Pre GE2025 Lissu awasili Mlimani City akiwa ndani ya gari yake aliyopigwa nayo risasi Dodoma na watu wasiojulikana, tena ikiwa bado na matundu yake ya risasi

Pre GE2025 Lissu awasili Mlimani City akiwa ndani ya gari yake aliyopigwa nayo risasi Dodoma na watu wasiojulikana, tena ikiwa bado na matundu yake ya risasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anatafuta kura za huruma kama ambavyo alifanya akigombea umakamu mwenyekiti

Anasaka kura za huruma wakati hana huruma na mwenyekiti wake Mbowe anamponda anaponda hadi Chadema na kukivua nguo na kukichafua kionekane rushwa tupu

Hana huruma kuchafua image ya chama halafu yeye anataka huruma za wapiga kura
Hayuko sahihi

Image ya chama ndio kila kitu
Mkuu haya ni mapambano hii ni vita. Siraha yoyote ambayo inaweza kukusaidia katika kushinda vita hiyo kunitumia ni halali. Katika vita nchi hubomoa madaraja yao wenyewe ili kuzuia adui asisonge mbele. A nacho fanya Lisu kisiasa ni sahihi kabisa. Mimi wala si mwana CDM wala CCM.
 
Hayo ni MATUNDU YA RISASI.

Hili ndio gari alilotumia kuenda kurejeshea FOMU ya kugombea Nafasi ya MWENYEKITI.

Hili ndio gari analitumia leo siku ya UCHAGUZI wa nafasi ya MWENYEKITI.

Hili gari ndio litamrudisha NYUMBANI kama mshindi wa NAFASI YA MWENYEKITI.

Gari inaendelea kuwa sehemu ya HISTORIA kwenye maisha ya TAL.

Kila lakheri.🙇🏾‍♂️🤝
Na iwe ushindi.
 
Siundi picha wale waliompiga risasi wanajisikiaje wakimuona na hilo gari leo.
Wakifanya kazi yao na walilipwa. 'Mission accomplished' walijisemea huku wakiwa na glass za champagne.
 
Kwa kweli Lissu yuko moyoni mwa Watanzania wengi. Tunamwombea aibuke kidedea katika uchaguzi wa leo.
 
mtu kapigwa risasi zote izo, afu DJ leo anakuja kutamka bila aibu kwamba, yeye ana pesa, wenzake hawana, na kwamba yeye ndio kawajenga wenzio wote, anaamini amejitoa kwa chama kuliko wengine. kaangalieni gari ya mbowe kama ilishawahi kupata hata pancha tu kwasababu ya harakati, hata kurushiwa jiwe tu. wenzie wamekuwa walemavu kwa sababu ya chama, wamepigwa risasi. yeye ananyonya asali tu, na hotuba zake za kinafikiiiiii.
 
Mgombea wa Uenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amewasili Mlimani City akiwa ndani ya gari alilopigiwa risasi na watu wasiojulikana mjiji Dodoma mwaka 2017 likiwa bado na alama za risasi katika ubavu wa kushoto ambao alikaa wakati akishambuliwa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa juu wa chama hicho.

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?

Lissu amewasili katika viwanja vya ukumbi huo saa 10:15 asubuhi, akiwa ndani ya gari jeusi la Land Cruiser lenye namba za usajili T216 DHH. Kitendo cha Lissu kuingia Mlimani City akiwa ndani ya gari aliyopigwa nayo risasi, tena ikiwa bado na matundu ya risasi, kumeibua hamasa kubwa kutoka kwa wafuasi wake.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotw
Lissu anadeka sana
 
Back
Top Bottom