PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Hapana, Lissu anatambua vyema kipi ni siri ila hauwezi ukayatumia ya sirini kutaka kumpiga halafu yeye akae kimya.Hamna kitu kibaya hapa duniani kama kuwa upande wa pili wa Lissu( Na uzuri wa Lissu huwa hana konakona, hata ukimwambia hii ni siri kuna siku utaikuta gazetini)
Mbowe hakupaswa kumshambulia Lissu kuwa anataka vyote na kwamba uamuzi wake wa kugombea ulikuwa ni wa 'ghafla sana' wakati akijua walikutana faragha na kulikuwa na makubaliano.
Kwanini aongee uongo? Kama Lissu angekuwa ni mtoa siri basi hili angeliongea tangu wakati ule anachukua form.
LIssu ameongea na kuhojiwa mara nyingi sana lakini hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kwamba kulikuwa na maongezi yoyote baina yao, ni Mbowe ambaye katekenywa kidogo tu, anatoa kauli zinzopelekea yaliyo sirini kuvuja sababu alitaka kuutumia usiri ule kujiweka salama akijifanya 'Mr. Smart'.
Lissu hakuwahi kumshambulia Mbowe, ila inaonekana Mbowe hawezi kujieleza akaeleweka bila ya kumshambulia Lissu