Lissu: Rais Samia akiniteua katika Serikali yake atakuwa hanipendi

Lissu: Rais Samia akiniteua katika Serikali yake atakuwa hanipendi

Akihojiwa na mtangazaji wa Star Tv bwana Odemba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Lissu amesema endapo Rais Samia atamteua kushika nafasi yoyote katika serikali basi atajua kuwa hampendi.

Kwa kifupi Tundu Lissu amesema hawezi kukubali uteuzi wowote ndani ya serikali kwa sababu atakuwa amezibwa mdomo kwa kutoa mawazo mbadala. Amesema yeye hawezi kuwa ndani ya serikali ili abaki huru kusema mazuri na mabaya ya serikali!
Huyu lisu niliwai mskia akisema yeye ni born rebel,
Hata chadema ikiingia ikulu anahis hata enjoy tena itabd ahamie upinzni tena ili aweze kukosoa..
 
Mtu anayekuteua ni udhihirisho wa kukupenda. Asingempenda asingemtembelea Nairobi na kukutana naye Ubelgiji. TL angesema hawezi kufanya kazi chini ya mifumo mibovu ya serikali pasipo mabadiliko au katiba mpya!

Hata hivyo, aliyeko serikalini hazuiwi kukosoa mabaya na kupongeza mazuri. Akubali kuteuliwa pasipo kuacha misimamo yake ya kutetea haki na kuinyoosha serikali.

Ndivyo alivyo Othman Masoud na ndivyo alivyokuwa Maalim Seif.
 
Ni kwamba kama Rais atamteua kushika nafasi yo yote katika serikali basi atakuwa kama amefungwa na hatakuwa huru tena kuikosoa serikali.
Vp kuhusu kukubali teuzi? Atakubali na kujua kuwa Rais hampendi au atakataa huo uteuzi?
 
Una kichwa kigumu hatari
Ndiyo, nikigumu kweli kweli, nashukuru kwa appreciation. Wengine wanabaki nalo moyoni bila hata kunipa pongezi. Mwanaume hutakiwa kuwa na kichwa legelege utakimbiwa.
 
Mtu anayekuteua ni udhihirisho wa kukupenda. Asingempenda asingemtembelea Nairobi na kukutana naye Ubelgiji. TL angesema hawezi kufanya kazi chini ya mifumo mibovu ya serikali pasipo mabadiliko au katiba mpya!

Hata hivyo, aliyeko serikalini hazuiwi kukosoa mabaya na kupongeza mazuri. Akubali kuteuliwa pasipo kuacha misimamo yake ya kutetea haki na kuinyoosha serikali.

Ndivyo alivyo Othman Masoud na ndivyo alivyokuwa Maalim Seif.
Hao uliowataja hawakuteuliwa na Rais bali chama chao!
 
Kitila Mkumbo alimshauri Hayati Dr Magufuli aache kuteua Wana taaluma wa Vyuo vikuu ili wabaki kufundisha vyuoni…alipoteuliwa Yeye akitokea Udsm akashukuru sana na hata zile tuhuma zake za kufoji cheti Makonda zikaisha
 
Back
Top Bottom