Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Hawa watu wanatengeneza scenes nyingi kulioko series ya isidingo
Kama watanzania wamepuuza, washeni mitandao ya kijamii tuendelee na maisha tuliyoyazoea!

Hizo porojo nyingine sina muda nazo!
 
Huyu anajishitukia tu, na hilo lipo wazi anatafuta huruma za mabeberu waendelee kumfadhili ili siku moja aje kuwalipa fidia hana jipya kwa sasa wala hata hao anao wahisi hawanahabari naye

sent from HUAWEI
 
Inamaana juzi balozi wa Ujerumani alimuacha Lissu home na kwenda kushuhudia Magufuli akiapishwa? Duniani kuna unafiki sana

Amefanya vema kama ni kweli anatishiwa kulinda maisha yake japo hao hao jamii ya kimataifa anaowaomba ushawishi ni ndumila kuwili wanaangalia maslahi ya nchi zao kwanza kwa Tanzania.
 
Nchi imekuwa ya hovyo kabisa hii!!
HAKUNA mwenye akili timamu kumtishia maisha Lissu, Lissu anatishwa na red brigade maana watu wanataka Mbowe aachie ngazi Sasa kahisi Lissu atapendekezwa na Mbowe Kama kawaida yake ukigusa uenyekiti lazima ufe au uhame chama. Anza na Zitto, Wangwe, Sumaye, Mwambe. Sasa ni zamu ya Lissu kumalizwa na Mbowe.
 
Hili halijakaaa vizuri inabidi mamlaka lizitolee ufafanuzi watu waelewe, wakikaa kimya itachafua taswira ya nchi hatujafikia hatua ya kuanza kuzalisha wakimbizi wa kisiasa!

Chochonde tusianze awamu hii ya 6 vibaya kwa kuchafua diplomasia yetu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ametafuta justification ya kuhalalisha kuishi Brussels. Nani ahangaike na Lissu wakati huu ambapo hana madhara. Labda ndani ya CHADEMA huenda anatishia uenyekiti wa mtu ambapo ni sawa na uhaini.
Maneno yako yanaleta hisia za muelekeo wa kaukweli vile. Tutafakari
 
Nasikia Kagame yeye wabaya wake huwa anawafuata huko huko waliko, anatafuta magenge yanayoweza kumfanyia kazi anayalipa yanatekeleza.

Sijui kwanini Lisu anawaambia anataka kurudi Ubeligiji, angekaa kimya wasije, maana wanaweza ku ajiri muuaji akamfuata huko na akamuua.

Ubeligiji siy binguni. Mi siwaamini ccm kabisa na maisha yangu.
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.
kwa Sheria ipi? Kwa sheria ipi?? kwanza mna akili za kutosha kumpatia hatia huyo mtu au unabwabwaja tu?
 
Wapopo husema," Dis matter get k-leg".

Hii ni Sultan Tamba Film, pure old school bongo movie.

Unampigaje mtama mtu ambaye tayari yupo chali yaani kifo cha mende?

Hii janjajanja ya kuwakwepa akina Thomas Simba na Wakyo Simon pale Kisutu na kutafuta uhalali wa kurejea alikotoka for good.

Hizo namba zingekuwa za kwanza kuwekwa mitandaoni na wapambe!

I can't buy this!
 
JPM ni mtu katili sana lakini mnafiki, wa tz naomba mniombee?
Tukuombee uumize wengine kisa wanakukosoa?

Mungu atakulipa sawasawa na matendo yako hapa duniani!
 
Ametafuta justification ya kuhalalisha kuishi Brussels. Nani ahangaike na Lissu wakati huu ambapo hana madhara. Labda ndani ya CHADEMA huenda anatishia uenyekiti wa mtu ambapo ni sawa na uhaini.

Ndugu, kama hana madhara kwa nini wanakata kutoa clearance ili aondoke zake.
 
Lissu na CHADEMA yake ndio wa hovyo kabisa. Hakuna matisho yoyote, ila anajitahidi kuichafua nchi. Hakuna MTU mwenye time na Lissu sasa hivi, ajipange na kusubiri 2025. Hizo mbinu zimefeli kabla ya utekelezaji!!!!
Hawezi kuchafua nchi ambayo tayari imeshachafuka, akishambuliwa au kuuwawa mfuasi au kiongozi wa chadema au ACT watuhumiwa hawajulikani! Akishambuliwa mfuasi wa CCM hata kofi moja wanakamatwa watu 50! Mmechafua nchi kwa uroho wa vyeo na madaraka ya kisiasa. Aibu kubwa sana.
 
Njama, hila na ulaghai wa Lissu umeshajulikana. Yaani kipindi chote cha kampeni hakukuwa na tishio, iweje baada ya Uchaguzi awe anatishiwa?

Asichofahamu ni kudhani alikuwa anapendwa na watanzania kumbe wananchi walikuwa wanaenda kwenye kampeni zake kumfurahisha maana alikuwa anataka Kura za huruma.

Uzuri ni kuwa hata hao Wazungu anawalilia sasa hivi wameshamfahamu kwamba ana matatizo ya kisakolojia.
Liongo sana hilo jamaa
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.
sawa tumekusikia dada, bila shaka wewe ni aina ya mwanamke ambaye huwa unawaombea mabaya wanaume zako wa zamani waliokupiga chini.
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.
Halafu kuna watu huko wanasema hakuna Mwenye time na Lissu aisee, hichi ni kithibitisho kua kuna watu bado wanamfuatilia Lissu na hawapendi kupingwa.
 
Back
Top Bottom