Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Ndugu acha kuongea utumbo basi, hueleweki kabisa. Hoja yako ni nini hasa? Unashindwaje kufahamu kwamba Serikali hii ya CCM haina tofauti na ile ya NDULI IDD AMIN DADAA?
 
Kumbe na wewe umeligumdua hilo? Huyu jamaa nadhani anayumiwa na wenzetu upande wa act
 
Ndugo MOTN, mengi ulitoyasema yana ukweli , na usiwasikilize wala kuwajibu hao bendera kama akina Salary Slip.

Naomba nikusahihishe au nikuongezee UKWELI mchezo ulivyo mpana kuliko unavyouona.

Lissu alikuwa mmoja wa waliotumia Nguvu zilizoamua Dr Slaa asiwe mgombea mwaka 2015 unfortunately ndiyo hizo hizo zitakazo muangusha naye. Mtego wa Panya....,

Zaidi ya hivyo hata ACT hawantaki, kuna mpango wa pamoja kati ya Mbowe na Zitto kuhakikisha wanamzima Lissu, Zitto anamchukia sana Lissu zaidi ta Mbowe, Mama yake Zitto alipifariki watu waliowashawishi chadema wasihudhurie mazishi ya mama Zitto, ambaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya chadema, walikuwa Dr Slaa na Lissu ndio waliokuwa wakali sana.

Pia wenye Chadema na hata Zitto wanaogopa Lissu akibahatika akawa raisi , basi atakuwa mkali zaidi ya JPM, na hatawasikiliza wala kupokea ushauri.

LISSU, fursa aliyokuwa nayo ni kujiunga na NCCR au vyama vingenevyo, na nina uhakika kwa nguvu zake pekee atakiunua chama chochote atakachojiunga nacho.
 
Huku kufarijiana Mkuu,,, mimi MWANA Chadema Damu na Mifupa,,,,Picha lishaonekana Lissu hatakiwi CHADEMA,,ANATAKIWA NYALANDU AU MBOWE,,,,,,Ila wote hawauziki kama. TUNDU ANTIPAS LISSU,,,Tena NYALANDU ndo mweupee kabisa ,,,,
Huko CCM nani atachukua fomu kupimana misuli na "yesu" wenu?
 
Jiandae tu kisaikolojia Lisu hatateuliwa na chadema Kuna issues nyingi Lisu kachemka

Amechemka kwenye mambo gani labda. Na kwanini cdm hawakumuambia mpaka atangaze nia ya kugombea?
 
Nani kakuambia Mbowe hana nia ya kugombea urais
 
Chadema wagombea watano tu Wa urais maneno yanaanza, hivi vipi mngekuwa kama ccm waliokuwa na wagombea 42? nini maana ya demokrasia? Jambo LA msingi haki itendeke kwenye vikao vya chama.Atakayepata kura nyingi asimamishwe Vila kujali wadhifa wake.Binafsi naamini hili andiko halina nia njema kwa chadema.
 
Lifanyikalo gizani linawekwa hadharani

Lissu akiisikia clip hii inabidi akae afikirie mara mbilimbili

Kama alidhani ana baraka za uongozi wa Chadema kupeperusha bendera ya chsma hicho kwenye uraisi basi ajipange upya. This is not the case!
Kwani akiomba urais lazima apate? Mini maana ya kuwa na baraka za uongozi Wa chama?
 
Pamoja na kununua vyama vya kina Lipumba na mbatia, naona Ccm aka gambas bado mko njia panda, baada ya kuona waliochukua fomu ya urais cdm wako wengi, sasa mnaianza kuweweseka, inafahamika wazi jiwe hataki kuwa na mpinzani kwenye kiti cha urais, sasa kitendo cha kujitokeza wagombea wengi mnaona dhahiri namna ya kuzuia cdm kusimamisha mgombea wa urais itakuwa ngumu, ndio mnakuja na hizi propaganda zenu uchwara.
 
Mimi natamani aje wakati ameshateuliwa kugombea urais na kampeni zinaanza Kama kesho tuone wa kumkamta?hao CCM sometimes mnawapa sifa wasizostahili na ndo maana wanaharibu nchi yetu

Mkuu acha hasira, kwani akija na akakamatwa nini kitatokea? Kumbuka hakamatwi na ccm, bali maagizo ya ccm ndio yanamkamata kupitia vyombo vya dola. Kama kuna mahali tulipobugi ni kwa kufundishwa siasa za kikondoo na kina Lowassa na Sumaye, eti tuache harakati na tufanye siasa za hoja. Matokeoa yake chaguzi zote za marudio tulizoshiriki tumepoteza, na zile tulizosusia wamejitangaza wapendavyo.

Hivi majuzi uchaguzi wa serikali za mitaa ndio wametuona wachumba kabisa, wamejitangaza wanavyotaka na hakuna lolote tumewafanya. Wangalau Lissu ndio namuona anaweza kuamsha ile hamasa ya siasa za kuheshimiana. Viongozi madictator huwa hawaogopi siasa za hoja, huwa wanaogopa siasa za misuguano tu.
 
Huko CCM nani atachukua fomu kupimana misuli na "yesu" wenu?
Kwahiyo makosa yaliyoko ccm yanahalalisha yanayofanyika chadema?

Humo vichwani mwenu uwa mmejaza takataka gani?
 
Huku kufarijiana Mkuu,,, mimi MWANA Chadema Damu na Mifupa,,,,Picha lishaonekana Lissu hatakiwi CHADEMA,,ANATAKIWA NYALANDU AU MBOWE,,,,,,Ila wote hawauziki kama. TUNDU ANTIPAS LISSU,,,Tena NYALANDU ndo mweupee kabisa ,,,,
Subiri vikao vitaamua Mkuu, ukijiita chama cha demokrasia vumilia, shida kubwa ya chadema kila mtu kambale, nidhamu Ni zero. Wagombea watano tu mnalalamika, wangekuwa 42 so mgepasuka.
 
Ngoja tuone hili picha mwisho wake bt nahisi wengine wamechukua form ili watengeze cv wengi tu wanahamu na ubunge wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…