Tofauti ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu (ingalau kwenye hili) ni ipi...?
Tatizo kubwa ninaliliona la Freeman Mbowe ni kutokuwa mkweli..
Alishindwa nini siku ile ya interview yake kuweka mambo wazi walijadili nini kwenye vikao na wakakubaliana nini.?
Ikawaje akajenga utetezi wake ktk namna ya kumtweza na kumjengea mwenzake picha ya kuonekana ni mtu asiyeheshimu makubaliano..?
Katika hili kwanini uone ajabu Tundu Lissu kuijibu hoja hiyo kwa namna hii aliyoijibu..?
Ni kweli Tundu Lissu ana mdomo mpana usioweza kuhimili kukaa na vitu au mambo ya hovyo...
Kama unafanya naye kazi, usiwe mtu wa konakona, kuwa straight na hapo mtaenda pamoja...
Otherwise, ukiwa na longolongo nyingi, atakulipua tu hata kama wewe ni baba yake...
Kwa maoni yangu, huyu mtu ni mzuri sana. Mkiwa naye kwenye utendaji, mta - achieve malengo yetu haraka bila stress...