ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Sijui..mbuzi wa kafara kivipi tena?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui..mbuzi wa kafara kivipi tena?
Mabadiriko ni muhimu sana, vinginevyo tutakuwa kama nyani tu, alivyoishi babu hata kitukuu kinaishi kama babu. Kama dunia inabadilika lazima watu, mifumo, tabia , taratibu na mbinu zibadirike ili kufikia malengo kulingana na mshindani wakoMAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)
VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?
Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.
VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?
Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?
Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.
VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?
Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele
VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako
Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.
M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.
Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo
VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?
Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?
Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.
VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?
Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.
Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan
VOA: Mr. Lissu, thank you very much!
TunduALissu: Thank you for having me on your program.
Kama ndivyo basi wamekuja na ubunifu mzuri maana wame kiki haswaa.Hizi ni siasa tu, Chadema wanachanga karata zao vizuri!! Wanataka Chama chao kiongelewe!!
Wewe jamaa ni mpuuzi huyu Msigwa labda ni basha wako unamsifia sana atakuwa anakupiga mashine.Hajamuuliza kuhusu Msigwa kumuendesha Lissu kama drone?
Nimesikiliza hayo mahojiano ila sikusikia chadema ipo nusu kaputi.MAHOJIANO YA LISSU NA VOICE OF AMERICA (VOA)
VOA: Nini kimetokea na uongozi wa sasa?
Lissu: Umekuwa madarakani kwa miaka 20 na muafaka tunatakiwa kufanya mabadiliko ya lazima ili tuweze kupeleka chama mbele.
VOA: Plani yako nini kama ukiwa M’kti, unapeleka chama vipi?
Lissu: Hapa tulipo, tupo kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mabadiliko ambayo tumezungumza kwenye maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa takribani miaka miwili, hakuna matunda yoyote. Njia ya kutoka hapa ni uongozi Mpya uje na uonyeshe na ukipeleke chama kwenye muelekeo tofauti. Kama maridhiano hayajafanya kazi, tuna nini mbadala?
Tunatakiwa tufanye mass mobilization (Nguvu Ya Umma) ili kukiongoza chama kwenye kuliamsha Taifa na kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, vyama vya siasa, ili tuweze kuleta mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili tuweze kulazimisha mabadiliko.
VOA: Kwa hiyo, Tunaweza kusema kuna tofauti kati yako na M’kiti (Mbowe) Juu ya namna ya kukipeleka chama mbele?
Lissu: You are right on the money (Umepiga sehemu sahihi kabisa). Nadhani tuna tofauti ya kimsingi kabisa namna ya kukipeleka Chama mbele
VOA: Kumekuwa na mengi yanaendelea Kati ya serikali na chama chako, kuna wanachama wenu wamekuwa wanatekwa na hatujaona hatua kubwa kutoka kwenye chama chako
Lissu: Hiyo ndio hoja ya msingi kabisa. Hoja ni kuwa chama kinaonekana kime-paralyze (kipo nusu kaputi) kwa sababu M’kiti wa sasa haonekani kutaka kupambana na Samia.
M’kti Hataki kubomoa daraja na uongozi wa Samia. Viongozi wetu na wanaharakati wametekwa na wengine kuuwawa kwa namna za kikatili. Wanachama wetu, viongozi wetu wa Wilaya nao wametekwa na kupotezwa.
Yote haya yanatokeo ni wazi tumerudi kwenye zama za Giza za Magufuli. Na uongozi wa chama unaonekana kutokujua namna ya kutoka kwenye mkwamo huu. Kwa hiyo, nina gombea kwa sababu tunatakiwa kutoka kwenye huu mkwamo
VOA: Umesema No Reforms, No Election. Unaweza elezea hili?
Lissu: Tumekuwa na uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa kama wiki mbili au tatu zilizo pita. Ilikuwa ni MAJANGA! (total disaster!). Ulikuwa ni uchaguzi mbaya kuliko wa 2020 kwa minajili ya manipulation ya uchaguzi kwa kiwango cha kitaifa. Kama hili litakuwa kawaida kwenye chaguzi zetu, ni wazi kwetu kuwa hawapo (CCM) tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani. Kwa hiyo, kama hawapo tayari kuwa na uchaguzi wa ushindani, kwa nini tushiriki chaguzi zijazo?
Kwa hiyo, tumeamua (CHADEMA) ili turudi kwenye uchaguzi, lazima tulazimishe mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Kwa hiyo, msimamo wetu ni: tupiganie mabadiliko, tukisha pata mabadiliko, tutakuwa tayari kushirki chaguzi. Tunasimama kwenye No reforms, No Election.
VOA: Pia, Unataka mabadiliko ndani ya CHADEMA pamoja na ukomo wa uongozi?
Lissu: Kabisa, Hatuwezi kupambana na udicteta wa Samia kama sisi ndani tupo tulivyo sasa. Kwa hiyo, lazima tusafishe nyumba yetu kwanza.
Lazima tusafishe matendo yetu kabla hatuja pambana na uongozi wa Samia. Kama hatuta jisafisha, itakatisha tamaa watu wetu na tutashindwa kupambana na tatizo kubwa ambalo limekuwa linatuathili la utawala wa Samia Suluhu Hassan
VOA: Mr. Lissu, thank you very much!
TunduALissu: Thank you for having me on your program.
Vizuri, msigwa atapata fursa mzuri kuzudi kumkotrol Lissu akiwa ccmLissu ndiye mwenyekiti wa CHADEMA ajaye, tumechoka kuongozwa na kilaza.
Lissu controlled by MsigwaSiungi mkono mbowe kuendelea na uenyekiti lakini naona pia hatari kubwa ya Lisu kuwa mwenyekiti.

🤪🤪🤪🤪😂😂😂😂😂😂🤪🤪Lissu na machine kubwa ,angekuwa ni mwanachama mwingine nadhani Mzee Mbowe angekuwa ameshachuka hatua za kumfukuza kwenye hii kampuni yake.Hakika mzee Mbowe kayakanyaga,
Sikukuona kwenye maandamano shujaa wa kweli.Haahaa kasababisha yepi mkuu shujaa wa mtandao I?😂
Yote ni sawa. Ninachopinga ni "the way he went about it". Alichokifanya ni badala ya kuonyesha tatizo lilikuwa CCM amemgeuza Mbowe kuwa ni tatizo. Sasa hivi kelele ni Mbowe must go sio CCM must go. Ukimya wake kwenye suala hili kunaashiria anakubalia hizo kelele...Tundu Lissu hakupinga Chadema kuingia ktk maridhiano.
..Kilichotokea ni Lissu kupinga danadana na ubabaishaji waliokuwa wakifanya Ccm wakati wa maridhiano.
..Maridhiano yalikuwa yanahusu mambo kama Tume Huru, Katiba Mpya, etc na imethibitika kwamba Ccm walikuwa wanawapotezea muda Chadema kupitia maridhiano, na ACt na wengine kupitia kikosi kazi.
..Kwa maoni yangu chama kinahitaji kujipanga upya, na kurudi kwa wananchi kwa ari kubwa zaidi.
Drama za Mbowe na Lissu katika kuinusuru dolari na anguko.Mbona naona hili suala kama liko 'staged'!?
Hapana.Mbowe ni pragmatic. Kabla ya mazungumzo ya maridhiano ( ambayo inaelekea Lissu aliyapinga) kulikuwa na zuio la mikutano ya hadhara. Kulikuwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliokuwa ndani ambapo wengine walikuwa mpaka na kesi za mauaji. Mazungumzo hayo ndio yaliyopelekea zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa na wengi waliokuwa ndani kesi zao kufutwa na wengi waliokuwa wameenda uhamishoni kurudi. Hayo sio mafanikio madogo. Sidhani kama yangepatikana njia mbadala aliyoitaka Lissu.
Lakini pamoja na mafanikio hayo Mbowe ametangaza wazi kuwa hana imani kuwa CCM wana nia nzuri na maridhiano. Huo umekuwa ndio msimamo wa chama chake na ndio maana hayo mazungumzo hayajaendelea. Kudai kuwa imani yake ya maridhiano ni kikwazo kwa Lissu ni uongo.
Amandla...
Kuna mazuri ya kuiga, toka huko CCM, lakini naona CHADEMA hawayafanyi hayo. Kwa mfano Namna CCM ilivyo jiimarisha hadi huko mitaani kwenyewe. Muundo huu wange utilia nguvu CHADEMA; hata hiyo Dola inayo tegemewa na CCM kuwabakisha madarakani isinge mudu kudhibiti nguvu za wananchi nchi nzima.Na hapa ndipo tatizo linapoanzia. Chadema wameiga mambo mengi sana ya ccm, na hivyo kukifanya chama hiki kisiwe na tofauti kubwa sana na ccm kiutendaji na mwenendo wake.