Lissu ndilo tegemeo tulilo nalo kwenye kuikomboa nchi hii sasa

Nimesoma Kwa makini sana hii mada na zile zingine na nimezielewa.

Ndani ya CHADEMA kuna uchaguzi unaendelea...

Nasikia Mbowe kaambiwa achague ama kugombea Uenyekiti au Urais.

1. Ni vizuri kuwa umesoma kwa makini, tena sana na hata na zile zingine na kuwa umezielewa bila shaka, vyema.

2. "No hate, no fear" mzizi wetu wa fitna uko hapa:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

3. Bila kujua falsafa na imani za chama zinazozaa misimamo ya wazi kwenye yote, tutafarakana.

4. Nani anagombea nini chamani au nchini, si agenda ya nyuzi hizi; ushindi wetu unahitaji CHADEMA thabiti.

5. CHADEMA thabiti itatokana na wote wenye dhamana na ikiwezekana (wakiwamo) wafuasi, kuwiva vilivyo katika falsafa na imani za chama.

6. Matendo na kauli zao tu zitaakisi hilo; watakuwa wenye ujasiri wa kuhoji, kujitetea, kukitetea na kuipigania chama na hata nchi.
 
Muda muafaka sasa kwa Lissu for Top Job.
 
Ni sehemu ipi ambayo humuelewi mleta mada??
Nimeanza nae tangu jana, akaja na hoja yake kuhusu imani na misimamo, akidai kina Lissu wanatakiwa kuwafunda wanachama, nenda katazame ule uzi wake utaelewa nachozungumzia.

Kuna vitu vingi vya msingi aliviacha pale, lakini kila nikijaribu kumuelewesha jamaa yako ni dikteta much know asiyetaka kuelewa chochote, bahati nzuri akaja Nowonmai kuongezea pale alipopungukiwa.

Ukitoka huko njoo hapa, nenda pale anapolazimisha kudai kauli ya Lissu ni kauli ya chama, comment #31, nikamjibu pale juu kwa kumuelekeza alivyopotoka..

Jamaa yako ukimbana kwenye hoja ukaenda kinyume na kile anachoamini yeye, anachofanya ni kukufukuza chamani na kukuita majina ya ajabu, hajioni alivyo dikteta, nashangaa hata nawe unaponiuliza tatizo lake kama vile huoni makosa yake mengi yaliyojaa humu!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
1. Thibitisha kuwa nimechanganyikiwa.

2. Ninaona wewe umechanganyiwa.

Uthibitisho:

"Umeshindwa kujibu hoja yàngu hata moja pqmoja na kukusihi mno kujikita kwenye mada."
Ukitofautiana na mtu mitazamo wewe ni kumfukuza tu, hufai kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Kwako kila anayetofautiana nawe mtazamo ni CCM, uko mwepesi sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hapa hakuna chuki binafsi wala kumtafuta mtakatifu bali ukweli Lazima usemwe.

Zitto siyo mshirika sahihi kwenye kuitoa CCM madarakani.
Hiki ulichomwambia hapa ukiendelea na huu msimamo wako atakubadilikia, hataki kuambiwa tofauti na kile anachoamini yeye, mwishowe atakufukuza Chadema!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Huyu Chiba masikini kutoka Singida anayenunulika kama pipi aliyeingia makubaliano na Acacia atetee wizi wao na aliposhindwa kazi walimmiminia golori za kutosha huyu jamaa ni mercenaries anatembeza bakuri akiongea ndio analipwa akipewa dola 1000 akaambiwa mtukane Magufuli anamtukana Sana akipewa tena dola 500 mtukane Samia anamtukwna huyu awe mkombozi masikini wa kutupwa
 
Kwetu sie wahenga kumbukumbu ya Mwalimu (RIP) ni pamoja na 'mapenzi yake ya kweli kwa nchi yetu ya Tanzania". Angalia pia kwa jicho hilo, Museveni anaipenda sana nchi yake, .... mapungufu yapo, well no one is perfect.
East African Community (EAC) secretary general Dr Peter Mathuki says, “Thank you so much for your words of wisdom. Every time you speak, you inspire many East Africans and some of us who believe in your philosophy, we listen carefully,” he told Museveni at State House, Entebbe, on Friday

Kwetu huku tunae TAL for sure! Laiti tungekua na mifumo ya kuthamini ipasavyo watu wetu wa namna hii na shukrane isiwe PhD (pull him down) au risasi 32.
TAL pia ni hazina ya taifa letu.
 
Ukitofautiana na mtu mitazamo wewe ni kumfukuza tu, hufai kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Kwako kila anayetofautiana nawe mtazamo ni CCM, uko mwepesi sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

1. Toa mifano kuthibitisha tuhuma zako ambazo aghalabu si kweli.

3. Maneno yangu kwako over and over again ni haya:



4. Kuwa CCM ni Imani. Unaweza kuwa Chadema na hata kuwa kiongozi ila hujui kuwa uko CCM.

5. Misimamo yako inaongea si mdomo wako.

6. Bottom line huwezi kupinga Moja katika haya: LGBTQ, Palestina au Ukraine halafu utuambie ni tofauti ndogo.

7. Tutakuelimisha, ukikomaa haina taabu lakini wewe utakuwa si muumini wa Uhuru, haki, usawa wala demokrasia.

8. Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu kwako kumeza.
 

Huna hoja ndugu na ni aibu sana kwa taifa kuwa na vijana kama wewe:

Your browser is not able to display this video.
 
Hamjifunzi toka kwa Magufuli? Usitegemee binadamu, je akifariki? Tengeneze taasisi yenye watu walikuwa na same caliber badala ya kumtegemea mtu mmoja.
 
Akuokoe we lofa ktk huo upumbavu wako km ataweza
 
Hiki ulichomwambia hapa ukiendelea na huu msimamo wako atakubadilikia, hataki kuambiwa tofauti na kile anachoamini yeye, mwishowe atakufukuza Chadema!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

1. Pole ndugu. Jielekeze zaidi kujua falsafa ya chama. Ujue imani na misingi yake. Misimamo kutokea hapo ni automatic.

2. Siasa si ushabiki. Si mihemko, Si kurukia hoja. Siasa ni sayansi ndiyo maana hakuna rafiki wala adui wa kudumu.

3. Siasa zenye misimamo isiyo wazi, ya kimachale machale, kiwizi wizi, kiujanja ujanja, gizani nk, kwa waliostaarabika no!

4. Hivi ulikumbuka kuandika usipoelewa angalau PM kwa bwana Allen Kilewella huko?
 
Hao wote hakuna mwenye akili timamu
 
Hamjifunzi toka kwa Magufuli? Usitegemee binadamu, je akifariki? Tengeneze taasisi yenye watu walikuwa na same caliber badala ya kumtegemea mtu mmoja.
Tujifunze nini kwa huyo mfu wako, umesahau watu walivyoshehekea kufa kwake? Mungu ni fundi anatupenda watanzania kutuondolea yule mhutu katili na fisadi aliyewapumbaza wajinga km wewe
 
Ukweli unaouzungumzia ni ramli tupu, hujui kitu; mifano gani nikupe badala wewe urudi kusoma comment zako, nyingine zipo uzi huu huu.

Hufai kuwa mwanachama wa siasa unless ubadilike, hujui hata kutofautiana mitazamo unaleta tu habari zako za imani kama vile wanachama wa vyama vya siasa ni robots!, uelewa wako sijui umeuficha wapi, na ni mbishi usiyetaka kuambiwa chochote tofauti.

Nakushangaa unavyoniita CCM eti kwa sababu ya imani, hiyo imani yenyewe nilikuuliza maswali jana ukashindwa kunielewesha badala yake ukawa unanijibu kwa maswali tena!, unashindwa kuelewa vitu vidogo sana, hata sijui wapi nimewahi kukwambia mimi ni CCM, au unapiga ramli?

Ajabu zaidi, unajiita muumini wa haki wakati umeshindwa kukemea ule unyama wa Hamas kwa watanzania wenzetu, unashangilia tu kile alichosema Lissu, hii haki unayoipigania wewe ni ya sampuli gani?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…