Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Hujamuelewa Lissu,rudia kusoma tena alichokiandika!Huoni anapendekeza tuwe kama hao uliowataja na tutoke hapa tulipo?Yaani kama ni kiswahili basi ndio kiwe lugha ya kufundishia,na kama ni kiingereza basi tuanze nacho toka chini!
Hivi hamuoni watoto wanaotoka medium schools wanakuwa na ahueni sekondari?
Sasahivi kwanini kila mwenye uwezo anamkimbiza mwanaye medium schools na sio hizi zetu za akina kayumba?
Tafakari!
 
Swali kwako mheshimiwa sana hzo nchi ulizotaja ipi lugha zao za taifa na ip inatumika ktk kufundishia kisha rudi bongo kama hutoona usanii mtupu
 

Mimi nadhani tatizo tulilonalo kwenye elimu yetu ni mitaala tu. Iboreshwe na iendane na uhalisia wa mazingira ya sasa na wakati tuliopo. Lugha sio tatizo. Lugha ni juhudi tu binafsi ya mtu mwenyewe kuweka bidii katika kujifunza.

Wanafunzi wakijizoesha kuzungumza kingereza wata master tu vizuri. Tatizo ni pale mtu anataka kuongea kama muingereza, hiyo haiwezekani. Na wengi hawajui kuongea hicho kingereza maana hata hawataki kujifunza kuongea. Wao wanataka waanze kukiongeaa wakiwa fluent..sasa utakuwa vipi fluent kabla hujachapia?

Ku master lugha yoyote ni kufanya practice mara kwa mara. Mfumo wetu wa elimu uko vizuri tu. Hapo kwenye mitaala ndio wabadilishe na kuboresha.
 
MATAGA bwana! China kwa taarifa imewekeza mno kwenye Kiingereza sasa.
Kwa taarifa yako tu ni kwamba, China ndiyo nchi inayoongoza kwa idadi ya watu watu wanaoongea Kiingereza kuliko nchi yoyote ile duniani.
 
We mataga acha kujishebedua, kwann lugha ya kufundishia ni kiingereza?
Hata wewe uelewa wako ni mdogo sana hujui kuwa kwa sasa sera yetu ni kukuza lugha yetu ya kiswahili ili iwe lugha ya Afrika na imeshaanza kukubalika sasa inatumika SADC!! Kweli wanasaccos hawajitambui
 
Sawa mkuu,ila kwa sasa kila mtu mwenye uwezo anamkimbiza mtoto wake medium schools!Hata wewe unaweza ukawa mchangiaji hapa ila mtoto wako yuko medium!Nikuambie tu mtoto mdogo ni rahisi kushika lugha kuliko akishakua!Shule za kayumba,lugha ya mawasiliano ni kiswahili,mtoto anapata wapi nafasi ya kufanyia mazoezi tenses anazojifunza darasani kwenye somo la kiingereza?Mtoto anaenda kuanza form 1,kuelewa somo inakuwa kazi!Masomo kama physics,chemistry,biology,geography inamlazimu awe anakariri sana kuliko kuelewa!Nimepita huko na kwakweli somo ambalo nilikuwa tayari kufanya mtihani wakati wowote ni hesabu maana haina maelezo!
Tuna changamoto kubwa sana ya lugha na hapo kwenye mitaala ulipotaja!Alichoshauri Lissu ni mjadala utakaokuja na majibu,sioni ubaya katika hilo!
Tatizo la lugha lipo na ni kubwa!
 
Miaka 59 ya chama cha makanikia kijani kibichi wameharibu kila sekta ,kila idara .
 
Mkuu nakubaliana na wewe sn naomba upite hapa kwenye huu uzi na ndipo utamuelewa Lissu alimaanisha nn, ofcz kwenye hilo suala namuunga mkono Lissu 100%, pita hapa kiongozi [emoji116][emoji116][emoji116]
[emoji116][emoji116][emoji116]

Kiingereza na somo la computer ni muhimu kwa maendeleo ya elimu yetu Tanzania

Kiingereza na somo la computer ni muhimu kwa maendeleo ya elimu yetu Tanzania
 
Ukijua kingereza halafu kichwani empty minded itakusaidia nini?
Hata mfumo wa ufundishaji ubadilike ni yale yale kama Kiswahili chenyewe mtu anakuambia kigumu mpaka Kamusi zetu sanifu zinatoka Kenya nothing new

Tatizo sio lugha ni mfumo wa elimu
 
K
In

Ingawa mimi lugha sina shida nayo ila leo huyu mkuu kaongea vizuri.unakuta unamtambulisha mh kwa jamaa akianza lugha duh aibu halafu eitni waziri
 

Mkuu kwani kujifunza kingereza na kuweza kuongea inachukua muda gani? Ndio sembuse miaka 6 ya darasani..hapo kuna uzembe. Halafu kama lugha ndio shida katika kujifunza na kufundishia vipi kwa wale wanaofeli shule za msingi? Kuna ambao hadi wanamaliza darasa la sabu hata kuandika insha ya maneno mia moja ni kazi.. hao tatizo inakuwa ni nini wakati lugha ni hiyo ya kila siku na kila wakati kiswahili?
Shida ni mitaala ya elimu yetu ni mibovu..lugha kila mwenye nia n akiweke juhudi ataiweza tu vizuri. Kuna sehemu watu hata hawakumaliza darasa la saba vizuri waliishia njiani lakini wako mtaani huko na wazungu wanavunja kingereza vizuri tu ma-fly catchers sasa ndio sembuse mtu amekaa darasani miaka 6 aseme ana tatizo la lugha ya kiingeteza? Huo ni uzembe.
 
Hahahah naona hata wewe umetumia lugha ya malkia kuipigia chapuo lugha ya kiswahili.

Lofa kabisa in " the late voice"
 
Hv unaelewa unachokiongea
 
Mimi nilisoma kijijini huko kasulu japo si mzawa wa huko!Ila darasani wakati mwingine mwalimu alikuwa akiona watoto hawaelewi anapiga hadi kiha(lugha ya asili) ili watoto waelewe!Ambao nilikuwa nasoma nao,hata kuwasiliana kwa kiswahili ilikuwa ngumu!So hayo ya mtoto wa darasa la saba kutomudu kuandika insha inawezekana kulingana na mazingira!
Je,medium schools umeona watoto wa namna hiyo?Huko kuna kitu gani special mpaka isiwe hivyo?
Vyuoni huko ni aibu,nilimaliza degree Engineering hapo UDSM na GPA nzuri sana awamu ya Kikwete,baadaye nilipata fursa ya kusomeshwa masters Uholanzi bure na taasisi moja ya global education!Nilichotakiwa kufanya mtihani wa IELTS kwenye centre mojawapo ya british council!IELTS maana yake ni International English Language Testing System!Nikalipia 300,000 kama ada ya mtihani!Hapa unafanya mitihani 4,Speaking,Hearing,Writing na Reading!
So unapofanya wanakurate kati ya 1 mpaka 9,mimi nilipiga point 6.5 kama wastani!Chuo kilihitaji point 7 ili nidahiliwe!Nikasema haina shida,nikaenda kozi kujiongezea ufundi miezi 3 ili niwahi deadline ya chuo!Nikalipia tena laki 3 nikaingia kwenye test nikascore point zilezile 6.5!Ndoto zangu zikafia hapo!
Ninachosema kuna vitu basic ambavyo ukiwa mtoto ni rahisi kuvishika na vikakukaa!Nilikosa fursa kwa sababu ya lugha!Ningekuwa nimepita shule zenye msingi mzuri wa kiingereza kama hizi medium ningekuwa mbali sana!
So inapokuja hoja kama hii anayoisema Lissu,wengine ni wahanga na tunaielewa sana!Mkuu hii hoja imenihuzunisha sana na imenikumbusha mbali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…