Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
ndo mjue effect ya asali. mbowe alilamba asali ya mama na kula sega kabisa sasa mdomo mzito balaa
 
Japo Lisu naye kuna maneno anayaongea yanamfunga. Kama kuna mabadiliko ya katiba na sera za chama kwann hakutumia nafasi yake ya makamu mwenyekiti kuchagiza yafanyike?
Chama ni mali ya Mzee Mbowe ,unadhani kura moja ya Lissu ndani ya vikao inasaidia nini?imagine hela ya chama inaingia kwenye account binafsi hadi leo ?
 
Tatizo team Mbowe wameanza kumtungia Lissu mizengwe, wanatengezeza chats za whatsapp fake kuonyesha Lissu anatumiwa na Msigwa.
Kuna kiongozi mmoja wa kanda alinidekeza hiki kwa masikitiko makubwa.
Walau msigwa anayo akili ya kumzidi Mzee Mbowe ,hapa wanazidi kujiharibia tu.
 
Hakuna kosa mkuu, ndo demokrasia tunayoipigania, ni uamuzi wake, kama walivyo wengine wameamua kuendeshwa na mwamba
Machawa wa mzee Mbowe wanaamini kuwa huyu mzee ni malaika anaeishi🙆‍♂️🙆‍♂️
 
MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)

VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?

Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.

VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?

Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?

Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.

VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?

Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele

VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako

Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.

M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.

Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo

VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?

Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?

Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.

VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?

Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.

Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan

VOA: Mr. Lissu, thank you very much!

TunduALissu: Thank you for having me on your program.
CCM hawataki Lisu awe Mwenyekiti sababu hawezi kuhongwa kirahisi.Aliyepo akioewa 500ml au bilion anauza mechi. Lisu yupo vizuri ila yupo kwenye 'chama maslahi'.Mpango uliyopo ni kuhakikisha mbowe anaendelea kubaki mwenyekiti,hili ndo ccm wanalitaka.Lisu ana watu wengi hata ndani ya ccm(nikiwemo mimi)ambao watamuunga mkono popote atakapoenda ila asije ccm.
 
Hivi ukiwaweka hata kwenye mizani kati ya Mbowe na Lisu nani mwenye CV nzito? nani msomi? bilashaka Lisu ana CV ya kueleweka.
 
Hebu tuwekeeni CV ya Mbowe na CV ya Lisu hapa ili tuone nani zaidi.
 
MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)

VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?

Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.

VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?

Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?

Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.

VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?

Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele

VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako

Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.

M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.

Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo

VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?

Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?

Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.

VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?

Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.

Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan

VOA: Mr. Lissu, thank you very much!

TunduALissu: Thank you for having me on your program.
Kama hii ni Kweli, Erythrocyte wangu tafuta kazi ingine
 
Nani alikuwa anauliza ubinafsi wa Tundu Lissu? Kama hujauona basi husaidiki katika kusoma between lines
 
Kinachonisikitisha kuhusu suala lote hili ni kuwa "it is so unnecessary". CDM walikuwa katika sehemu nzuri ya kuingia katika hiyo hatua anayoizungumzia Lissu. Sasa hivi watu wamebaki wakishughulukiana na kumuacha yule anayewasababishia maumivu yote waliyonayo. Na kwa huzuni kubwa naweza kusema kuwa aliyesababisha yote haya ni Lissu na sio mwingine.

Amandla...
Lissu lazima awe mbaya kwa kuwa amemchalenji kipenzi chenu.

Mbowe anafanya biashara ya siasa.

Ajawai jitokeza kujibu tuhuma za rushwa kutoka kwa Abdul kwenye chaguzi za ndani za chama zilizotolewa na msadizi wake Tundu Lissu.

Mbowe hataki kupisha wengine waongoze chama sasa kugombea kwa Lissu anakuwa mbaya. Lazima alazimishwe kutoka kama hataki kutoka kwa heshima na ukishaingia kwenye uchaguzi utawekwa wazi madudu yako.

Mbowe hajawai sema maridhiano ajenda zilikuwa ni zipi anadanganya wafuasi wake na vitu cheap kama kuruhusiwa mikutano ya hadhara ila issues za maridhiano anafanya siri ila anataka watu wamuamini kwa kuwa yeye ni malaika.

Mbowe kaitaka mwenyewe aibu angesoma alama za nyakati watu wamemchoka.
 
Team Mbowe ipi hiyo? Mbowe mpaka sasa hajatamka lolote lakini bado mnamsingizia. Lissu mwenyewe alituhumu CCM kuwa inaingiza pesa kuvuruga chama. Pamoja na kusema hivyo naamini kuna wajinga kutoka kila upande wanaodhani kumchafua yule wanaemuona kama ni mpinzani wao kutamjenga mtu wao. Tuhuma hizo za kijinga kuhusu Msigwa na Lissu zipo kama zilivyo za kijinga za kudai Mbowe na wachaga wenzake wana mpango wa kumtilia fitna Lissu asigombee. Lissu atagombea tu bila shaka yeyote. Ila haijulikani atapambana na nani. Hizi vurugu zinazoletwa na washabiki zake kwa kweli hazimsaidii.

Amandla...
Kama Chadema inapokea pesa za CCM,yeye atashindia wapi Sasa zaidi ya kubwabwaja?
 
..Tundu Lissu hakupinga Chadema kuingia ktk maridhiano.

..Kilichotokea ni Lissu kupinga danadana na ubabaishaji waliokuwa wakifanya Ccm wakati wa maridhiano.

..Maridhiano yalikuwa yanahusu mambo kama Tume Huru, Katiba Mpya, etc na imethibitika kwamba Ccm walikuwa wanawapotezea muda Chadema kupitia maridhiano, na ACt na wengine kupitia kikosi kazi.

..Kwa maoni yangu chama kinahitaji kujipanga upya, na kurudi kwa wananchi kwa ari kubwa zaidi.
Wananchi wa Nchi gani hao ambao watakuwa mbuzi wa kafara Kwa maslahi ya Chadema? 😆😆
 
Back
Top Bottom