Lissu ndilo tegemeo tulilo nalo kwenye kuikomboa nchi hii sasa

Lissu ndilo tegemeo tulilo nalo kwenye kuikomboa nchi hii sasa

Inawezekana wana weledi Lakini maadili yao yanatiliwa shaka.

Ngumu sana kumwamini mtu kama Zitto kwenye harakati za kuitoa CCM madarakani.

Tuache chuki binafsi na tukubali kutokukubaliana. Hakuna aliye mtakatifu. Lazima tuanze na tulio nao mambo yaende kidemokrasia. Tatizo liko wapi?
 
Tuache chuki binafsi na tukubali kutokukubaliana. Hakuna aliye mtakatifu. Lazima tuanze na tulio nao mambo yaende kidemokrasia. Tatizo liko wapi?
Hapa hakuna chuki binafsi wala kumtafuta mtakatifu bali ukweli Lazima usemwe.

Zitto siyo mshirika sahihi kwenye kuitoa CCM madarakani.
 
Hapana Kwa Zitto siyo ramli Bali ni Uhalisia.

Zitto siyo siyo mtu wa kuaminika kwenye ushirika wa kuitoa CCM madarakani.

Zitto ni mbinafsi mno na mtu mwenye hisia za kisasi dhidi ya wanasiasa wenzie nje ya CCM. Ni rahisi kwake kufanya Siasa na CCM kuliko CHADEMA.

Tunawaongelea Kitila hadi Mpina Bado tuna taabu na Zitto?

Tuko serious kweli?

Tunawashashi je nguli wa aina za kina Shivji, Ulimwengu, Kitime nk kwa mawazo mgando hivyo?

Malaika kumbe tukawapate wapi?
 
Hapa hakuna chuki binafsi wala kumtafuta mtakatifu bali ukweli Lazima usemwe.

Zitto siyo mshirika sahihi kwenye kuitoa CCM madarakani.

Ukweli mchungu:

1. TAL hawezi kukubaliana nawe hapa.

2. Umoja ni nguvu na siasa ni sayansi.

3. Lini tutatoka kwenye kuchezeshwa ngoma ya utengano na maccm?
 
Tunawaongelea Kitila hadi Mpina Bado tuna taabu na Zitto?

Tuko serious kweli?

Tunawashashi je nguli wa aina za kina Shivji, Ulimwengu, Kitime nk kwa mawazo mgando hivyo?

Malaika kumbe tukawapate wapi?
Hakuna mahali nimesema kuwa tunahitaji Malaika kutuongoza kuitoa CCM madarakani.

Lakini Zitto hafai labda abadilike!!
 
Imeandikwa katika misahafu kuwa, Mungu hataliacha taifa lake.

View attachment 2845647

"The lord can't forget his people."

Kwa hakika katika zama hizi ni kupitia kwa mja wake TAL:

1. Tofauti na wote, TAL anao usomi, uelewa, uungwaji mkono, wafuasi, charisma, uthubutu, nk unaohitajika kulikomboa taifa hili.

2. TAL ni Nyerere, Mandela, Che Guevara, Castro, Gandhi, nk wa zama zetu.

3. TAL ni wa aina za kina Shivji, Ulimwengu, Kingunge, Chachage, Mtikila, Maalim Seif na wa namna hiyo; akiwaongelea Nyerere kama vijana jeuri wa zama zake alioota mno watanzania tuwe nao siku zote.

4. TAL ni wa aina ya kina Mwabukusi, Slaa, Ismail Jussa, Nshalla, Madeleka na wa namna hiyo wa zama hizi.

5. TAL si mbinafsi, si mnafiki, hamung'unyi maneno, ameelimika na anajua namna ya kuitendea haki elimu na ufahamu wake.

6. TAL ni hazina ya thamani mno, lulu au dhahabu safi kwa taifa hili.

7. Kina Mdude ni wa aina ya kina TAL wanaokosa elimu ya kutosha; elimu haina mwisho hawa ni hazina inayo hitaji nurturing ya akina Lissu, Slaa, Mwabukusi na wa namna hiyo; ukikaa na waridi nawe utanukia; kina Mdude watafika kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha.

8. TAL apewe nafasi aionyooshe CHADEMA; tunahitaji mageuzi ya msingi ndani ya chama hiki pendwa, sasa!

9. Tatizo lililopo Tanzania lipo vyamani kote, lakini sisi nani kuwapa ushauri CCM, CUF, UDP au wa namna hiyo?

10. Ni upuuzi watanzania kukosa heshima au shukurani; kwani wapuuzi hata hawajui heshima wala inatokea wapi:

Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

11. Ni upuuzi watanzania kukosa nidhamu kwani wasiokuwa na nidhamu hawajui hata umuhimu wake:

Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

12. Ni ujinga uliopitiliza watanzania kutojua tofauti za vyama; kwanini vinatofautiana au hata vinasimamia nini:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

13. Combination hii ni ya kutafuta kwa udi na uvumba panapo majaliwa kuwa chini ya mwamvuli mmoja:

"TAL, Zitto, Jussa, Mwabukusi, Mdude, Nshalla, Slaa, Shivji, Ulimwengu, Kitila, Mpina, Madeleka, Kigaila, Maria Sarungi, askofu Mwamakula, askofu Bagonza, Father Kitime, Sheikh Ponda na wa namna hiyo."

14. #13 ni combination ya ushindi.

Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.

Mungu umbariki TAL.
lakani watoa taarifa wengi hawamuelewi wala kumuamini
 
Ukweli mchungu:

1. TAL hawezi kukubaliana nawe hapa.
Hata kama TAL asipokubaliana na mimi lakini huo ndiyo ukweli NINAOUAMINI.
2. Umoja ni nguvu na siasa ni sayansi.
Sayansi ya Siasa inakataa kukubaliana nje ya kanuni mnazoziamini.
3. Lini tutatoka kwenye kuchezeshwa ngoma ya utengano na maccm?
Zitto ndiye aliyejitenga na wenzake na kuamua kuwa na shirika na CCM.
 
Hakuna mahali nimesema kuwa tunahitaji Malaika kutuongoza kuitoa CCM madarakani.

Lakini Zitto hafai labda abadilike!!
bila kuaminiana na kuungana hakuna mahali upinzani inaeza sogelea ikulu ya TZ......

Kwa Ushindi wa asilimia chini ya 20 hadi kuandamana inatia uvivu na kibaraka mjanja atakachofanya ni kukwea pipa, shaaaaa hadi ng'ambo kwa kisingizio maisha yake yako hatarini akati alikuepo tangu mwanzo hadi mwisho wa kampeni 🤣

Mnabaki kujilaumu tu aaa bora ata angegombea fulani au fulani
 
Hakuna mahali nimesema kuwa tunahitaji Malaika kutuongoza kuitoa CCM madarakani.

Lakini Zitto hafai labda abadilike!!

1. Anabadilika vipi wakati umesha mhukumu kifo kuwa hafai?

1664543999224.jpg

2. Itakuwa kukaza ubongo kudhani tulio sahihi ni sisi tu tuwasilikilize na wengine; we may be wrong!

3. Tutachezeshwa ngoma za utengano na ma CCM hadi lini?

4. Lissu hawezi kukubaliana nawe kwenye mawazo yako hayo.
 
1. Anabadilika vipi wakati umesha mhukumu kifo kuwa hafai?
Kwa Sasa hafai ila kwa kuwa binadamu siyo jiwe ivo anaweza kubadilika, basi akibadilika atakubaliwa.
2. Itakuwa kukaza ubongo kudhani tulio sahihi ni sisi tu tuwasilikilize na wengine; we may be wrong!
Kuwasikiliza wengine hakuwezi kulazimisha kukubaliana nao.
4. Lissu hawezi kukubaliana nawe kwenye mawazo yako hayo.
Sijali kama Lissu atakubaliana nami ama la!!
 
Hata kama TAL asipokubaliana na mimi lakini huo ndiyo ukweli NINAOUAMINI.

1. Hii hatua njema tunaliweka hilo pembeni. Ki demokrasia tutakwenda kwenye primaries Hadi elections.

2. Tutashawishiana Kwa hoja Zitto akipita wengi wape.

3. Pana taabu hapo?

Sayansi ya Siasa inakataa kukubaliana nje ya kanuni mnazoziamini.

1. Sawa Hilo kama hapo juu demokrasia itamua.

2. Hapo napo waona je?

Zitto ndiye aliyejitenga na wenzake na kuamua kuwa na shirika na CCM.

1. Haya ni mawazo yako Kila mtu ana yake.

2. Tukumbuke misahafu inasema tusihukumu tusije tukahukumiwa.

NB: Zaidi sana nikukumbushe hili hukujibu:

#3. Tutachezeshwa ngoma za utengano na ma CCM hadi lini?
 
Naunga mkono HOJA.

Lissu angalau anaeleweka, na akiongea anamaanisha.

Tuhakikishe bila Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya, haufanyiki uchaguzi wowote!!
uchaguzi unafanyika vizur sana 2024 serikali za mtaa na 2025 uchaguzi mkuu, kuwepo au kusiwepo kwa hizo vitu ambazo pia bunge litaona ikiwa inafaa au haina maana yeyeote
 
Kwa Sasa hafai ila kwa kuwa binadamu siyo jiwe ivo anaweza kubadilika, basi akibadilika atakubaliwa.

Sina maana hIyo.

Bahati mbaya tunajadili in duplicates.

Nadhani hapa tumekubaliana kuipa demokrasia nafasi.

Kuwasikiliza wengine hakuwezi kulazimisha kukubaliana nao.

Sina maana hIyo.

Nadhani tuipe demokrasia nafasi.
Sijali kama Lissu atakubaliana nami ama la!!

Sina maana hIyo.

Bahati mbaya tunajadili in duplicates.

Nadhani hapa pia tumekubaliana kuipa demokrasia nafasi.
 
LISSU ni chaguo la Mungu..........He is treasure for this country

1. Tumechelewa sana kwa kutompa huyu bwana atunyooshee mambo.

2. Nchi haiwezi kukombolewa kwa siasa za kuvizia, kinafiki, misimamo isiyoeleweka, utengano usiokuwa na tija, kuendekeza ujinga nk.

3. Muda wa kutoka hadharani na kutoleana uvivu ni sasa.

4. Hakuna mwenye chama wala nchi. Vyote ni Mali ya umma.
 
Nimesoma Kwa makini sana hii mada na zile zingine na nimezielewa.

Ndani ya CHADEMA kuna uchaguzi unaendelea...

Nasikia Mbowe kaambiwa achague ama kugombea Uenyekiti au Urais.
 
Back
Top Bottom