Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits

Pamoja na mazuri yake mengi, kuua mfumo wa vyama vingi kwa takribani miaka 30 ulikuwa ni uamuzi mbaya sana. Mpaka sasa taifa hili bado linakabiliwa na kivuli kizito cha utawala wa chama kimoja kutokana na legacy hiyo.
Ulikua uamuzi mbaya kwa maoni yako wewe, demokrasia ya vyama vingi sio maji kwamba kila mtu lazima atakunywa. China hakuna vyama vingi, Saud arabia pia nk. Huko kote kuna maisha na maendeleo makubwa kuliko nchi za vyama vingi
 
Wewe mkuu kweli ni thinker na unaweza ku critise bila kutukan.
Tundu Lissu angekuwa hivyo hakuna mtu angemsumbua.
Hata siku anamaliza muda wake Mwalimu alisema tena hadharani kuwa kama binadamu kuna mabo watanzania wamsamehe, kwani alifanya kwa nia njema.
Sra za viji vya ujamaa na kuwakusanya atu kwa nguvu, lile halikuwa zuri.
Na Mwalimu hadi alitoa machozi wakati akimwomba msamaha Rashidi Kawawa kuwa alilaumiwa sana kwa niaba yake, lakini Kawawa hakuacha kumuamini Mwalimu.

Sisi ni binadamu tunakosea, tuombe radhi pale tunapokosea.

Lakini kumtukana Mwalimu, kumkebehi na kumdhalilisha Lissu styel, madara yake ni makubwa.
 
Lakini kumtukana Mwalimu, kumkebehi na kumdhalilisha Lissu styel, madara yake ni makubwa.
Kwa sifa zingine zote ulizonipa sawa, nashukuru..

Ninachokikataa ni hiki ambacho na wewe unakisema hapa..

Tangu lini kutofautina na kupinga mtazamo na mawazo juu ya mtu fulani kiongozi anachotenda na aliyowahi kutenda ikawa ni matusi na kumdhalilisha?

Tundu Lissu hajawahi kumtukana wala kumdhalilisha Hayati Mwl Nyerere unless uoneshe mifano ya matusi hayo!!
 
Unamzungumzia Tundu huyu aliyesema Serikali itafungwa jela sababu ya makinikia...Tundu huyu anayetetea ushoga..au Kuna mwingine
Unadhani ustahili kujibiwa kweli wewe?

Sentensi hii pekee inakutosha
 
umesema ukweli ambao mungu anaoutaka! huwezi kuijenga tanzania imara bila kwanza kukosoa utendaji mbovu wa waliotangulia kuufanya. Hivi leo watanzania wengi hatujui kuongea kiingereza kwa sababu ya mtu mmoja tuu kuamua kingereza kifutwe mashuleni. hivi hiyo ni sawa kweli? leo hata michezo ya jumuia ya madola tunashindwa kuchati na wenzenzetu ambao ni wanachama.
 
Acha kuzingua, acha watu waongee, unafiki kitu cha ovyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…