Lissu azuru Kenya, asema hataki wala hajawahi kutaka kuishi uhamishoni

Lissu azuru Kenya, asema hataki wala hajawahi kutaka kuishi uhamishoni

mng'ato,

Huo mstari namba moja ulioniquote sijauandika kwa bahati mbaya bali naelewa nilichokiandika. Nadhani ww unajua, mimi ninajua na wengi pia wanajua kuwa chini ya Magufuli wapinzani hawafanyiwi siasa za kistaarabu wala za haki, usishangae mabomu kupigwa kwenye mikutano ya cdm. Je katika mazingira hayo na hali yake Lissu ya sasa itakuwaje hayo yakitokea? Inawezekana kweli Lisu anajiamini kwenye nafasi hiyo, na mimi namkubali kwa 100%, je mazingira yanamruhusu?

Tuje kwa Zitto, kwanza kumbuka silazimishi Zito kuwa mgombea wa upinzani au cdm kama unavyootaka ionekane, lakini hiyo hainizuii kushindwa kuona uwezo wake kwenye nafasi hiyo kutoka upinzani. Kuna kumkubali mtu hata kwa mahaba niue, lakini kuna mtu ana uwezo, uwe unamkubali au la, lakini hilo ni jambo jingine. Ifahamike cdm sio chama pekee cha upinzani, hivyo tunaposema upinzani tunajaribu kuangalia wagombea wote wa upinzani, sifa na madhaifu yao, kutokea hapo tunapata chaguo sahihi. Hivyo hicho unachokifanya ww hapa uko sawa, na mimi niko sawa kabisa ili kufanikisha kupata mtu sahihi, sio yule mzee tapeli aliyeokotwa 2015 kwa mwendo kasi na upinzani na kupewa nafasi adhimu, kisha alipopanda jukwaani akishia kusema "elimu, elimu, elimu" na mambo mengine yako kwenye mtandao!
 
Kumbe mnashindana hahaha hiyo timing ni coincidence au?, kuna watu maisha magumu sana aisee, naona walipoona P.Kabudi kapewa steji na kujadiliwa huko Kenya hawakulala, sasa unashindana na mtu hata asiyejua wala kujali kama wewe ni mshindani wake? I mean Kabudi sidhani hata kama anajua mnashindana naye, yeye yuko kazini na wala hashindani mtu, kujitesa tu buree!
Kabudi yupi?huyu huyu anaetoa macho na kuongea kwa tashwishi?
 
Lissu kishapona sasa anaogopa kurudi nyumbani
Akirudi tu lazima ashitakiwe kwa uhaini,kwa usaliti wake kwa nchi
 
tindo,

Khs siasa za mabomu&vurugu hizo zinajulikana ndio siasa zetu na mwenye uwezo wa ku-determine kama yuko fit/unfit kushindana kwny huo uchaguzi ni Lissu mwenyewe.

Zitto uwezo wa kuchambua vitu anao especially kwa kujua ku-take advantage ya mazingira ya upepo wa kisiasa ulivyo lkn kwangu mimi he's just another Warid Kaburu tu.

Khs utapeli wa huyo mzee ni kweli alizingua na CDM ilizingua big time lkn cha ajabu Dr.Slaa(aliyetakiwa kugombea kupitia CDM) ndiye aliyemleta Lowassa na kumu-introduce kwa Mbowe,kwanini?Hilo sijui.

BTW hapa ni kama tunafurahisha genge tu sababu ya kiu ya kutaka kuona CCM inapewa changamoto kwny uchaguzi hapo 2020 lkn kwa tume hii ya uchaguzi Magu kutoka hatoki na wabunge wa upinzani watakaorudi bungeni sidhani hata kama 20% watafika.
 
manengelo,
Good nadhani sasa Lissu anakaribia kurudi nyumbani, kama kafika Kenya, naamini in twoor three days atavuka hapo Namanga au Hororo au Sirari (karibu na kwao mkewe) au Misenyi ili aingie nyumbani kwao, TANZANIA. Karibu nyumbani Mwanaharakati wetu.
 
Lissu ndiye mpinzani ambaye sina shaka naye kabisa kwa 100% anatakiwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi
Uzuri wa jf ina reserve nzuri ya kumbukumbu tusikimbiane tu, wapi Dr slaa? Nimeuliza tu.
 
Usishangae wakaungana wakati ukifika
Watu wawili ambao wanaweza kuitia kiwewe CCM ni Tundu na Membe tu tuelekeapo 2020. Hawa wameweza kujipambanua vyema, na hata Mh. Rais wanamkosesha usingizi sawia.
 
Nimebahatika kusikiliza marudio KTN leo tar 29 saa 6 mchana.......kuna sentensi kidogo ananichanganya,siwezi kurudi Tz kwasababu bado natishiwa maisha yangu,jambo ambalo kila mtu angeogopa hata ningekuwa mm,ila ameulizwa utagombea urais "kama chama changu na washirika watanipa nafasi nitagombea" najiuliza hapo atakujaje kugombea wakati anasema bado maisha yake si salama?
 
Lissu atakua taahira akiungana na Membe.

Membe uchungu na wapinzani/watanzania ameuanza lini.

Kwny kipindi cha dakika 45 ITV alipewa nafasi ya kuzungumza miaka hio akawa anasema vijana wa chadema wana shida sana nikikutana nao hua nawanunulia misosi tu basi shida zao zimeisha mara itabidi mbowe kama kiongozi wa upinzani bungeni na yeye aanze kuulizwa maswali kama waziri mkuu anavyoulizwa maswali kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Membe anatengenezwa aonekane anaweza kupambana na serikali then upinzani unampa nafasi ya kugombea urais anashindwa fresh kabisa then anarudi zake CCM kula pensheni yake kama Lowasa vile alivyofanya.

Hamna kitu pale,bure kabisaaa.
Usishangae wakaungana wakati ukifika
 
Good nadhani sasa Lissu anakaribia kurudi nyumbani, kama kafika Kenya, naamini in twoor three days atavuka hapo Namanga au Hororo au Sirari (karibu na kwao mkewe) au Misenyi ili aingie nyumbani kwao, TANZANIA. Karibu nyumbani Mwanaharakati wetu.


Naona umeamua kumpangia kbs na route!halo halo...huyu sio wa kupita hizo route bwana!
 
Back
Top Bottom