Lissu na Muungano wa mchongo, aeleza kutekwa kwa Jumbe

Lissu na Muungano wa mchongo, aeleza kutekwa kwa Jumbe

lisu anacho kifanya ni kusambaza chuki zenye nia ovu nchini

mungano ni jambo jema na lakulindwa kwa hali na mali ikibidi nguvu itumike
 
Tundu Lissu akielezea kuhusu muungano wa mchongo.

Aelezea kuhusu wapinga muungano wa kizanzibari kutekwa na kuwekwa vizuizini, Jumbe na wenzake.

Sikilizeni hapa cheche zake.
Sasa ukweli kama huu utauficha wapi na ni nani huko CCM anaweza kuukanusha ukweli huu?

Akitokea huyo, bila shaka atakuwa ni mwendawazimu kwa 100%..!
 
kiuhalisia, siku muungano ukija kuvunjika watakaofurahi zaidi ni watanganyika. wazanzibar wanajifanya watafurahi lakini watapata shida sana kuacha mali zao hapa au kuuza kwa lazima na waondoke tusiwaone kabisa hapa bara bila VIZA.
 
Alisema Nyerere alikuwa ni muongo muongo!! Lakin baadaye anamsifia Nyerere. Wanasiasa wanatafuta Kiki na umaarufu tu. Hakuna kitu.
Nikweli kuwa hakuwahi kuwa muongo?
Pia mtu akisema wewe ni muongo anakuwa amekutusi?
 
Nakala imefika

Ukweli ni kama upembe wa ng'ombe , haufichiki

Viongozi wanajidanganya ! hali ya Muungano ni mbaya sana, chuki imetamalaki na waliobeba Muungano yaani Watanganyika wamechoka. Wakitoa hoja ni uchochezi ni matusi. Wazanzibae waakidai Passport ni sawa tu, wakitukana Muungano kama anavyofanya Jussa na Masoud Othman inaitwa kero.

Tunahitaji Tanganyika, kama hawataki jina hilo basi tunahitaji serikali ya Bara, kama hawataki wachague jina lakini kinachohitajika hakibadiliki , ni serikali ya Tanganyika isimamie masilahi yake na itue baadhi ya mizigo

Kuna wajinga wanasema serikali 3 ni gharama, well, serikali mbili ni gharama zaidi kwasababu Tanganyika inabeba mambo yake, mambo ya Muungano na inabeba SMZ.

Hakuna namna, tunahitaji Serikali ya Tanganyika. Rais SSH akipuuza huu Muungano utafia mikononi mwake! 100%
 
ikiwa ni kwa makubaliano ya kiapo cha kuungana ndio na huwezi kutenganisha
Kuungana ni kwa udongo pekee? Nini maana ya muungano? Kipi kinachokifamya uamini Tanganyika imeungana na Zanzibar? Je kuna rais mmoja? Kuna jeshi moja? Kuna bunge moja? Au ni kipi?
 
Nikweli kuwa hakuwahi kuwa muongo?
Pia mtu akisema wewe ni muongo anakuwa amekutusi?
Yaap!! Ww unaweza kusema kuwa baba yako alikuwa muongo muongo!! Tujaribu kuheshimu watu waliotutangulia, au water wetu. Tukijifanya tunamjua kila kitu, mwisho wetu utakuwa, sio mzuri.
 
Yaap!! Ww unaweza kusema kuwa baba yako alikuwa muongo muongo!! Tujaribu kuheshimu watu waliotutangulia, au water wetu. Tukijifanya tunamjua kila kitu, mwisho wetu utakuwa, sio mzuri.
Siyo tabia nzuri kwa mujibu wa mila zetu lakini ukweli utabaki kuwa ukweli japo unauma,pia siyo sahihi ukweli kuuita tusi japo ni vizuri kuchagua ukweli wa kuusema hadharani
 
Back
Top Bottom