Maelezo yako na conclusion uliyofikia kama haviendani. Awali umeeleza wasiwasi aliokua nao TL kuhusu usalama wa maisha yake hadi akaamua kuomba hifadhi kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani.
Sasa jinsi ulivyomalizia ndio sijaelelewa. Ni kwamba tujihadhari naye kwasababu tu ya yeye kua mwanasheria tricky au ni kitu gani? Jamaa hana jeshi, hana polisi au hata mgambo. Hana chombo chochote cha habari pengine ataeneza propaganda zake za "kuhatarisha amani" na usalama wa nchi, na hata angekua nacho kingefungiwa na Mamlaka za Udhibiti, Hiyo hatari yake mpaka sisi tulioshinda kwa tsunami na wananchi wanatupenda kwelikweli tuanze kumuogopa iko wapi?