Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Kwanza kabisa niweke wazi kwamba tuhuma bila ushahidi ni uzushi .bil 100 ni nyingi sana .

Pili hizi pesa ambazo TL amedai zilikutwa nyumbani kwa hayati magufuli ni nyingi sana ,ni pesa ambazo huwezi ficha kwenye begi ni fedha za kuweka kwenye chumba .

Je hayati Magufuli huko Chato alikuwa anaishi peke yake ?

Je hayati alikuwa mtuhumiwa mpaka watu wakapekue kwake ?

Je TL anadanganya umma​

Unapaswa kuwa na Ubongo was maiti ili umuamini lisu kichaa

USSR
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize, hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.
Kwamba afe muda wote na pesa ziwepo tu zimekaa. Hivi anaijua billioni 100 huyo?
 
Imekuwa tabia ya baadhi ya watawala wa Afrika. Wa Malawi naye ilikuwa hivyo hivyo.

Ni jambo lililosikika sana, kuwa mara tu baada ya kifo, waliokuwa wanafanya kazi ya kupeleka pesa, ndio walioenda kuvunja nyumba na kuzikomba zote. Waluzipeleka wapi, hata hatujui. Na hao walifurahia sana kifo cha Magufuli maana kwao ilikuwa ndio mwanzo wa utajiri mkubwa.

Mungu, ukuu wake ni wa ajabu sana. Historia inaonesha watawala waliojilimbikizia utajiri mkubwa, na mara nyingi siyo kutokana na mapato halali, hawakupata nafasi ya kuutumia.

Tanzania ya Nyerere, ya viongozi waliotosheka, imepotea.

Kama wana wa Mungu, tunachotakiwa kufanya ni kumwombea msamaha kwa Mungu. Mema yake yakawe sababu ya yeye kuupokea msamaha wa Mungu. Kama Yesu aliwasamehe na kuwaombea msamaha wauaji wake (Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo) basi nasi twastahili kuiga mafundisho yake kwa vitendo. Lakini waliozichukua hizo pesa wanastahili kuzirejesha hazina, la sivyo, laana ijuu ya vichwa vyao.
 
Kwani alishafanya biashara hii msikitini,ahaaaaa

Nimeipenda hii sentensi
 
View attachment 2709511

View attachment 2709509

Wewe kila siku huwa nakwambia ni zwazwa moja linalotetea na kusifia ujinga.

Ni mtu wa kuja hapa na kusifia watu wanaoharibu mashirika ya umma na kutumia nguvu bila ya kuelewa unasifia nini.

Hiyo faida ya billion 109 hipo wapi hapo. Angalia other income ni kiasi gani kwenye kutengeneza hiyo faida; halafu soma note 11 uangalie what constitute other income 80% sio liquidity ambayo utaikuta bank.

Sasa kama unaweza ongopewa wazi hivyo, kwanini nishangae wewoe kukubali hadithi za mitandaoni. Ni mtu mmoja wa hovyo kazi yako kusifia na kutukana watu tu kwenye hili jukwaa, huku mods wakikuchekea.

Nyie ndio watu mlioharibu uraisi wa Samia kwa kumuongepea na maujinga yenu.
Ulitakiwa uwe ulishatiwa Kitanzi umekunya kabisa
 
Lissu hajui siasa ni mchafuzi nafiki lengo lake kutaka Chadema isikubalike Geita

Kwa nini anajua mwenyewe

GEITA Magufuli ni household name Kawapelekea maendeleo vitu kibao hata umwite mwizi hawakuelewi. Nilikuwa kule wakasema hata waseme mwizi aliiba atujengee hospitali nzuri,uwanja wa ndege, mbuga, Crdb nk na pia yule kabila yetu.

Kuna watu wakabila kama wasukuma, wachaga, wanyakyusa na wahaya? Lissu kachemka msukuma huwezi mtukana Msukuma mwenzie hadharani akakubali huo ujinga hata kama unayemtukana alikosea kweli huuliza kwa nini aje atutukanie Msukuma mwenzetu nyumbani kwetu yaani Geita au Chato?

Matusi ya hadharani kule hawajazoea hasa ukitukana mtu kabila yao wa eneo hilo ni kama kilimanjaro.Lisu haelewi kabisa kuwa lipi aseme wapi na lipi asiseme

Anaua Chadema kwa wasukuma huyo

kuna Tetesi kuwa anajua 2025 Chadema hawatamteua kuwa mgombea uraisi anataka kuhamia ACT wazalendo. Kwa hiyo kabla kuhama anataka kuua Chadema kanda ya ziwa

Lisu hajui eneo lipi aseme nini .Anachoongea mdomoni .Mdomo wake hauna connections na ubongo.

Geita au Chato waweza ponda Magufuli? Au uende mwanasiasa Hai halafu umponde Mbowe hutoboi kwenye kura
 
Labda alivyoenda yeye ndio amefanya utafiti kazikuta..mbona hakutueleza kwenye ile mikutano waliyokuja na kauli mbiu ya kumchana magu wakakosa watu wakaachana kabla ya kurudi na DP world.
 
Kupekuliwa nyumban kwa Magufuli mi sioni ni hoja, madam hakuwa Tena rais lazima security wafanye clearance mambo ya nchi yasije fika mikono isiyo salama
 
CCM team Samia wajanja sana wanavunja ngome ya CHATO kwa kuitumia CHADEMA then baadae wakishawaaminisha kwamba bwana yule alikuwa fisadi basi itakuwa rahisi sana wao kumalizia tu.
Kosa moja halihalalishi mengine.
 
Labda alivyoenda yeye ndio amefanya utafiti kazikuta..mbona hakutueleza kwenye ile mikutano waliyokuja na kauli mbiu ya kumchana magu wakakosa watu wakaachana kabla ya kurudi na DP world.
Lisu yeye chochote anachosikia juu ya Magufuli anaropoka! Mazwazwa nao wanalala nae mbele kushangilia!
Lakini hutamsikia akiongelea ufisadi wa Kikwete na Riziwani!
Hivi Lisu ashindwe kujua habari za Magufuli aje aseme leo! Hizo ni habari za kusikia na kuropoka!
 
Utaelewa tu. Serikali ina mkono mrefu
Samia alivyotaka kumchafua Magufuli tokea mwanzo wa utawala wake ashindwe kulisema hata kama sio yeye machawa wake akina Nape washinde kumwandika hata tweeter au kumzodoa Bashiru au Pole pole kwa jinsi alivyowasumbua mpaka kumpa ubalozi!
 
View attachment 2709505


Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania The Late, John Magufuli baada ya Kufariki kiasi Cha Dolla za Kimarekani milioni 42 (zaidi ya Sh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais, Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mstuko nilioupata.
Kwani uongo?
 
Back
Top Bottom