Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.

Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM. Fatma Karume amshtaki Polisi aliyemzonga Mahakamani, adai fidia ya bilioni moja

Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.

My Take
Cross Examination za Tundu Lissu hazijawahi kumuacha askari salama
Maigizo na Uhuni wa Kitaaluma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee. Tofautisha maana ya kusoma hukumu na jopo la mahakama.

Sawa, maana yangu kesi kuendeshwa na jaji zaidi ya mmoja. Hapa suala ni Lissu kuongoza jopo la mawakili. Swali: kesi yenye jaji zaidi ya mmoja, ni mmoja anasoma hukumu, je inamaanisha wengine hawakushiriki kwenye kuandaa hiyo hukumu?
 
Ok. Wote wameshiriki kuandaa hukumu. Tatizo hapa ni idadi ya mawakili wanaomwakilisha mwanasheria mwenzao kama vile hajui sheria, Je, wote watashiriki kuandaa madai na kuyatetea hayo madai?
 
Ok. Wote wameshiriki kuandaa hukumu. Tatizo hapa ni idadi ya mawakili wanaomwakilisha mwanasheria mwenzao kama vile hajui sheria, Je, wote watashiriki kuandaa madai na kuyatetea hayo madai?

Mbona ile idadi ya mawakili (18) walioongozwa na Bi Fatma kumtetea Lissu haikuwa issue? Kwani inakuathiri vipi hiyo idadi katika maisha yako ya kawaida kama mtanzania?
 
Siasa ipo wapi hapo?
kwa utaratibu wa mienendo ya mashtaka katika mahakama ya tanzania, wakili (au mawakili wakiwa wengi) huwa na mda muafaka wa kutoa hoja zao, na zote zinaingia kwenye record. sasa hawa walio zaidi ya 20 hata wakijipanga kila mtu atoe neno moja ni mahakama gani itaweza kuaccomodate hoja zao wote? tena ni kwa nini hawaendi kutetea watu wasio na uwakilishi wa wanasheria na wenye uhitaji, ni mpaka walazimishwe kwa mujibu wa sheria?
Tena kumbuka kuwa hawa wanasheria wanaojirundika kesi zenye umaarufu wanafuata zile zenye umaarufu wa kisiasa zaidi.
Kila siku wanatoa matamko eti wanafanya mshikamano, lakini mshikamano wao uko ki-mlengo flani. si kila mwanasheria anaruhusiwa hata kuchungulia mafaili ya hawa jamaa, au hat kuwakilisha bure. Ni wale marafiki zao tu, ambao wapo mlengo mmoja kisiasa.
 
Mbona ile idadi ya mawakili (18) walioongozwa na Bi Fatma kumtetea Lissu haikuwa issue? Kwani inakuathiri vipi hiyo idadi katika maisha yako ya kawaida kama mtanzania?
rejea post yangu hapo juu
 
hivi ile kesi ya makabichi kule moshi mliyodai million 500+ imeishia wapi? mmelipwa? au ombi la DC kumjumuisha AG lilikubaliwa ?, mkumbukage kuleta mrejesho basi makamanda uchwara
 
Back
Top Bottom