Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

..yale mabulungutu tuliyokuwa tunamuona akigawa wakati wa safari zake yalikwenda wapi? Alikuwa akiyahifadhi wapi wakati akiwa hai? Nani aliyachukua baada ya kifo chake?
Alikuwa akigawa dollars? Si shillings tu, tena alikuwa wala hazishiki yeye wasaidizi wake. Hela zao za matumizi kwenye ziara.
 
Fine. It’s a personal choice of mine.

Kama wewe unajali, sawa. Huo ni uamuzi wako.

Uamuzi wangu ni kutokujali.
Lakini hata kutokujali nako hujafanya sawaswa, unafanya kutokujali kunakojali.

Kwa sababu umetumia muda wako na nishati kujadili hili suala.

Wasiojali kweli ni wale wanaoangalia tu na kusema "aah, ona Matanzania haya yanabishana ujinga wao" halafu mtu anasepa bila hata kugonga like post moja 😀 😀 😀
 
Niliwahi kushauri, threads za tuhuma za kuchafua watu humu, kwa hearsay ziendane na uthibitisho usiotia shaka, usikute mtoa tuhuma anatafuta a honorary exit ili akitakiwa kuthibitisha, huyooo... anajitimkia zake kurejea kule kwake na kusingizia ametafutwa ili... Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Why umtuhumu tuhuma nzito hivi zisizo na uthibitisho al marhum asiyeweza kujitetea?

Kanuni ya tuhuma ni "he who alleges, must proves!".

Kwa msiojua Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

P
Al marhum,,,,umenikonga moyo[emoji120][emoji120][emoji120]
 
View attachment 2709505

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania The Late, John Magufuli baada ya Kufariki kiasi Cha Dolla za Kimarekani milioni 42 (zaidi ya Sh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais, Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mstuko nilioupata.
Nilisema hili humu nikatukanwa tena zilikua zimewekwa kwenye majaba na viroba mwendazake bhana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwamba Tundu Antipas Lisu anatuambia baada ya kufa Nyumba ya Shujaa Magufuli ikasachiwa na fedha hizo zikakutwa?

Kwanini alisachiwa kama ndivyo?

Tundu Antipas Lisu ana habari gani kwa Watanzania ambazo hawazijui? Tamaduni za misiba ya kitanzania zinajulikana mambo ya kusachiana hayapo

Niishie hapo

Mlale Unono [emoji3]
Wapi hujaelewa ?
 
Nilisema hili humu nikatukanwa tena zilikua zimewekwa kwenye majaba na viroba mwendazake bhana[emoji23][emoji23][emoji23]
🤣🤣Sasa mbona aliwah tuna tisii wakaenda kumvamia kakobe kanisan navkubeba sadaka zilizokuwa kwenye mahaba?
Afu hakuwa mjanja,alipaswa kujenga money vault ndani kwake ya kuhifadhia hiyo mizigo,alifanya kienyeji Sana,labda na ushamba ulichangia🙏
 
Wewe unaamini kabisa habari hizo zingefichika na kutozungumzwa na watu na Samia mwenyewe alivyotaka kumuonesha kwamba Magufuli hakiwa mtu mzuri!
Kwanza propaganda zilianzaga Bashiru kaiba fedha mara blahblah kibao ushahidi zero!
Unajua JPM alitaka viongozi imara, kulinganisha na huyu mama ni mbingu na ardhi.

Bashiru, Polepile, Kalemani, Lukuvi, Kabudi, Hussein Mwinyi
 
Kama Lissu ni muongo, wamshitaki kwa uongo kesi iende mahakamani aoneshe ushahidi wake.

Watawala wasipomshitaki, wamekubali Lissu anasema kweli na wameogopa atatoa ushahidi zaidi ikiwa kesi itafuka mahakamani.
Kabisa ndugu, anayepingana na hoja ya Lissu na atangulie Mahakamani ili akapatiwe ushahidi huko. Kwa bahati nzuri Mahakama zimewekwa mfukoni na maccm, kwahivi hakuna kitakachofichwa
 
Una umbea Sana hata mtu akipiga mihayo unaleta uzi alfu Bila kufafanua vyema ,,,huu Ni ujinga aisee umesoma wapi elimu yako ya upili
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize, hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.

100B kwa Rais naona alikutwa nazo chache sana.
 
View attachment 2709505

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania The Late, John Magufuli baada ya Kufariki kiasi Cha Dolla za Kimarekani milioni 42 (zaidi ya Sh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais, Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mstuko nilioupata.
Nililisema hili humu nikatukanwa haya muko wapi mloniita Muongo??
 
Kama Lissu ni muongo, wamshitaki kwa uongo kesi iende mahakamani aoneshe ushahidi wake.

Watawala wasipomshitaki, wamekubali Lissu anasema kweli na wameogopa atatoa ushahidi zaidi ikiwa kesi itafuka mahakamani.
Aaah kijana hebu achia watu watumbue pesa bhana. Mbona una nongwa kijana!
 
Umeandika "Tundu Lissu ana historia ya kusema uongo".

Una attack character ya Tundu Lissu badala ya kuchambua kesi aliyoleta, that is the textbook definition of ad hominem attack.
Kusema ukweli kuhusu mtu ndo kum attack character yake?

Tundu Lissu alidanganya kuhusu huyo mlinzi wa Magufuli. Nimeweka ushahidi wa video na picha.

Unasema nimemu attack character badala ya kuchambua kesi aliyoileta.

Seriously?? Tundu Lissu hapa kaleta kesi gani zaidi ya hearsay?

Sikliza/ angalia tena hiyo clip. Lissu mwenyewe anasema kwamba “Naambiwa amekutwa na pesa za kigeni dola za Kimarekani milioni 42 nyumbani kwake baada ya kufa”

Hiyo ni nukuu.

Umezungumzia textbook definition, siyo? Basi hicho alichokidai Tundu Lissu hapo ni hearsay.

Hajatoa ushahidi wowote ile. Kasema kaambiwa kuwa Magufuli alikutwa na hizo hela.

Kama kuna mtu anayechafua character ya mwenzake hapa basi ni Tundu Lissu anayedai Magufuli alikuwa ameiba dola milioni 42, bila ushahidi wowote ule.

Mimi kuutaja uongo wa Lissu ambao uko documented si character assasination.

Tundu Lissu lied then and he might be lying now as well.

Yeye kaambiwa tu halafu anapanda jukwaani anasema Magufuli alikutwa na mahela nyumbani kwake.

Ushahidi wake uko wapi?
 
Lakini hata kutokujali nako hujafanya sawaswa, unafanya kutokujali kunakojali.

Kwa sababu umetumia muda wako na nishati kujadili hili suala.

Wasiojali kweli ni wale wanaoangalia tu na kusema "aah, ona Matanzania haya yanabishana ujinga wao" halafu mtu anasepa bila hata kugonga like post moja 😀 😀 😀
That’s only because I have time to waste today. Otherwise I wouldn’t even bother.
 
Back
Top Bottom