Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii video/audio yake iko wapi mtandaoni?
 
Wanachotakiwa kufanya chadema kwanza kuaminika kwa umma na baada ya hapo kuuamsha
 
Wanachotakiwa kufanya chadema kwanza kuaminika kwa umma na baada ya hapo kuuamsha

..sasa ni nani wa kukipeleka chama kwa umma ili kiaminike, na umma uhamasike?

..Mbowe amefanya kazi kubwa, lakini nadhani sasa hivi amechoka.

..Hata hamasa ya kufanya shughuli za chama haonyeshi kuwa nayo.

..Na sisemi hivyo kwa kumlaumu Mbowe. Miaka 30 ya kufanya siasa za kiharakati ni lazima mhusika atachoka kiakili, na kimwili.
 
Busara imuongoze Mbowe ampishe Lissu!.
Ana mikakati thabiti ya kupambana na ma ccm, Mbowe toka apewe ule msamaha na Samia amekuwa hana tofauti na mtu aliyehongwa tuu...kawa mpoleee sn dhidi yake!.
Pia umri umesonga, woga umeingia
 
Uko sahihi. Lakini,Lisuu asimlaumu! Lawama hazisaidii. Mbowe amewekwa mahabusu muda mrefu tuu kwa ajili ya Chama. Mmesahau mara hii. Nashauri Vikao vikae,Mbowe abaki kwenye Ulezi au cheo kingine. Bado Chama kinamhitaji.
 
Uko sahihi. Lakini,Lisuu asimlaumu! Lawama hazisaidii. Mbowe amewekwa mahabusu muda mrefu tuu kwa ajili ya Chama. Mmesahau mara hii. Nashauri Vikao vikae,Mbowe abaki kwenye Ulezi au cheo kingine. Bado Chama kinamhitaji.

..ukisikiliza majibu ya Lissu kutokana na maswali ya waandishi wa habari ametoa kauli za kumheshimu Mbowe.

..lakini unapogombea uongozi ktk hatua ya awali ni lazima kama mgombea ujitofautishe na mtangulizi / aliyeko ktk nafasi.
 
..ukisikiliza majibu ya Lissu kutokana na maswali ya waandishi wa habari ametoa kauli za kumheshimu Mbowe.

..lakini unapogombea uongozi ktk hatua ya awali ni lazima kama mgombea ujitofautishe na mtangulizi / aliyeko ktk nafasi.
Hakika.
 
Makamu mwenyekiti hana nguvu
 
Mbowe ni tapeli wa siasa za Tanzania
 
Mbowe angekua na akili kidogo ilitakiwa apumzike bila kelele
 
Asante sana Mkuu kwa kunijibu kwa heshima inavyotakiwa ingawa unatofautiana na mimi. Nashukuru sana kwa heshima uliyonipa. Na mimi nitakujibu kwa heshima abayo kwa kweli unastahili.
Mimi sikubaliani na wewe kwa sababu zifuazo:
1.Mtu pragmatic ni mtu strategic zaidi ya kuwa tactician. Ana uwezo wa kuangalia picha kubwa na kukubali kushindwa sehemu nyingine ili mradi anajua siku ya siku atafikia malengo yake.
2. Mbowe alikuwa na haki ya kukataa kuingia katika majadiliano na CCM kwa sababu ndio kwanza alikuwa ametoka lupango alipowekwa kwa miezi saba wakati kesi yake ya ugaidi ikisikilizwa. Kesi ambayo hukumu yake ni kifo na viongozi wa juu walituhakikishia kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumkuta na hatia. Ni lazima alikuwa ana hasira na hakuwa na imani kuwa haki itatendeka kutokana na yaliyompata. Angeweza kususa, kukaa nyumbani na kuendeleza mpambano kwenye mitandao na barabarani. Lakini wote tunajua muitiko wetu watanzania bara linapokuja suala la kupambania haki yetu hasa wakati kulikuwa na zuio la mikutano ya aina yeyote. Au angeweza kuingia katika majadiliano ili zuio la mikutano liondolewe, wanachama na wafuasi wa CHADEMA walio ndani watolewe, waanze kupokea ruzuku ili mzigo wa kuendesha chama upunguzwe, viongozi wenzake waliokuwa nje ya nchi wahakikishiwe usalama wao pindi watakaporudi, viongozi ambao walinyimwa stahili zao walipwe. Na yote haya alifanikiwa. Angesusa ili ajipatie sifa za haraka haraka asingefanikiwa kitu. Kumsifia Samia wakati ule ilikuwa ni namna ya kumfanya asibadili mawazo maana ndani ya CCM hoja ya maridhiano ilikuwa inapingwa sana. Na pengine, alikuwa na matumaini kuwa Mheshimiwa Rais akipata ushirikiano atatambua kuwa hakuna haja ya siasa za kibabe.
2. Ulitaka aseme nini zaidi ya kuwafukuza katika chama hao Covid 19? Mnyika amesema wazi kuwa hakuna barua au fomu kutoka kwake iliyowapendekeza. Mimi nahisi wakina Halima waliwekewa presha kubwa ili kufikia uamuzi ule. Nahisi walimuambia Mbowe kuhusu hizo presha nae aka sympathize nao. Aidha, alitegemea kuwa angeweza kuwashauri wenzake wawe na huruma nao. Lakini alipopima joto na kuona kuwa huruma ya aina yeyote haina nafasi hakusita kuunga mkono msimamo wa wengi na kuwatimua. Hiyo ndio pragmatism. Hapo hapo hajaficha kuwa bado ana ukaribu na wakina Halima kibinadamu. Ndio maana aliwaalika wazi wazi kwenye shughuli za kuchangia kanisa lake kijijini kwao. Alifanya hivyo kama Mbowe na sio kama Mwenyekiti Mbowe.
3. CCM isigeweza kukubali kwa namna yeyote kuwatoa wakina Halima bungeni maana legitimacy ya Bunge ingepotea. Ingekuwa ni ku commit suicide baada ya kufanya juhudi za ziada kuwaingiza Bunge. Si Lissu au mtu mwingine angeweza kubadili ukweli huu. Mbowe alitambua hili.
4. Mbowe ni Mwenyekiti wa CDM na msimamo wa CDM kuhusu Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi umewekwa wazi na Mbowe na viongozi wenzake. Viongozi wote wa CDM ( akiwemo Lissu) wana wajibu wa kuyazungumzia masuala haya na wamefanya hivyo. Chadema na taasisi zake zimeandaa mafunzo na makongamano kwa wanachama wao kila mahali. Sijui wangeweza kufanya nini zaidi ili wawaridhishe. Kwa kusema kweli hoja ya kuwa Mbowe amenunuliwa haina mashiko maana tunaona jinsi yeye na wenzake wanavyoendelea kusumbuliwa. Kama hiyo ni kweli basi ina maana Mbowe haumizwi na yaliyowapata wanachama wenzake waliopotea na kuuawa? Kwenye hilo hamumtendei haki.
5. Wakati Msigwa ameanzisha vita ya kumbomoa Mbowe Lissu alikaa kimya. Hata pale watu waliposema kuwa Lissu ndie anayempa kiburi Msigwa alikaa kimya. Wakati wa uchaguzi wa ndani wa CDM, Lissu akatoa shutuma za uwepo wa pesa chafu ndani ya CHADEMA zenye lengo la kuwanyima fursa watu makini wenye moyo wa kupigania haki za wananchi. Wengi tulihisi kuwa alikuwa anamzungumzia Msigwa. Na kweli Msigwa akapigwa stop. Matokeo yake kakimbilia CCM ambako kajipa cheo cha jemadari wa mapambano dhidi ya Mbowe na Chadema. Sijamsikia Lissu akisema lolote kuhusu mambo anayofanya Msigwa. Tofauti kabisa na anavyokuwa mkali kwenye suala la Covid 19 ambao toka wafukuzwe hawajawahi kutoa matamko yeyote kubeza chama chao cha awali. Hii ni moja ya sababu zinazonifanya nimtilie shaka Lissu. Naona kama sifa zimemuingia kichwani na kujiona kama Mussa wa wayahudi.
Naona niishie hapa. Asante tena kwa kuibua hoja kiungwana.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…