Nakala imefika
Ukweli ni kama upembe wa ng'ombe , haufichiki
Viongozi wanajidanganya ! hali ya Muungano ni mbaya sana, chuki imetamalaki na waliobeba Muungano yaani Watanganyika wamechoka. Wakitoa hoja ni uchochezi ni matusi. Wazanzibae waakidai Passport ni sawa tu, wakitukana Muungano kama anavyofanya Jussa na Masoud Othman inaitwa kero.
Tunahitaji Tanganyika, kama hawataki jina hilo basi tunahitaji serikali ya Bara, kama hawataki wachague jina lakini kinachohitajika hakibadiliki , ni serikali ya Tanganyika isimamie masilahi yake na itue baadhi ya mizigo
Kuna wajinga wanasema serikali 3 ni gharama, well, serikali mbili ni gharama zaidi kwasababu Tanganyika inabeba mambo yake, mambo ya Muungano na inabeba SMZ.
Hakuna namna, tunahitaji Serikali ya Tanganyika. Rais SSH akipuuza huu Muungano utafia mikononi mwake! 100%