Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Lissu hana sera bali anasubiri Magufuli kesho afungue kampeni, atakachokuwa anaongea Magufuli basi Lissu atakuwa na kazi ya kumjibu. Kimsingi Lissu bado viatu vya Urais havimtoshi
Hivyo wanasubiri CCM waongee na wao ndo wachezee humo humo ?
 
Siasa tamu sana huwezi kosa jibu la hoja yoyote inayoletwa jukwaani.​
Kama huamini fuatilia kuona CDM wanavyopangua hii hoja.​
 
Nimemuelewa. Binafsi nilitaka kusikia pia yeye atafanya nini ili kuweka mazingira mazuri kwa wakulima na wafanyakazi wa Tanzania ?
Hayo y apo lkn haina maana kuongelea sera wakati hata wagombea wenzie wa kuzisimamia wameenguliwa kinyemela tuu.

Ccm hatak kushindana kwa sera alishasema SG Bashiru kuwa.wao wana dola hivyo hawatakubali ccm ifutike kwenye raman kama kanu
 
Umenena vyema. Na huu ni uthibitisho hamna kura za huruma toka kwa watanzania.
 
Siku ya kwanza tu anatoa pasi fyongo?je akichanga so ile mihasira yake ndio itakua inatawala
Kumbe wengi mmeona ?Inje mvua lije jua alitakiwa leo awamalize kabisa CCM.
 
Ilikuwa hivyo pia kule Tunisia, Egypt na kwingineko duniani ambapo madikteta walijisahau na kudhani vyombo vya dola vitawalinda milele huku wakiendeleza udhalimu wao lakini wananchi waliposema sasa basi cha moto walikiona. Hivyo hapa Tanzania pia yaliyotokea katika nchi hizo yanaweza kabisa kutokea na yesu wa lugola akaikimbia Ikulu. Usicheze kabisa na NGUVU YA UMMA wanaposema sasa basi LIWALO NA LIWE.

Hapo kwenye maandamano ndo pagumu. Watanzania hawawezi kuandamana.
 
Hayo y apo lkn haina maana kuongelea sera wakati hata wagombea wenzie wa kuzisimamia wameenguliwa kinyemela tuu.

Ccm hatak kushindana kwa sera alishasema SG Bashiru kuwa.wao wana dola hivyo hawatakubali ccm ifutike kwenye raman kama kanu
Yeye mwenyewe aliweka pingamizi ili Magufuli aeunguliwe.
Hiyo siyo sababu ya wao kutokuongea sera zao. Ila muda wa kupitisha bakuli wamepata.
Lissu leo kafail big time.
Ila bado naangalia mbele ili nimsikilize tena. Hope ataacha kutumia muda mwingi kuelezea alivyopigwa risasi nk.Hiyo historia inakula muda mwingi mno. Anatakiwa awe short and clear katika historia hiyo.Aipe dakika tano tu.
Ukizingatia siku anatua Bongo alituelezea.
 
Siku ya kwanza hii, kaa mkao wa kula sasa
First impression matters...kabugi...tutajua huko mbele ataongea sasa sababu wananchi wamemlazimisha aongee atafanya nini...angeanza na mwanzo walau...
 
Mm nafikiri hujasikia vzr, ni kwamba Leo ilani haijazinduliwa sababu ya kuweka sawa suala la wagombea walioenguliwa
Kiswahili ni kirahisi mno
Suala la wagombea haliwezi kuzidi uzito wa Ilani. Leo ilikua uzinduzi wa Kampeni na ndiyo siku ya kuzindua ilani ili kuwaambia watanzania wanaenda kuwafanyia nini. Hili la wagombea lingeweza tu kushughulikiwa kwa namna yoyote ile ambayo wangeona inafaa, lakini siyo kuzuia ilani.Ukweli ni kwamba, Mwitikio wa watu Leo ulikua mdogo sana tofauti na mategemeo yao. Wameamua kubadili gia angani maana ni aibu sana, wataenda kuizindua sehemu watakayopata watu wengi.
 
Si umeona kule Tunduma? Siombei machafuko yatokee lakini madhara ya kuminya haki na uhuru wa Watanzania katika kuamua Viongozi wawatakao yanaweza kuwa makubwa sana hasa wakati huu ambapo Watanzania wengi hawana furaha kutokana na maamuzi mbali mbali ya kutowajali yanayofanywa na walio madarakani.

Hapo kwenye maandamano ndo pagumu. Je watu wataitikia ?Watanzania tunavyoogopa kipigo cha mbwa koko.
 
Ila watu walikuwepo bwana. Ila naungana na wewe leo ndo walitakiwa wamwage sera zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…