Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

ALISEMA LEO HAZUNGUMZI ILANI KWAKUWA JAMBO KUBWA NI KUENGULIWA WAGOMBEA
Tatizo hili wamechagia sana kulijenga. Uchaguzi wa serikali za mitaa,walivyoenguliwa walitakiwa wawashe moto. Sema wao wakaamua kuzila. Na CCM lengo lao wanataka wapinzani wazile tena.
Kipindi kile serikali za mitaa Chadema et al,walitakiwa wasimame kidete.
 
Urais siyo makalio kwamba kila mtu anasitahili kuupata.
Mwambieni lissu Magufuli anatosha kabisaa kwasbabu ni predential material.
 
Siku kadhaa zilizopita Niliposema Lissu is not a " Presidential material", kwa wengi sikueleweka. Leo nadhani wengi watakuwa wameanza kunielewa!

Yaani badala ya kujenga hoja kwa wananchi wamchague, " Ni yeye" anaifitinisha Tanzania dhidi ya Jumuiya yamkimataifa. Tanzania ya watanzania tena ya wananchi wenye uwezo wa kumuweka madarakani. Yaani anataka Jumuiya ya kimataifa ndiyo imuweke madarakani hapa nchini badala ya sisi watanzania ndiyo tumuweke madarakani. Sasa Lissu akisha wekwa madarakani na jumuiya hiyo ya Ulimwengu, atailipa nini!? Siyo ndiyo, mwanzo wa Lissu kutuuza watanzania kwa mafungu...!!! Kwa hili, leo amepoteza nafasi adhimu ya kuwashawishi watanzania kwa hoja ili wamuweke madarakani.

Jumuiya ya kimataifa hii mnayoita mabeberu ndio unalaumu anatukosanisha nayo?? Nilidhani mnasema hatuhitaji mabeberu.
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Amesema,atasema siku nyingiene na siyo kwenye vurugu mshenzi ya leo.
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Hii ni fikra makini, kama Watanzania wote tutaamua kujiuliza na kujitafakari katika uchaguzi wa kipindi hiki, basi tutaona kwa usahihi kiongozi aneyesitahili kuiongoza Tanzania ya Sasa.
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Kama ulifuatilia mkutano huu na kama ulimfuatilia Mnyika , usingeleta uzi huu
 
Siku kadhaa zilizopita Niliposema Lissu is not a " Presidential material", kwa wengi sikueleweka. Leo nadhani wengi watakuwa wameanza kunielewa!

Yaani badala ya kujenga hoja kwa wananchi wamchague, " Ni yeye" anaifitinisha Tanzania dhidi ya Jumuiya yamkimataifa. Tanzania ya watanzania tena ya wananchi wenye uwezo wa kumuweka madarakani. Yaani anataka Jumuiya ya kimataifa ndiyo imuweke madarakani hapa nchini badala ya sisi watanzania ndiyo tumuweke madarakani. Sasa Lissu akisha wekwa madarakani na jumuiya hiyo ya Ulimwengu, atailipa nini!? Siyo ndiyo, mwanzo wa Lissu kutuuza watanzania kwa mafungu...!!! Kwa hili, leo amepoteza nafasi adhimu ya kuwashawishi watanzania kwa hoja ili wamuweke madarakani.
Presidential material ni mtu wa aina gani?
 
Kasema hotuba amabayo aliiandaa hataisoma.

Wanataka wadeal kwanza na wagombea walioenguliwa.

Sasa kwa nini wasingeahirisha kwanza hadi wa-resolve hizo issue badala ya kuwachosha watu kuja na kuishia kuambulia maneno.
 
Binafsi niliumia sana Lissu kupigwa Risasi. Ila Mungu kamuokoa. Sasa ninamsihi awe kama Yusuphu. Yusuphu pamoja na aliyofanyiwa still alisonga mbele,still aliweka mikakati Misri ikawa nchi yenye chakula tele.
Lissu be Joseph now ,yaliyopita yamepita.

..Yule Askofu alizungumza vizuri sana.

..He was the star of the campaign kwa leo.
 
Mwanzoni Mbowe alivyoongea TBC hawajaonyesha. Ila all in all.Hakuna sababu yeyote ambayo ilitakiwa kuwazuia leo kumwaga sera zao. Wangesema kwa nini tuwachague na still wangesemea walioenguliwa pia.
Kususia kutoa hotuba kuna lengo la kuonyesha u-seriousness wa shida iliyopo mbele. Muda wa kumwaga sera badoooo ndiyo kwanza unaanza. Unajua mwaka 2015 CCM walipata mteremko sana kwa sababu Lowassa alikuwa hawezi kutamba jukwaani. Mpaka Magufuli akaonekana ni mzuri kumbe wapi. Hii kampeni itawasumbua sana CCM kwani kosa alilofanya Magufuli ya kuzuia mikutano ya wapinzani halafu yeye akawa anatamba mwenyewe kulimfanya adhanie kuwa anapendeka na kuheshimika na wananchi wengi sana. Sasa hivi anapokumbana na reality check anajikuta anachanganyikiwa. Hivi kosa kama lile la kuweka picha ya namna ile kwenye fomu badala ya kuweka picha ya halisi ya passport size ukiambia limefanywa na rais anayemaliza muda wake utaamini ni kweli?
 
Sasa kwa nini wasingeahirisha kwanza hadi wa-resolve hizo issue badala ya kuwachosha watu kuja na kuishia kuambulia maneno.
Sasa hayo maneno wangewaambilia wapi.
Kama sio kwa mkutano.

Walikuwa wanaprovide way forward kwa yale wanayodai haki haijatendeka.
 
Kama ulifuatilia mkutano huu na kama ulimfuatilia Mnyika , usingeleta uzi huu
Hakuna sababu yeyote ingemzuia leo mgombea kujinadi. Unaniita kwako nije kula pilau,nikifika kwako unanipa ugali eti pilau siku nyingine tena 😭😭😭😭😭come on. Leo wamechemsha. Kubalini tu.
 
Siku ya kwanza hii, kaa mkao wa kula sasa
Siku ya kwanza ndio ilitakiwa itoe mwanga wa nini kinaenda kuongelewa kwenye kampeni zao..

Sasa yeye anaongelea kupigwa risasi mkutano mzima hakuna sera hata moja wala nini ataenda kufanya..

Kwa mtindo huo wasitegemee watapata wasikilizaji kwenye hiyo mikutano yao..
 
Kususia kutoa hotuba kuna lengo la kuonyesha u-seriousness wa shida iliyopo mbele. Muda wa kumwaga sera badoooo ndiyo kwanza unaanza. Unajua mwaka 2015 CCM walipata mteremko sana kwa sababu Lowassa alikuwa hawezi kutamba jukwaani. Mpaka Magufuli akaonekana ni mzuri kumbe wapi. Hii kampeni itawasumbua sana CCM kwani kosa alilofanya Magufuli ya kuzuia mikutano ya wapinzani halafu yeye akawa anatamba mwenyewe kulimfanya adhanie kuwa anapendeka na kuheshimika na wananchi wengi sana. Sasa hivi anapokumbana na reality check anajikuta anachanganyikiwa. Hivi kosa kama lile la kuweka picha ya namna ile kwenye fomu badala ya kuweka picha ya halisi ya passport size ukiambia limefanywa na rais anayemaliza muda wake utaamini ni kweli?
Leo Lissu alitakiwa awashe moto.Sasa hii ya leo itawapa CCM la kusema kesho. Believe me kesho CCM watatamba sana. Watapiga vijembe mpaka basi.
 
Huyu Victoire ni mnafiki tena mnafiki mkubwa sana, usiwahi kuthubutu hata kidogo ukamuamini.

Nimebahatika kuona makaburi yake kadhaa humu HAFAI.
Ila wewe ndio umechekesha
Unaacha kujibu hoja unaanza kufukua makaburi !!!!! Hahahahhaa
Jibu hoja acha kumfuatilia mtu alichoandika zamani binadamu tunabadilika kila uchwao
Mm wa Leo sio Yule was Jana
Na hii inatokana na kupitia Mambo mbalimbali na kujifunza kila siku
 
Hapo kwenye maandamano ndo pagumu. Watanzania hawawezi kuandamana.
Kama hawawezi kuandamana maana yake hawataki haki any way acha tuone Kama Lissu ataandamana pekee yake kesho Kama kweli watanzania hawawezi kuandamana
 
Leo Lissu alitakiwa awashe moto.Sasa hii ya leo itawapa CCM la kusema kesho. Believe me kesho CCM watatamba sana. Watapiga vijembe mpaka basi.
Wewe huna ulijuwalo, kesho Chadema wapo Tanganyika Packers.

Vijembe ndio uwezo wa ccm kisiass, zaidi ya vijembe wana jipya gani?
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.

Utakuwa hukumsikiliza, hivi aliposema aliandaa hotuba ya uzinduzi wa kampeni yenye kurasa 20 lakini hataweza kuisoma hadi siku nyingine ulikuwa unaongea na simu. Maana hakufanya kampeni leo bali ametoa tamko la. CDM kifuatia kuenguliwa wagombea ubunge na madiwani.
 
Back
Top Bottom