Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lisu hata akiwa Mwenyekiti kwani atawafanya nini CCM? Mbona Kila siku anazuiwa mikutano huko na hajawahi fanya lolote?

Mwambukusi yuko wapi? 😁😁
Naona jamaa anaweza kuandamana hata peke yake akama alivyokuwaga Kiiza Besigye.

Aftaroo, hawezi kushindana na dola tena za Kiafrika ambazo hazioni aibu katika jumuiya ya kimataifa lakini yeye ni kama vile amejitoa muhanga.

Lakini tujiulize, je, nchi za Kiafrika zinahitaji ukombozi wa mara ya pili baada ya wakoloni au watu kama Lisu ni wachafuzi wa amani?
 
Hajamuuliza kuhusu Msigwa kumuendesha Lissu kama drone?
Lazima utakuwa punguani wewe, si bure!!

Msigwa ana nguvu gani ya kumwendesha Lisu?

Kama Mbowe hawezi kumwendesha Lisu, kama Magufi alishindwa kumwendesha Lisu, hivi hata kwa akili ndogo hiyo uliyo nayo unaamini kuna wa kumwendesha Lisu?
 
Lisu hata akiwa Mwenyekiti kwani atawafanya nini CCM? Mbona Kila siku anazuiwa mikutano huko na hajawahi fanya lolote?

Mwambukusi yuko wapi? 😁😁
Naona jamaa anaweza kuandamana hata peke yake kama alivyokuwaga Kiiza Besigye.

Aftaroo, hawezi kushindana na dola tena za Kiafrika ambazo hazioni aibu katika jumuiya ya kimataifa lakini yeye ni kama vile amejitoa muhanga ni ngumu sana kuzishinda dola za Kiafrika ambazo zinataka kuendelea kutawala, mtaishia kupigana tu kama huko Sudan. Nilitamani Tanzania tuwe kama Botswana na Ghana!

Lisu anachotafuta ni kuandika historia ya kupigania mabadiliko ya kidemokrasia hivyo atawachachafya haswa CCM hata kwa kuandamana peke yake ingawa ni ngumu kuwashinda CCM mana wana mizizi mirefu.

Lakini tujiulize, je, nchi za Kiafrika zinahitaji ukombozi wa mara ya pili baada ya wakoloni au watu kama Lisu ni wachafuzi wa amani?
 
. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo
Makamu Mwenyekiti wa Chama na Bado unasema uongozi umekwama. Si wewe ni kiongozi mzito ndani ya Chama Tena unayetakiwa kumsaidia Mwenyekiti!!! Ebu tueleze ulichukua hatua gani kumsaidia Mwenyekiti na Mwenyekiti akakataa msaada wako? Au ulikuwa umenyamaza badala ya kumsaidia, ili aharibu nawe upate upenyo wa kumuangamiza kiuongozi?

Ebu fafanua!
 
Kwamba Lissu anashikiwa akili na msigwa?
Unajua Mbowe anapewa support na dola ya kupambana na Lissu? Tulia uione show ya lissu
Uzuri wa haya yote, sasa kila kitu kina jipambanua wazi; hata wenye uwezo mdogo wa kutafsiri mambo watayaona kwa uwazi zaidi.

Mbowe, na wale wote walio pokea hela za Bw. Abdul, ni wazi sasa watakuwa katika hali ngumu ya kupambana na Lissu.

Msigwa jambo pekee linalo muunganisha na Lissu ni urafiki kati yao, nje ya siasa.
Sasa Msigwa huyo huyo kanunuliwa kimoja, kama walivyo nunuliwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA.
Lakini sasa watu wanataka Msigwa asiwe kundi moja na hao walio nunuliwa na Abdul; lakini wana himiza awe upande wa aliye kataa kununuliwa. Hii inaingia akilini?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama na Bado unasema uongozi umekwama. Si wewe ni kiongozi mzito ndani ya Chama Tena unayetakiwa kumsaidia Mwenyekiti!!! Ebu tueleze ulichukua hatua gani kumsaidia Mwenyekiti na Mwenyekiti akakataa msaada wako? Au ulikuwa umenyamaza badala ya kumsaidia, ili aharibu nawe upate upenyo wa kumuangamiza kiuongozi?

Ebu fafanua!
Ni kama hujui kinacho/ambacho kimekuwa kikiendelea ndani ya chama kwa muda kitambo sasa. Ni kama leo ndipo umezinduka na kukutana na hali halisi ambayo imekuwepo kwa muda kitambo ndani ya chama.

Wewe hujawahi kusikia malalamiko yoyote kuhusu mwelekeo wa chama, ambao Mwenyekiti amekuwa sehemu muhimu juu yake?
Kumsaidia Mwenyekiti unataka kuweje; kumlazimisha aachane na ndoto zake alizo jenga kuhusu "Mazungumzo ya Maridhiano"? Akikataa, unataka Makamu Mwenye kiti afanye nini?

Mbowe kapewa muda mwingi sana wa kuamua anasimamia wapi na wapi chama kinakopashwa kuwa. Hata uchafuzi wa uchaguzi wa serikali za mitaa inaonyesha haujamstua chochote; halafu utaona bado kuna watu wanahoji mwelekeo wa chama unako kwenda?

Mbowe kalaghaiwa na Samia vibaya sana. Anasubiri kushirikishwa katika serikali ya kipuuzi 2025; mithili ya yale yale tunayo yaona kwa jirani hapo Kaskazini

Sasa kama hayo ndiyo matumaini yenu makubwa, itabidi kuya pambania waziwazi ili watu wawatambue kungali mapema.
 
Japo Lisu naye kuna maneno anayaongea yanamfunga. Kama kuna mabadiliko ya katiba na sera za chama kwann hakutumia nafasi yake ya makamu mwenyekiti kuchagiza yafanyike?
 
Japo Lisu naye kuna maneno anayaongea yanamfunga. Kama kuna mabadiliko ya katiba na sera za chama kwann hakutumia nafasi yake ya makamu mwenyekiti kuchagiza yafanyike?
Amekwambia kuna kutofautiana kati ya yeye na mwenyekiti which means hiki ndio kikwazo,
 
Kumsaidia Mwenyekiti unataka kuweje; kumlazimisha aachane na ndoto zake alizo jenga kuhusu "Mazungumzo ya Maridhiano"? Akikataa, unataka Makamu Mwenye kiti afanye nini?
Kwani ushauri kwa mwenyekiti unafanyika kama ule wa mke kwa mume? Haufanyiki kupitia vikao? Na kama unafanyika kupitia vikao, ndiyo kusema mwenyekiti ana kura ya veto kupinga ushauri wa wajumbe wa vikao akiwemo na makamu mwenyekiti?
 
Watanzania tunapenda sana majibu mepesi ya watu wanaotuambia kuwa wao ni masia wetu. Kusema kuwa Mbowe hataki mapambano na utawala ni uongo mkubwa. Mifano michache ya kuthibitisha uongo huo ni hii:
1. Aliongoza maandamano ambamo Alikwina Akwiline alipoteza uhai wake. Mbowe na wenzake ( akiwemo Halima, Heche, Msigwa na wengine) walifunguliwa mashtaka kutokana na tukio hilo na kukaa rumande na hatimae kuhukumiwa kifungo. Ni michango ya wananchi ndio iliyowatoa jela, Mbowe akiwa wa mwisho kutoka.
2. Tarehe 28 Februari 2020 Mbowe alikamatwa akiwa Hai. Aliachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa masaa mawili.
3. Mwaka 2020 baada ya uchaguzi Mbowe na wenzake walitangaza maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi na jinsi ulivyoendeshwa. Mbowe na wenzake wakina Lema walikamatwa na kufichwa. Zitto na wananchi hawakujitokeza. Kama nakumbuka vizuri vizuri aliokolewa na balozi mmoja ambae alimsindikiza airport ili aende Ulaya.
4. Mwaka 2021 Mbowe alikamatwa Mwanza alipokuwa akijiandaa kwenda kwenye kongamano ya kushinikiza Katiba Mpya.
5. Mwaka 2021 Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi ambayo hukumu yake ni adhabu ya kifo. Alikaa rumande kwa miezi saba kabla ya DPP kuiondoa kesi hiyo Mahakamani. DPP bado ana haki ya kuifufua kesi hiyo.
6. Mwezi Septemba Mbowe na binti yake Nicole wakamatwa Magomeni wakati wameenda kuongoza maandamano ambayo wananchi pamoja na viongozi wengi wa CDM hawakujitokeza. Kwenye maandamano hayo angalau Bawacha walijitahidi. Pamoja na kuwa kusudi la maandamano ilikuwa ni kupinga utekaji na mauaji ya raia, wengi wa walioathirika hawakujitokeza.
7. Mwezi Novemba 2024 Mbowe alikamatwa Songwe wakati anaenda kuwasaidia Lissu na wenzake waliokamatwa mjini Mbeya.

Lissu ana haki ya kupingana na utawala uliokuwepo lakini hana haki ya facts zake. Hiyo mob mobilisation ambayo anaisema imejaribiwa na wakina Mbowe lakini mara zote watanzania wamekuwa wakiingia mitini. Alipaswa kusema kuwa yeye ata mobilise watu kitofauti lakini sio ku insinuate kuwa wenzake ni cowards na mwenye kifua ni peke yake. Kwa mtu wa calibre yake ni lazima achague maneno yake kwa makini ili asitoboe mtumbwi ambao wote wameupanda. Unless yeye ana life vest wakati wenzake hawana. Mbowe anaheshimiwa na wengi na hatapata faida yeyote kwa kujaribu kumvunjia hiyo heshima. Angojee mpaka wagombea wa kiti hicho watakapotangazwa halafu afanye kampeni kwa kuonyesha tofauti yake na watakaoshindana nae na kuweka wazi namna atakavyoboresha chama chake ili kiwe katika nafasi nzuri ya kutwaa dola. Kwa hali hii, inaelekea kwake yeye matokeo pekee atakayoona ya haki ni yale yatakayomtangaza kuwa mshindi. Hiyo sio demokrasia.

Amandla...
 
Amekwambia kuna kutofautiana kati ya yeye na mwenyekiti which means hiki ndio kikwazo,
Mmh ! Ila mambo ya chadema yanachanganya sana. Hivi ni kweli kwamba kila anayegombea uenyekiti huwa anakuwa amenunuliwa na ccm? Napata mashaka sana na hii kasumba?

Why iwe nongwa kwa Lisu baada ya kutangaza kugombea uenyekiti??
 
Binafsi naona kuna watu siku hizi hawalali kutoka CHADEMA kwa kushirikiana na upande wa pili ili kuangalia namna ya kumzuia Lisu asigombee mana wanaona ataleta fujo nchini.

Unajua mzew Mbowe sijui ikikuwa ni busara kama alivyokuwa akipenda kusema au alikuwa anatumika, mana alikuwa hataki kabisa siasa za fujo kwa miaka hii!

Sasa sidhani kama mfumo utaruhusu Lisu awe mwenyekiti. Na asipokuwa mwenyekiti lazima CHADEMA ife mana wanachama pia wamemchoka Mbowe.

Suluhisho. Mbowe akae pembeni na wajitokeze wagombea wengine wapya hata kama asipopewa Lisu basi apewe mwingine tofauti na Mbowe!

..Lissu yuko kwenye siasa tangu mwaka 1995 alipogombea ubunge kwa mara ya kwanza na kushindwa.

..Na miaka yote 29 ambayo Lissu amekuwa akifanya siasa na harakati hajawahi kufanya fujo wala kumuumiza mtu.

..sanasana yeye Lissu ndio amekuwa akifanyiwa fujo, akifunguliwa makesi ya uongo, na hata kujaribu kumuua.

..wenye dola na mamlaka wanamchukia Lissu sio kwasababu analeta vurugu, bali kwasababu ana kipaji kuwazidi, sio muoga, si mlarushwa, na hajakata tamaa.
 
Ni kama hujui kinacho/ambacho kimekuwa kikiendelea ndani ya chama kwa muda kitambo sasa. Ni kama leo ndipo umezinduka na kukutana na hali halisi ambayo imekuwepo kwa muda kitambo ndani ya chama.

Wewe hujawahi kusikia malalamiko yoyote kuhusu mwelekeo wa chama, ambao Mwenyekiti amekuwa sehemu muhimu juu yake?
Kumsaidia Mwenyekiti unataka kuweje; kumlazimisha aachane na ndoto zake alizo jenga kuhusu "Mazungumzo ya Maridhiano"? Akikataa, unataka Makamu Mwenye kiti afanye nini?

Mbowe kapewa muda mwingi sana wa kuamua anasimamia wapi na wapi chama kinakopashwa kuwa. Hata uchafuzi wa uchaguzi wa serikali za mitaa inaonyesha haujamstua chochote; halafu utaona bado kuna watu wanahoji mwelekeo wa chama unako kwenda?

Mbowe kalaghaiwa na Samia vibaya sana. Anasubiri kushirikishwa katika serikali ya kipuuzi 2025; mithili ya yale yale tunayo yaona kwa jirani hapo Kaskazini

Sasa kama hayo ndiyo matumaini yenu makubwa, itabidi kuya pambania waziwazi ili watu wawatambue kungali mapema.
Mbowe ni pragmatic. Kabla ya mazungumzo ya maridhiano ( ambayo inaelekea Lissu aliyapinga) kulikuwa na zuio la mikutano ya hadhara. Kulikuwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliokuwa ndani ambapo wengine walikuwa mpaka na kesi za mauaji. Mazungumzo hayo ndio yaliyopelekea zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa na wengi waliokuwa ndani kesi zao kufutwa na wengi waliokuwa wameenda uhamishoni kurudi. Hayo sio mafanikio madogo. Sidhani kama yangepatikana njia mbadala aliyoitaka Lissu.
Lakini pamoja na mafanikio hayo Mbowe ametangaza wazi kuwa hana imani kuwa CCM wana nia nzuri na maridhiano. Huo umekuwa ndio msimamo wa chama chake na ndio maana hayo mazungumzo hayajaendelea. Kudai kuwa imani yake ya maridhiano ni kikwazo kwa Lissu ni uongo.

Amandla...
 
Kweli kabisa, lkn ktk hili anaendeshwa na msigwa
Viongozi wote wa CCM kuanzia Mkapa, Kikwete na Magufuli wanajua shughuli ya TAL, sasa unapokuja na hoja nyepesi kama hii inaonyesha utoto wako katika mambo ya siasa za upinzani.
 
..wenye dola na mamlaka wanamchukia Lissu sio kwasababu analeta vurugu, bali kwasababu ana kipaji kuwazidi, sio muoga, si mlarushwa, na hajakata tamaa.
Lissu anaogopewa kwa sababu hafichi kitu. Kama ni ujinga atakwambiwa ni ujinga. Kama ni rushwa atasema ni rushwa.
Wananchi wana yasikia haya na kuona yanavyo fanyika.
Hakuna mwana siasa mfaanya maovu atampenda Lissu kwa uwazi alio nao.

Sehemu aliyo pedewa Magufuli, hata kama ni kwa kutoelewa, ni hiyo hiyo ya kuanika baadhi ya maovu yanayo fanyika humo humo kwenye uongozi na nje ya chama; kwa mfano kwenye maswala ya biashara.
 
Back
Top Bottom