Lissu awasilisha maombi kwa hati ya dharura Mahakama ya Rufani

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewasilisha maombi mbele ya Mahakama ya Rufaa akiomba kusikilizwa kwa haraka kwa kesi yake ya uhaini.

Kesi hiyo iliahirishwa wiki tatu zilizopita baada ya upande Jamhuri kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani, ukitaka marejeo ya uamuzi wa Mahakama kuu kukubaliana na mapingamizi ya Lissu ya kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.

Mpaka sasa haijajulikana rufaa hiyo itasikilizwa lini ili kesi ya msingi iendelee.

Lissu anaynayekabiliwa na kesi ya uhaini, ameshakaa gerezani kwa zaidi ya miezi 11 tangu alipokamatwa Aprili 9 na kufunguliwa kesi hiyo Aprili 10, 2025.

Katika barua ya Lissu iliyosainiwa Machi 10, Lissu ameomba rufani hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura, huku ikielezwa kuwa hali yake kiafya inazidi kuzorota.

1774107064537.png

1774107076911.png
​
 
Mwenyekiti wa CHADEMA,
Tundu Lissu amewasilisha maombi mbele ya Mahakama ya Rufaa akiomba kusikilizwa kwa haraka kwa kesi yake ya uhaini.

Kesi hiyo iliahirishwa wiki tatu zilizopita baada ya upande Jamhuri kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani, ukitaka marejeo ya uamuzi wa Mahakama kuu kukubaliana na mapingamizi ya Lissu ya kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.

Mpaka sasa haijajulikana rufaa hiyo itasikilizwa lini ili kesi ya msingi iendelee.

Lissu a aynayekabiliwa na kesi ya uhaini, ameshakaa gerezani kwa zaidi ya miezi 11 tangu alipokamatwa Aprili 9 na kufunguliwa kesi hiyo Aprili 10, 2025.

Katika barua ya Lissu iliyosainiwa Machi 10, Lissu ameomba rufani hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura, huku ikielezwa kuwa hali yake kiafya inazidi kuzorota.
mahakama ya Tanzania ni muhimili huru na unaofanya kazi zake kwa uwazi, haki na usawa bila kushurutishwa na matakwa ya mtuhumiwa, licha ya kua na haki kuomba anachotaka.
kupewa sio lazima.

ni muhimu sana kwa kila raia mwema kutii shgeria bila shuruti na kujiepusha na mipango ovu ya kihalifu inayokiuka sheria na katiba ya nchi, ili hatimae kuepuka majuto, mahangaiko na kiwewe cha kisaikolojia kama anachopitia huyu kibaraka anasota korokoroni kwa kosa la uhaini alilopanga kwa makusudi na chama chake akifadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi.
 
Mtoa mada, sasa hayo maombi yapo wapi na sisi tunufaike?
Weka nondo, huyo Bwana ni fundi wa sheria, hayo maandishi yake yanaweza kuwa shule kwa watu humu. Kama kuna mtu anayo iyo legal document atupe tujifunze.
 
mahakama ya Tanzania ni muhimili huru na unaofanya kazi zake kwa uwazi, haki na usawa bila kushurutishwa na matakwa ya mtuhumiwa, licha ya kua na haki kuomba anachotaka.
kupewa sio lazima.

ni muhimu sana kwa kila raia mwema kutii shgeria bila shuruti na kujiepusha na mipango ovu ya kihalifu inayokiuka sheria na katiba ya nchi, ili hatimae kuepuka majuto, mahangaiko na kiwewe cha kisaikolojia kama anachopitia huyu kibaraka anasota korokoroni kwa kosa la uhaini alilopanga kwa makusudi na chama chake akifadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi.
 
Alafu yapo tu yanaona sawa, wao wapo nyumbani na familia zao,wanafuraia mwenzao kua jera kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu
Mazingira kama haya yanayoendelea hapa kwetu baadaye itokee Marekani kafanya uvamizi utasikia watu wakilalamika kuwa Marekani mkorofi ana invade nchi ambazo zina uhuru wa kujiendesha
 
Back
Top Bottom