Sawa tuseme kuwa Lissu ndio aliyotaka lakini hayakutokea. Kwa mtazamo wangu ni kuwa hakuwa pragmatic. Unapoingia katika maadiliano hauwezi kung'ang'ania kupata kila kitu unachotaka. Mtu yeyote anajua kuwa hamna namna CCM watakubali Covid 19 waondolewe maana wao ndio wanalipa legitimacy Bunge lao. Bila wao hakuna upinzani, na bila upinzani kamati nyingi za Bunge zisingeweza kuundwa. Hicho ni kilima ambacho CCM wlikuwa wako tayari kufia. Sasa kama katika matakwa yao yote, ni hilo tu ndio halijafanikiwa sioni sababu ya kumtuhumu Mbowe kuwa njia yake ilishindwa.
Mbowe kwa kukubali kuingia katika majadiliano, aliwapa CCM kmba ya kujinyongea. Sasa hivi CCM haiwezi kuituhumu CDM kuwa ni chama cha vurugu na hakiko tayari kukaa mezani kwa majadiliano. Hatua ya Mowe ndio imeupa uhalali hatua anayozungumzia Lissu kufuata.
Sijui ni mimi tu lakini nimemsikia Mbowe akisema kuwa CCM haikuonyesha utayari kuhusu suala la Covid 19, Katiba Mpya na Tume ya Uchaguzi. Kujitoa kwa CDM katika tume na kamati zilizoanzishwa kama sehemu ya mchakato wa vitu hivi ni ishara tosha kuwa wanataka mabadiliko ya dhati na si ya kiini macho.
Mimi nisichoelewa ni way forward ipi amayo CDM inatakiwa kuonyesha. Kama wananchi wanajifungia ndani wakiona askari wanafanya mazoezi au usafi hamna litakalo fanikiwa. Mimi sidhani kama Mbowe anapinga watu kuchukua hatua kali zaidi. Ndio maana Bavicha walipotaka kulianzisha Mbeya na wakakamatwa hakusita kwenda kusimama nao.
Inawezekana Lissu ana point lakini hatua na maneno yanaharibu kuliko kujenga. Kwangu mimi anaonyesha dalili za unafik unafik ambao sio mzuri. Karibu yote anayoyasema ni furaha kwa CCM ambao naamini wanamuogopa zaidi Mbowe kuliko Lissu. Sio bure kumsikia Steve Mengele akimpongeza Lissu. Sio bure kusikia watu wakidai kuwa Msigwa ndie anayembeba Lissu. Sio bure kusikia tetesi kuwa mwisho wa safari yake ni kujiunga na CCM. Aidha, sio bure kusikia tuhuma kuhusu ubadhirifu wa Mbowe zikija kwa kasi. Ni Lissu ndio anayapa oxygen haya yote.
Lissu ana nguvu sana ya ushawishi lakini kwenye hili amekurupuka. Nahisi ameanza kuamini kuwa yeye ni zaidi ya chama na viongozi wenzake. Mawazo kama hayo hayana afya kwa chama chake maana apende asipende kuna wengi wamepitia mengi na Mbowe na wana imani kubwa nae. Matendo na maneno yake yana wa alienate hao watu.
Timu ya Mbowe na Lissu ni formidable na CCM wanajua hilo. Bahati mbaya inaelekea Lissu haoni hilo na anaamini yeye ndie Stelin peke yake.
Amandla...