Tundu Lissu anaongelea chanzo cha matatizo, watu wanaongelea Ugali ni akina Mh Wassira
Wassira amekuwa mkuu wa mkoa wa Mara miaka ya 1970+ , akawa Waziri wa Kilimo wakati wa Nyerere.
Mwezi uliopita alikuwa Tarime kama Makamu Mwenyekiti wa CCM akiwaasa Vijana wasitumiwe na CHADEMA, watulie Tarime Serikali itawawezesha katika kilimo na Mifugo.
Huyu mtu ujana wake alikuwa RC Mkoa wa Mara na Tarime ikiwemo, akawa Waziri wa Kilimo hakuweza kubadilisha maisha ya Vijana wa Tarime, leo anaongelea '' ugali, huduma n.k.'' kama anavyoshauri
Missile of the Nation . Yaani aliyeshindwa kutatua tatizo ndiye anayeongelea tatizo lile lile aliloshindwa
Missile of the Nation anataka tuongelee bei za vibaba vya unga, tusiongelee sheria za manununzi zinazokiukwa kwa kununua Magari V8 500 ya kutembelea. Tuna tatizo kubwa katika jamii hasa tunavyofikiri