Akizungumza na Watanzania kupitia katika mtandao wa clubhouse mheshimiwa Lissu amejibu maswali mengi aliyoulizwa na Watanzania. Miongoni mwa mambo aliyoulizwa ni kuhusu faida za maridhiano zilizoelezwa na mwenyekiti Mbowe. Akijibu swali hilo, Ndugu Lissu akasema, anashangaa ndugu Mbowe kuwatangazia wananchi kuwa haki zao za kikatiba kama vile haki ya kufanya mikutano, kufuta kesi za kubambikiwa eti ni matunda ya maridhiano. Lissu akasema kuwa hayo ni haki zao za kikatiba NI NON-NEGOTIATABLE AT THE FIRST PLACE (yaani si jambo la kukaa vikaoni na kujadili eti hizo haki wapeweje)
Mheshimiwa Lissu akasema kuwa , Yeye alipokutana na Samia kule Brussels alimwambia wazi kuwa kwanza afungulie haki zao za kikatiba kisha baada ya hapo ndo wazungumze maridhiano. Mheshimiwa Lissu akasema kuwa kwake maridhiano siyo kupewa kilicho chao kwa mujibu wa katiba, bali maridhiano ni kukubaliana namna ya kufanya REFORMS ZA MSINGI za KATIBA MPYA na SHERIA FAIR ZA UCHAGUZI. Hiyo ndo definition ya maridhiano kwa mujibu wa Lissu.
Lissu akasema, Mwenyekiti alipokuwa kwenye kikao cha baraza la wazee huko Zanzibar alikiri wazi kuwa Mardhiano yalikuwa ni FAILURE na akasema wenzie walioyapinga toka mwanzo walikuwa sahihi, sasa anashangaa leo Mwenyekiti anayapongeza maridhiano kuwa eti yalikuwa mazuri.
Mheshimiwa Lissu akaeleza kuwa Serikali/CCM walikataa mambo ya msingi yote ambayo CHADEMA walitaka kuwa ndio yawe maridhiano halisi, tena waliyakataa kwa barua siyo kwa maneno matupu. Sasa inakuwaje leo Mwenyekiti anasema eti maridhiano yalikuwa ni mafanikio?
Wakati huohuo Ndugu Lissu akampongeza na kumshukuru mheshimiwa Mbowe kwa huduma yake kwa chama, kwa kujitolea kwa namna nyingi sana kukisaidia chama. Hata hivyo Mheshimiwa Lissu akasema, kila mwanachama wa CHADEMA kwa nafasi yake wamakichangia chama. Wapo waliolipia gharama ya juu kabisa ya kujitolea ikiwemo uhai wao, mfano watu kama Ben Saanane, Mzee Kibao, Alphonce Mawazo n.k
UNAWEZA KUSIKIA SAUTI YA LISSU AKIELEZEA MAMBO HAYO HAPA"
View attachment 3183725