Lissu, Heche na Lema mnataka mtumie "ulipo tupo"? Mnaenda kujimaliza kisiasa

Lissu, Heche na Lema mnataka mtumie "ulipo tupo"? Mnaenda kujimaliza kisiasa

Wakati maalim seif aliposhindwa vita vya kisiasa na Lpumba alitumia msemo huu, "shusha Tanga, pandisha Tanga"
"ulipo tupo"

Hili alifanikiwa na kumwachia jengo tupu Lipumba. Leo Zanzibar yote cuf imekufa na ACT ndio inayoonekana.
Hii kwa sababu Maalim ni gwiji la siasa, amesomea political science UDSM, ni mtu aliekubalika Zanzibar na duniani.

Heche, LEMA, LISSU
Lema siasa yake ni uzoefu sio ya kusoma darasani. Heche kilichomnyanyua kisiaasa ni kelele na ukali bungeni. Lkn nakumbuka uchaguzi mmoja alishindwa na Ester matiko, Mbowe akambeba kumueeka kamati kuu. Lissu mwanasheria aliebobea sio mwanasiasa msomi.

Siasa za Tanzania Bara ni tofauti, watu wanajali zaid maslahi fedha , unaweza ukajikuta na wanachama 10. Mnaweza kuhamia CHAUMA Mkajikuta mnatengenezewa mgogoro ndani ya CHAUMA mkahangaika nao, Mnakataka kuhamia ACT nako mkakwama.

Ushauri wangu: Tulieni msisikilize mihemko ya mitandaoni itakupotezeni kisiasa
Pumba tupu
 
Maalim alikuwa na nguvu kisiasa kwa sababu nyingi, moja ya kihistoria, ubaguzi kwa wapemba, utetezi wa uzanzibari. Lissu hakuna anachosimamia, na hana community iliyoapata kufa naye kama ilivyokuwa kwa maalim
Utahangaika sana, huyo sultani kafika mwisho wake.
Huwezi kupambana na muda ukashinda
 
Back
Top Bottom