Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe ni pragmatic. Kabla ya mazungumzo ya maridhiano ( ambayo inaelekea Lissu aliyapinga) kulikuwa na zuio la mikutano ya hadhara. Kulikuwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliokuwa ndani ambapo wengine walikuwa mpaka na kesi za mauaji. Mazungumzo hayo ndio yaliyopelekea zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa na wengi waliokuwa ndani kesi zao kufutwa na wengi waliokuwa wameenda uhamishoni kurudi. Hayo sio mafanikio madogo. Sidhani kama yangepatikana njia mbadala aliyoitaka Lissu.
Lakini pamoja na mafanikio hayo Mbowe ametangaza wazi kuwa hana imani kuwa CCM wana nia nzuri na maridhiano. Huo umekuwa ndio msimamo wa chama chake na ndio maana hayo mazungumzo hayajaendelea. Kudai kuwa imani yake ya maridhiano ni kikwazo kwa Lissu ni uongo.

Amandla...
Zuio la mikutano ya kisiasa ulikuwa uhuni wa CCM na kunajisi katiba. Hauna hoja.
 
MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)

VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?

Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.

VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?

Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?

Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.

VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?

Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele

VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako

Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.

M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.

Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo

VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?

Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?

Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.

VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?

Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.

Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan

VOA: Mr. Lissu, thank you very much!

TunduALissu: Thank you for having me on your program.
huyu kiongozi atalizwa vibaya sana na Mbowe, hata amini macho yake..

huo mdomo huo hahahaheeeyooohh 🤣
 
Kwani ushauri kwa mwenyekiti unafanyika kama ule wa mke kwa mume? Haufanyiki kupitia vikao? Na kama unafanyika kupitia vikao, ndiyo kusema mwenyekiti ana kura ya veto kupinga ushauri wa wajumbe wa vikao akiwemo na makamu mwenyekiti?
Umeuliza swali zuri ambalo mimi sina jibu juu yake, kwa sababu sijui hao wajumbe wa hicho kikundi ni watu wa namna gani. Lakini kutokana na kusoma dalili tu za nje, ni wazi Mbowe anayo madaraka makubwa juu ya kikundi hicho; kiasi kwamba hakuna jambo asilo litaka Mwenyekiti lipitishwe. Sioni kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA inayo tofauti kubwa na ile ya CCM; ambayo Mwenyekiti atakacho ndicho kiwacho.

Kwa hiyo hapa ukija na huo mfano wa mke na mume, sioni kuwa kuna tofauti yoyote.
Mifano ipo, tokea huko nyuma nyakati za akina Lowassa na mwenzake Waziri Mkuu wa Mkapa. Kwa hiyo siwezi kusema kutakuwa na mabadiliko makubwa sasa katika ushawishi wa Mbowe ndani ya vikao vya kikundi hicho.
 
Very articulated, Lissu na Mbowe tofauti zao ni za kisiasa/kimtazamo, tofauti na Mi-ccm inavyotaka kuaminisha umma
Tatizo team Mbowe wameanza kumtungia Lissu mizengwe, wanatengezeza chats za whatsapp fake kuonyesha Lissu anatumiwa na Msigwa.
Kuna kiongozi mmoja wa kanda alinidekeza hiki kwa masikitiko makubwa.
 
Sioni kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA inayo tofauti kubwa na ile ya CCM; ambayo Mwenyekiti atakacho ndicho kiwacho.
Na hapa ndipo tatizo linapoanzia. Chadema wameiga mambo mengi sana ya ccm, na hivyo kukifanya chama hiki kisiwe na tofauti kubwa sana na ccm kiutendaji na mwenendo wake.
 
Zuio la mikutano ya kisiasa ulikuwa uhuni wa CCM na kunajisi katiba. Hauna hoja.
Kama ni hivyo mbona hamkujitokeza kuandamana kupinga zuio hilo haramu? Wakati wakina Mbowe wanafungwa na wanafunguliwa kesi kwa sababu ya kupinga hilo zuio na mengine mengi mlikuwa wapi?

Ndio leo mnajifanya mtaitikia wito wa Lissu wa kuingia barabarani kwa wingi? Thubutu.

Amandla...
 
Tatizo team Mbowe wameanza kumtungia Lissu mizengwe, wanatengezeza chats za whatsapp fake kuonyesha Lissu anatumiwa na Msigwa.
Kuna kiongozi mmoja wa kanda alinidekeza hiki kwa masikitiko makubwa.
Team Mbowe ipi hiyo? Mbowe mpaka sasa hajatamka lolote lakini bado mnamsingizia. Lissu mwenyewe alituhumu CCM kuwa inaingiza pesa kuvuruga chama. Pamoja na kusema hivyo naamini kuna wajinga kutoka kila upande wanaodhani kumchafua yule wanaemuona kama ni mpinzani wao kutamjenga mtu wao. Tuhuma hizo za kijinga kuhusu Msigwa na Lissu zipo kama zilivyo za kijinga za kudai Mbowe na wachaga wenzake wana mpango wa kumtilia fitna Lissu asigombee. Lissu atagombea tu bila shaka yeyote. Ila haijulikani atapambana na nani. Hizi vurugu zinazoletwa na washabiki zake kwa kweli hazimsaidii.

Amandla...
 
Na hapa ndipo tatizo linapoanzia. Chadema wameiga mambo mengi sana ya ccm, na hivyo kukifanya chama hiki kisiwe na tofauti kubwa sana na ccm kiutendaji na mwenendo wake.
Hivi kwa nini hamtaki kukubali kuwa ndani ya chama chake Mbowe ana ushawishi kuliko Lissu. Hata hivyo siamini kuwa kila wakati mawazo yake ndio yanayotawala. Kwa mfano, siamini kuwa alitaka wakina Halima watimuliwe. Lakini wenzake walipoamua kuwa watimuliwe alitekeleza uamuzi wao. Hivi mna amini huyu Lissu mnayempigia debe atakubali kweli mawazo yaliyo tofauti nae? Thubutu.

Amandla...
 
MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)

VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?

Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.

VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?

Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?

Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.

VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?

Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele

VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako

Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.

M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.

Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo

VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?

Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?

Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.

VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?

Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.

Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan

VOA: Mr. Lissu, thank you very much!

TunduALissu: Thank you for having me on your program.
Hizi stunt zinatengenezwa tuu ila sizani kama kuna issue yoyote kati ya hawa wawili.
 
Team Mbowe ipi hiyo? Mbowe mpaka sasa hajatamka lolote lakini bado mnamsingizia. Lissu mwenyewe alituhumu CCM kuwa inaingiza pesa kuvuruga chama. Pamoja na kusema hivyo naamini kuna wajinga kutoka kila upande wanaodhani kumchafua yule wanaemuona kama ni mpinzani wao kutamjenga mtu wao. Tuhuma hizo za kijinga kuhusu Msigwa na Lissu zipo kama zilivyo za kijinga za kudai Mbowe na wachaga wenzake wana mpango wa kumtilia fitna Lissu asigombee. Lissu atagombea tu bila shaka yeyote. Ila haijulikani atapambana na nani. Hizi vurugu zinazoletwa na washabiki zake kwa kweli hazimsaidii.

Amandla...
Uache ujinga wa kutetea usichokijua.
Jibu haya yafuatayo;
1. Lissu alituhumu cdm kupokea pesa za msma Abdul ili kuvuruga uchaguzi wa ndani. Kwanini Mbowe alikaa kimya?

2. Je unajua kuwa Lissu alitoa tuhuma hizo akiwa Iringa..wajua kwanini?

naomba majibu hayo nikugukie ukweli wote.
 
Mbowe ni pragmatic. Kabla ya mazungumzo ya maridhiano ( ambayo inaelekea Lissu aliyapinga) kulikuwa na zuio la mikutano ya hadhara. Kulikuwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliokuwa ndani ambapo wengine walikuwa mpaka na kesi za mauaji. Mazungumzo hayo ndio yaliyopelekea zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa na wengi waliokuwa ndani kesi zao kufutwa na wengi waliokuwa wameenda uhamishoni kurudi. Hayo sio mafanikio madogo. Sidhani kama yangepatikana njia mbadala aliyoitaka Lissu.
Lakini pamoja na mafanikio hayo Mbowe ametangaza wazi kuwa hana imani kuwa CCM wana nia nzuri na maridhiano. Huo umekuwa ndio msimamo wa chama chake na ndio maana hayo mazungumzo hayajaendelea. Kudai kuwa imani yake ya maridhiano ni kikwazo kwa Lissu ni uongo.

Amandla...

..Tundu Lissu ametoa maelezo kwamba kilichokuwa masharti ya kufanyika kwa mazungumzo ya maridhiano, ndio kimegeuzwa na Ccm kwa udanganyifu kuwa mafanikio au matokeo ya maridhiano.

..katika maelezo yake Lissu anasema kabla ya mazungumzo Chadema waliweka masharti kwamba Mbowe aachiwe, mamia ya mahabusu wa Chadema waachiwe, Covid 19 waondolewe, mikutano ifunguliwe, na mengine. Baada ya hayo kufanyika ndipo CCM na Chadema walitakiwa kuanza kuzungumza kuhusu namna ya kubadili sheria, na mifumo, ili maovu na ukatili uliotokea hapo awali usijirudie.

..Kwa hiyo Lissu sio mpinga maridhiano, ila ni mpinga uongo na ulaghai wa CCM kuhusu maridhiano.

..Tofauti kati ya Lissu na Mbowe ni kwamba ilimchukua muda mrefu zaidi Mbowe kukata shauri kwamba CCM hawakuwa na nia njema katika maridhiano.

..Jambo lingine kwa maoni yangu naona Mbowe anakosea ni kutojitokeza kwa Watanzania na kueleza kwa bayana nini kilijitokeza mpaka kupelekea maridhiano kuvunjika.

..Kuna ombwe katika kuwahabarisha wananchi nini kimetokea katika maridhiano, what is the way forward.

..Jambo lingine ni kwamba pamoja na mikutano kufunguliwa lakini hazionekani jitihada za kutosha kwa Chadema kwenda kwa wananchi. Sijui kama viongozi wamechoka, kuna jambo lingine linasababisha hali hiyo.
 
Hahaha anafanya nini humo Chadema kama iko nusu kaputi naye ni makamu mwenyekiti? Yani maamuzi ya mwenyekiti na makamu yako tofauti au anasemaje, haridhiki na umakamu mwenyekiti?
 
Uache ujinga wa kutetea usichokijua.
Jibu haya yafuatayo;
1. Lissu alituhumu cdm kupokea pesa za msma Abdul ili kuvuruga uchaguzi wa ndani. Kwanini Mbowe alikaa kimya?

2. Je unajua kuwa Lissu alitoa tuhuma hizo akiwa Iringa..wajua kwanini?

naomba majibu hayo nikugukie ukweli wote.
Sijibishani na watu wanaotaka ubishi.

Amandla...
 
..Tundu Lissu ametoa maelezo kwamba kilichokuwa masharti ya kufanyika kwa mazungumzo ya maridhiano, ndio kimegeuzwa na Ccm kwa udanganyifu kuwa mafanikio au matokeo ya maridhiano.

..katika maelezo yake Lissu anasema kabla ya mazungumzo Chadema waliweka masharti kwamba Mbowe aachiwe, mamia ya mahabusu wa Chadema waachiwe, Covid 19 waondolewe, mikutano ifunguliwe, na mengine. Baada ya hayo kufanyika ndipo CCM na Chadema walitakiwa kuanza kuzungumza kuhusu namna ya kubadili sheria, na mifumo, ili maovu na ukatili uliotokea hapo awali usijirudie.

..Kwa hiyo Lissu sio mpinga maridhiano, ila ni mpinga uongo na ulaghai wa CCM kuhusu maridhiano.

..Tofauti kati ya Lissu na Mbowe ni kwamba ilimchukua muda mrefu zaidi Mbowe kukata shauri kwamba CCM hawakuwa na nia njema katika maridhiano.

..Jambo lingine kwa maoni yangu naona Mbowe anakosea ni kutojitokeza kwa Watanzania na kueleza kwa bayana nini kilijitokeza mpaka kupelekea maridhiano kuvunjika.

..Kuna ombwe katika kuwahabarisha wananchi nini kimetokea katika maridhiano, what is the way forward.

..Jambo lingine ni kwamba pamoja na mikutano kufunguliwa lakini hazionekani jitihada za kutosha kwa Chadema kwenda kwa wananchi. Sijui kama viongozi wamechoka, kuna jambo lingine linasababisha hali hiyo.
Sawa tuseme kuwa Lissu ndio aliyotaka lakini hayakutokea. Kwa mtazamo wangu ni kuwa hakuwa pragmatic. Unapoingia katika maadiliano hauwezi kung'ang'ania kupata kila kitu unachotaka. Mtu yeyote anajua kuwa hamna namna CCM watakubali Covid 19 waondolewe maana wao ndio wanalipa legitimacy Bunge lao. Bila wao hakuna upinzani, na bila upinzani kamati nyingi za Bunge zisingeweza kuundwa. Hicho ni kilima ambacho CCM wlikuwa wako tayari kufia. Sasa kama katika matakwa yao yote, ni hilo tu ndio halijafanikiwa sioni sababu ya kumtuhumu Mbowe kuwa njia yake ilishindwa.

Mbowe kwa kukubali kuingia katika majadiliano, aliwapa CCM kmba ya kujinyongea. Sasa hivi CCM haiwezi kuituhumu CDM kuwa ni chama cha vurugu na hakiko tayari kukaa mezani kwa majadiliano. Hatua ya Mowe ndio imeupa uhalali hatua anayozungumzia Lissu kufuata.

Sijui ni mimi tu lakini nimemsikia Mbowe akisema kuwa CCM haikuonyesha utayari kuhusu suala la Covid 19, Katiba Mpya na Tume ya Uchaguzi. Kujitoa kwa CDM katika tume na kamati zilizoanzishwa kama sehemu ya mchakato wa vitu hivi ni ishara tosha kuwa wanataka mabadiliko ya dhati na si ya kiini macho.

Mimi nisichoelewa ni way forward ipi amayo CDM inatakiwa kuonyesha. Kama wananchi wanajifungia ndani wakiona askari wanafanya mazoezi au usafi hamna litakalo fanikiwa. Mimi sidhani kama Mbowe anapinga watu kuchukua hatua kali zaidi. Ndio maana Bavicha walipotaka kulianzisha Mbeya na wakakamatwa hakusita kwenda kusimama nao.

Inawezekana Lissu ana point lakini hatua na maneno yanaharibu kuliko kujenga. Kwangu mimi anaonyesha dalili za unafik unafik ambao sio mzuri. Karibu yote anayoyasema ni furaha kwa CCM ambao naamini wanamuogopa zaidi Mbowe kuliko Lissu. Sio bure kumsikia Steve Mengele akimpongeza Lissu. Sio bure kusikia watu wakidai kuwa Msigwa ndie anayembeba Lissu. Sio bure kusikia tetesi kuwa mwisho wa safari yake ni kujiunga na CCM. Aidha, sio bure kusikia tuhuma kuhusu ubadhirifu wa Mbowe zikija kwa kasi. Ni Lissu ndio anayapa oxygen haya yote.

Lissu ana nguvu sana ya ushawishi lakini kwenye hili amekurupuka. Nahisi ameanza kuamini kuwa yeye ni zaidi ya chama na viongozi wenzake. Mawazo kama hayo hayana afya kwa chama chake maana apende asipende kuna wengi wamepitia mengi na Mbowe na wana imani kubwa nae. Matendo na maneno yake yana wa alienate hao watu.

Timu ya Mbowe na Lissu ni formidable na CCM wanajua hilo. Bahati mbaya inaelekea Lissu haoni hilo na anaamini yeye ndie Stelin peke yake.

Amandla...
 
Kinachonisikitisha kuhusu suala lote hili ni kuwa "it is so unnecessary". CDM walikuwa katika sehemu nzuri ya kuingia katika hiyo hatua anayoizungumzia Lissu. Sasa hivi watu wamebaki wakishughulukiana na kumuacha yule anayewasababishia maumivu yote waliyonayo. Na kwa huzuni kubwa naweza kusema kuwa aliyesababisha yote haya ni Lissu na sio mwingine.

Amandla...
 
Back
Top Bottom