Lissu azuru Kenya, asema hataki wala hajawahi kutaka kuishi uhamishoni

Lissu azuru Kenya, asema hataki wala hajawahi kutaka kuishi uhamishoni

Atagombea urais wakati rais aliyeko madarakani hawezi siasa za ushindani? Yeye atakuja kuishia mahakamani au jela.
Au futi sita ardhini! Yote yawezekana hapa, na hakuna wa kuhoji. Hali ndivyo ilivyo.

Atapata shida sana huyo. Labda aachane na mambo hayo kabisa.
 
November 28, 2019
Nairobi, Kenya
Mahojiano kamili na Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki Tanzania
Mahojiano na Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki Tanzania.

Paul Nambisu mtangazaji wa KTN News chaneli ya televisheni ya Kenya alifanya mahojiano marefu na Tundu Lissu ambaye hajarejea Tanzania kutokana na kupata matibabu ya muda mrefu mjini Nairobi na baadaye nchini Belgium, kufuatia kushambuliwa na watu waliokatiwa jina 'wasiojulikana' mjini Dodoma Tanzania wakati akihudhuria kikao rasmi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.

Source: KTN News Kenya
 
Ndani ya mwezi mmoja usalama wake umehakikishwa baada ya kudai hawezi kuja Tanzania kwa sababu ya kuhofia usalama wake!

Nimshukuru kwa kutii wito wa mahakama baada ya mdhamini wake kuambiwa na mahakama lazima mtu wake awepo mahakamani au yeye aende segerea!

Wanasiasa wana vituko!

Kimenuka mtego wa panya.
 
Ndani ya mwezi mmoja usalama wake umehakikishwa baada ya kudai hawezi kuja Tanzania kwa sababu ya kuhofia usalama wake!

Nimshukuru kwa kutii wito wa mahakama baada ya mdhamini wake kuambiwa na mahakama lazima mtu wake awepo mahakamani au yeye aende segerea!

Wanasiasa wana vituko!

Acha uongo wa kitoto hivyo. Hakimu gani kamwambia amlete LA sivyo mdhamini aende Segerea?
Na wewe umekuwa mzushi siku hizi?
 
Hiyo ni habari njema sana, ningependa kuona vijana wa Chadema wakijichangisha na kumchukulia form , agombee uenye kiti wa chama chao, huyu ndiye anayefaa kushika hiyo nafasi.

Ama ndiye Katibu mkuu wa mbowe ajaye. Duh na ikiwa hivyo tukiombee mungu chama pinzani kikubwa nchini, mafahali wawili zizi moja, ina shida zake.
 
Kusimamia unayoyaamini na kukubali kulipa bei ya gharama yoyote juu yake ni HESHIMA ya pekee kwa mtu anayehusika.

Kama gharama ni kuwekwa jela au kaburini kwa sababu ya kuyapinga mambo yasiyo ya haki wanayofanyiwa wananchi, ni heshima ipi anayoweza kupewa mtu wa aina hiyo!

Wakati umefika sasa, watu wenye uamini wa namna hiyo wajitokeze kwa wingi, waweke maisha yao chini ya uhai wa mama Tanzania.
Vitisho ndio imekuwa silaha kubwa ya kuwaogopesha watu. Itafika mahali hivi vitisho vitakuwa vinachochea watu
kukubali gharama yoyote watakayotwishwa ili kuihifadhi nchi yetu.

Lissu utakuwa mfano mzuri wa kuigwa na watu wa aina hiyo..
 
Balozi namba 2 wa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Palamagamba Kabudi leo Mh. Tundu Lissu ameingia Nairobi.

Swali safari hiyo Prof. Palamagamba Kabudi kama mjumbe maalum ilikuwa pamoja na mengine kutafuta ushawishi kumzuia Tundu Lissu asiruhusiwe kuingia Kenya ?

Maana mambo yote haya mawili kujitokeza wakati mmoja yanazuwa maswali mengi ikiwemo lile ulilosema Prof. Palamagamba Kabudi nanukuu."..mambo mengine tuliyozungumza ... not for public consumption"

 
Haya ameyaongea leo Bwana Tundu Lissu hii leo kupitia chaneli ya KTN Kenya!
Amewashukuru sana wakenya kwa kujitolea kumchangia damu!

.Aisome John Pombe Magufuli
.............. Palamagamba Kabudi
............... Job Ndugai!

VIVA TUNDU!


Well said!
Welcome back Mheshimiwa
Una uthubutu una mapenzi mema na Taifa
Mungu azidi kukulinda
 
All the best Lissu,pia ni tiketi nzuri kuhakikishiwa usalama kurejea nyumbani. Hakuna mtawala hata mjinga vp ataruhusu media kuandika ".... Tz presidential nominee has been short dead....."
 
Karibu Lissu.Tunamshukuru Mungu kwa muujiza wako.
 
hakuna probing questions

mgeni katambulishwa kama mwanasiasa aliyefukuzwa ubunge

swali lake la kwanza anamuuliza kama ni kweli kafukuzwa ubunge, which means hakufanya research za kujua political status ya mgeni wake

ndio maana hatuwanoi viongozi wetu kwa "maswali ya kushambulia" kama alivyosema Mkapa akirejea usaili uliomrusha akili wa BBC's Hard Talk. Mwandishi wa BBC ana dakika chache na mambo ni mengi ya kuuliza na ku follow up kuchimbua majibu, hawezi kupoteza muda na swali kama "je ni kweli umefukuzwa ubunge" ?

swali la kijinga sana.... Hawa wakenya ndio huwa tunadhani wamesooooma, wameendelea mbeeele , kumbe bana third world wote tunafanana, hata elementary journalism inatushinda
 
Back
Top Bottom