajitambulisha kuwa "nguli".

Sikumbuki kuwahi kukusoma popote humu JF. Baada ya kusoma haya uliyo andika humu, sioni sababu tena ya kupoteza muda kila nikikutana na maandishi ya "kinguli" unayo leta humu.
 
Trump unamchukulia poa? Ndiyo hivyo wamarekani wanamwelewa sasa.
Haya mmeyajua baada ya kusema anagombea nafasi ya kuwa mwenyekiti au?
Lissu aliyekuwa mbunge wa jimbo kwao huko Singida. Elimu yake wala haikuleta mabadiliko kwa jimbo lake tena zaidi ya kipindi kimmoja,aka Mr deep promise without a success.

Call a spade a spade not a big spoon.
Hon Lissu hana kitu cha ku proof kwa wananchi wake waliompeleka bungeni.

Vivyo hivyo akiwa Mwenyekiti wa
Chama cha wanasheria hakuweka kitu tangible.Au labda hajui Latin?NADA ni kireno tutakutana kwenye.....

Na hata katika chama chake alionekana kituko alipigwa vibaya bila kunywa maji almost nill.Hakujua Mjomba Magu alikuwa ndio kidume cha Bongo.
Nadhani Chadema leta Barongo type wanaume wa vitendo sio wachumba.
 
Kuna shuuma nzito dhidi ya Lisu zimeandikwa na Yericko Nyerere ambazo Lisu anapaswa kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi ama aombe radhi.
1. Kusema kuwa hajalipwa hela yake ya matibabu kumbe kalipwa.
2. Madai kuwa Abdul alienda nyumbani kwake kumhonga wakati kumbe alikuwa anamsaidia kufanikisha malipo ya matibabu yake.
3. Kupewa nafasi kubwa ktk chama lkn hazitendei haki

Lisu anapaswa kutoka hadharani na kujisafiaha ama kuomba radhi.
Sasa katika yote hayo uliyo orodhesha hapo, kuna lipi la maana sana ambalo lina mlazimu Tundu Lissu ajitokeze kulijibu?

Chukulia kama hiyo namba 2. Abdul anao wadhifa gani ndani ya serikali hadi awe yeye ndiye mpigania haki za Tundu Lissu? Kuna sababu zozote za kumfuata nyumbani kwa jambo kama hilo?

Hiyo namba tatu, hata haieleweki unayo maana gani?
Hivi watu wenye akili timamu nao sasa wanageuka kuwa machizi kwa sababu tu Tundu Lissu kajitokeza kutaka nafasi ya kuongoza chama?
 
Chama kimekosa ubunifu na kimepoteza ushawishi kwa makundi mengi hasa vijana, wanaishi kwa mazoea. Mfano halisi ni idara ya vijana Bavicha, nilitarajia idara hii iendeshwe kisasa kuvutia vijana wengi kuingia kwenye chama, lakini kimezima ni tofauti na wakati alipokuwa Heche, sasa hivi unaweza sikia uVCCM zaidi kuliko Bavicha.

Hiyo ndio sura hadi kwenye uongozi wa juu, kumedumaa, hamna jipya, watu ni walewale pamoja na failures nyingi, hakuna anawejabika kwa kisingizio cha kuonewa na CCM mda wote.

Wakisema mwamba tuvushe, wanamaanisha vusha familia zetu na maslahi yetu, sasa hivi kila aliyewahi kuwa Mbunge Chadema anafikiria kurudi tena bungeni, hii inamaana hakuna nafasi kwa wengine kujaribu na kupewa nafasi za uongozi. Nimeona hili kwa Professor Jay na wengine wanaona hizo nafasi ni kwaajili yao pekee.
 
Nafasi ambayo, inahitaji watu watulivu, waliojaa hekima na maamzi yasiyo ya kukurupuka, nafasi ambayo kwa neno moja tu la mkuu wa nchi, linaweeza kuhatarisha usalama wa nchi na wananchi
Watu wa namna hii viongozi wa chama kikuu cha upinzani wanaotoa tuzo kwa Mwenyekiti wa chama tawala mpinzania wao mkuu na wanayetamani kumtoa madarakani.
20241207_190633.jpg
 
Chukulia kama hiyo namba 2. Abdul anao wadhifa gani ndani ya serikali hadi awe yeye ndiye mpigania haki za Tundu Lissu? Kuna sababu zozote za kumfuata nyumbani kwa jambo kama hilo?
Ni kweli hana cheo chochote serikalini, anatumiwa na watu kama chambo cha kupata connection, kitu ambacho siyo rasmi ktk utendaji wa serikali.

Hoja ni kwamba Lisu kasema Abdul alimpelekea rushwa nyumbani kwake ili ahamie ccm, lkn za ndani ya chadema zinasema HAPANA. Sasa which is which? Zikiachwa hizi habari bila kukwnushwa zitamchafua Lisu mwenyewe.

For number 3, ni madai yaliyotolewa na watu toka ndani ya chadema, sasa sisi wasikilizaji inatuchqnganya. Umenisoma mkuu?
 
Hoja ni kwamba Lisu kasema Abdul alimpelekea rushwa nyumbani kwake ili ahamie ccm, lkn za ndani ya chadema zinasema HAPANA. Sasa which is which? Zikiachwa hizi habari bila kukwnushwa zitamchafua Lisu mwenyewe.
Mkuu 'Sex', unajua lakini , kwamba hatufanyi mzaha hapa! Haya ni maswala mazito ya nchi yetu, au siyo? Sasa hao unao wasema wa CHADEMA wanao eleza habari za "HAPANA" wakiwa wenyewe ni wanufaika wa fadhira za Bw. Abdul; unataka Tundu Lissu aeleze mara ngapi ndipo uelewe?
Unataka akajitokeze aeleze tena yale yale aliyo kwisha eleza hata kabla ya kutia nia yake kwenye nafasi inayo gombewa? Kama hujaelewa au hukuamini mara ya kwanza alipo yasema hayo; utamwelewa sasa atakapo itikia mwito wako huu wa kujitokeza mbele kuyasemea tena kwa mara nyingine?

Ndiyo, "nime kusoma" na kuelewa kuwa unalo kusudio la kujichanganya mwenyewe, au kuwachanganya wengine kwa maksudi kabisa. Haieleweki kwa nini unachukua jukumu hilo.
 
Back
Top Bottom