Pre GE2025 Lissu: UDSM na vyuo vikuu vingine vya Tanzania vimekuwa magereza ambako mijadala ya kisiasa imefungiwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lazima ashuughulike kwanza na yale yanayofanya watu kuwa masikini, kisha maji huu meme vitapatikana kwa urahisi
 
Ukiwashauri hivi wanakuona una chuki!! Hata katika majukwaa Lissu huzungumzia sana mambo ya sheria na katiba na uchaguzi vitu ambavyo kihalisia humnufaisha yeye binafsi na wanasiasa!!
Lissu si rahisi kuuzika kwa umma kwa hizi ajenda za kibinafsi.
Chuki yako ya uchaguzi haiishi tu
 
Vijana wa fashion na siasa wapi na wapi, vyuo ilikua zamani.

Hivi sasa ni kuzalisha chawa tu, kama jinsi ambavyo wanaume wengi wanalialia mitandaoni juu ya tabia za wake zao/wanawake ndivyo ilivyo kwa wanavyuo nao kilichobaki ni kulialia mitandaoni bila kusuggest nini kifanyike ama lah ataishia kutoa lawama huku akimuomba mama awasaidie.
 
Waliosoma Mlimani wanaona ndo wenye akili,

Naweza pata nafasi kampla au Amazon college?.
 
Kuna Waziri Mkuu mmoja enzi za chama kimoja awamu ya pili aliwashambulia sana wabunge kwa kupoteza muda na nguvu nyingi kujadili ubovu mkubwa wa vyama vya ushirika badala ya kujadili namna ya kuwasaidia na kuwawezesha wakulima jinsi ya kupata pembejeo bora, za kutosha kwa bei nafuu na wakati muafaka; jinsi ya kuvuna na kuhifadhi mazao yao kwa ufanisi; na jinsi ya kupata masoko mazuri kwa mazao yao.

Watu walimsifu sana yule Waziri mkuu kwa kuzungumzia masuala ambayo ni relevant kwa wakulima na kuwaponda wabunge kwa kuhangaika na vitu visivyo na tija! walisahau kuwa enzi zile, serikali ya kijamaa ilivipa vyama vya ushirika ukiritimba wa masuala yote ya kilimo. Pembejeo, viwatilifu, magunia, uchakataji wa awali na masoko, n.k. vyote vilikuwa chini ya vyama vya ushirika. Sekta binafsi haikuwa na nafasi kabisa. Vyama vya ushirika vilijaa rushwa, ufisadi na uzembe wa kila namna kiasi cha kudidimiza sana sekta nzima ya kilimo. Huyo Waziri Mkuu leo hii ana heshima kubwa sana kwenye jamii anaongea "busara" tupu siku hizi.

Kuna kitu kinaitwa context (mazingira). Vyama vya ushikrika vilikuwa context muhimu sana kwa sekta ya kilimo na shughuli za wakulima nchini enzi zile. Yale yote aliyosisitiza Waziri Mkuu yule yasingeweza kupata ufumbuzi nje ya vyama vya ushirika. Labda sera ingebadilishwa kuondoa ukiritimba wa vyama vya ushirika (context reform) - jambo ambalo serikali na chama tawala hawakuwa tayari kulifanya. Yamekuja kufanywa baadaye sana baada ya kuacha madhara makubwa yasiyoisha kwenye sekta.

Hayo yote unayoita "issue zinazohusu maisha ya kila siku ya wananchi" pia "vitu vinavyohusu ugali wao" havitapata jawabu kamwe katika mazingira mabovu hasa ya kikatiba, kisheria, kisiasa na kiutawala yaliyopo hivi sasa nchini. Lissu anashughulikia the context ili kutengeneza mazingira bora yatakayoiwajibisha serikali inayokuwa madarakani itumie rasilimali za taifa kwa usahihi na ufanisi kutatua matatizo ya wananchi.

Masuala ya Katiba, Sheria, na mifumo ya utawala bora ndio kipaumbele cha sasa katika suala zima la maendeleo ya taifa hili. Asiyeuona ukweli huo basi itakuwa ama ni tatizo la kukosa uelewa (ignorance) au tatizo la kutojali mustakabali wa nchi na wananchi. Wananchi wanatakiwa kuelimishwa kuhusu haya masuala wakati wote badala ya kufanyiwa janja janja za kitapeli.
 

Hakuna mahali hii mada imesema Lissu aachane na mambo yake ya sheria. Tunasema kuwa mwananchi ni zaidi ya sheria, kuna uchumi pia!.
Vyama vya siasa ni pamoja na sera mbadala wa mambo mengi.
 
Lisu ni akili kubwa sana, ndiyo maana huwa anaongelea zaidi mambo yanayohusu chanzo cha matatizo yetu, kuliko kuongelea matokeo.

Kukosa maji, chakula, umaskini, ni matokeo. Tukitaka kutoka mahali tulipo, lazima twende kwenye chanzo cha matatizo.
Inahitaji akili sana kumwelewa TAL, kwa bahati mbaya sana Watanzania wengi hawana weledi huo.

Jumapili iliyopita TAL aliongelea ugawaji wa majimbo ya uchaguzi. Juzi Mwenyekiti wa ''INEC '' akasema majimbo yatagawanywa kwa kuzingatia huduma! Kaazima kazi ya TAL.
Wasiojua watasema '' haina ugali'' wanaojua watajua ina maana gani

TAL ataongeleaje ugali, umeme, afya wakati huduma hizo zinategema fedha! TAL anaongelea taarifa ya CAG na jinsi sheria zilivyo lose na kuruhusu Trilioni kuibiwa, pesa ambazo zingepunguza makali ya kodi ya Ugali, kujenga shule , afya n.k. Watu hawamwelewi TAL kwasababu anaongea level ya juu sana
 
Huu nao ni ujinga mwingine wa miwa go cha juu! Yaani theme inazungumzia legacy ya mwalimu kwa mtazamo wa demokrasia, then aanze kuzungumzia wamachinga?
 
Tundu Lissu anaongelea chanzo cha matatizo, watu wanaongelea Ugali ni akina Mh Wassira

Wassira amekuwa mkuu wa mkoa wa Mara miaka ya 1970+ , akawa Waziri wa Kilimo wakati wa Nyerere.
Mwezi uliopita alikuwa Tarime kama Makamu Mwenyekiti wa CCM akiwaasa Vijana wasitumiwe na CHADEMA, watulie Tarime Serikali itawawezesha katika kilimo na Mifugo.

Huyu mtu ujana wake alikuwa RC Mkoa wa Mara na Tarime ikiwemo, akawa Waziri wa Kilimo hakuweza kubadilisha maisha ya Vijana wa Tarime, leo anaongelea '' ugali, huduma n.k.'' kama anavyoshauri Missile of the Nation . Yaani aliyeshindwa kutatua tatizo ndiye anayeongelea tatizo lile lile aliloshindwa

Missile of the Nation anataka tuongelee bei za vibaba vya unga, tusiongelee sheria za manununzi zinazokiukwa kwa kununua Magari V8 500 ya kutembelea. Tuna tatizo kubwa katika jamii hasa tunavyofikiri
 
Pumbaf kabisa ww ni zero brain
 
.
 
Kiongozi nawe unakuwa serious na huyo lissu?!! Mwache aropokee mwisho akwende zake basi
 

Bei ya mkate ni political issue.

Kama hili hamlioni, basi mnapenda siasa za vifungu vya sheria zaidi kuliko yale yanayomatter zaidi kwa wananchi wengi.

Sheria inaprovide "order" ambayo ni meta-need, ila mkate ni basic need ambayo ndiyo msingi wa uhai duniani (msome Maslow).

Ukitaka kujua kuwa bei ya mkate na unga ni political issue na ni priority kubwa sana, wape wananchi choice kuwa tuendelee na tume hiihii na tufanye bei ya unga ni ndogo AU tuwape tume mpya lakini Bei ya Unga iwe juu. Kisha lete mrejesho wa maamuzi ya wananchi wengi.

Kiufupi, Wananchi wataiunga mkono CHADEMA zaidi ikifanya BOTH, yaani kupigania hizo sheria zao na kupigania mambo yao ya Ugali. Not one at the expense of the other.
 
Kwa taarifa yako maisha ya kila siku ni ''political issue''. Hakuna kitu kisichohusiana na siasa
Ukisoma Katiba kwa nia ya kuielewa utaelewa nakuambia nini. Kwahiyo, unapoacha kuzungumzia source ukadakia matokeo ni hatari sana.

''Homa'' si ugonjwa ni dalili ya Ugonjwa. Daktari hutibu chanzo cha ''Homa'' si kupunguza maumivu ya Homa. Ukimpa mtu '' Panadol a.k.a mkate '' unapunguza maumivu hutibu ugonjwa.
TAL anazungumzia chanzo cha matatizo si kutoa panadol kutwa mara 3
Yes kwa Tanzania ni kweli, watu wanauza hadi kura kwa kofia za CCM. Kwa Mataifa yenye weledi choice yao hawezi kuwa Mkate !
Kiufupi, Wananchi wataiunga mkono CHADEMA zaidi ikifanya BOTH, yaani kupigania hizo sheria zao na kupigania mambo yao ya Ugali. Not one at the expense of the other.
Yes nadhani ndicho wanafanya, hii haina maana wazungumzie mkate tu na Ugali bila kuwaeleza Watanzania nini chanzo chake, miaka 63 baada ya mkoloni kuondoka
 

Unfortunately Lissu hazungumzii "Ugali" wa wananchi "almost" kabisa.
 
Duu!! Hivi ni hayo matatizo uliyoyataja ndio huleta shida kwa watu au hayo unayosema yupo busy ndio huleta hayo matatizo ya watu? Kweli akili ni nywele ila cc black people nywele zetu ni fupi! Sijui unausadifu msemo huu!!
 
Tapeli la kisiasa
 
Huyu jamaa ni genius sana,I hope TISS wanaona namna mtu sahihi anatakiwa kuendesha taifa hili
Yaani ukimpima nyani kwa namna anavyoruka kwenye matawi ya miti, utamuona ni genius kuliko kobe.

Kama Lissu ni genius basi nchi yetu haina watu wenye akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…