Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Lisu kaongea ukweli kuhusu swala la lugha ya kufundishia. Vijana wetu wengi hawapati maarifa ya kutosha shuleni na vyuoni kwa sababu ya kutoelewa lugha wanayofundishiwa. Mfano, mtihani wa kidato cha 4 wanafuzi wengi wasingepata 0. mtihani huo ni rahisi na maswali mengine ni ya kawaida sana. lakini ukiangalia matokeo utaona nusu au zaid ya wahitimu hupata alama 4 au 0.

Watanzania tuwe wakweli tuache unafiki na ushabiki. Elimu yetu ipo mahututi , na selikali ya CCM haitaki kulikubali hilo.
Raisi wetu ni mhanga wa mfumo huo, mawaziri wabunge wote ni wahanga lakini hakuna anaechukua hatua.

Tanzania itaendelea endapo tutawekeza kenye elimu sio elimu majengo bali ubora
 
Muongee kiingereza humu tusipoelewana Lissu yuko sawa tukielewana hayuko sawa Alahh[emoji34][emoji34][emoji34]
Anatuchuliaje Wa Tz Kisa yeye anakijua na amesoma Sheria
 
Kiswahili chenyewe unakijua?
Kuna watu hadi leo wanaingia shule hawajui hicho kiswahili unachokipigania.

Pili inawezekana kukijua kiingereza vizuri na tukaendelea kutumia kiswahili.
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
 
Mbona umeongea pumba mkuu. Kwani China ina lugha mbili katika mambo yao?

Kisayansi, sehemu ya ubongo inayohusika na ulimi (lugha) hukua na kufikia karibia na kikomo katika muda wa miaka 0 mpaka 14. Na umri huu hapa kwetu mtoto huyu yuko shule ya msingi. Anakwenda form 1 akiwa hajui na hapo anabadilisha lugha ya kufundishia kwa kiingereza. Anakwenda tayari na uwezo mdogo sana.

Point ni ndimi mbili. Kiswahili au Kiingereza??? Wanaotaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia ni wale wasiohitaji lugha nyingine. Wanaotaka Kiingereza kianzie chini ndio hasa wanaojua mapungufu ya kiswahili katika fani! Tumebaki kuona kiswahili kama ni jambo muhimu kuliko ufahamu. Kuna wanafunzi wengi sana wanafeli si kwa kuwa hawana uwezo wa kushika mambo akilini - baki kwa sababu hawaelewi hata wanachofundishwa.

Muulize mwalimu atakuambia ili uelewe jambo na kulishika, jambo hilo litapaswa kuelezwa katika lugha unayoifahamu zaidi. Watoto wetu wanafundishwa kwa kutumia kiingereza lakini kwa sababu ya kutokielewa - wanatumia kishwahili na lugha za kinyumbani. Anatumia muda mwingi kujaribu kuelewa badala ya kushika tu!
 
Kiswahili ni lugha ngumu linapokuja suala la sayansi.
Misamiati ni migumu wala haina uhusiano na kitu kinachoekezewa.
Mfano tungamo,ujazo nene,kishikwambi,na ujinga mwingi kama huo..
Mbona umeongea pumba mkuu. Kwani China ina lugha mbili katika mambo yao?

Kisayansi, sehemu ya ubongo inayohusika na ulimi (lugha) hukua na kufikia karibia na kikomo katika muda wa miaka 0 mpaka 14. Na umri huu hapa kwetu mtoto huyu yuko shule ya msingi. Anakwenda form 1 akiwa hajui na hapo anabadilisha lugha ya kufundishia kwa kiingereza. Anakwenda tayari na uwezo mdogo sana.

Point ni ndimi mbili. Kiswahili au Kiingereza??? Wanaotaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia ni wale wasiohitaji lugha nyingine. Wanaotaka Kiingereza kianzie chini ndio hasa wanaojua mapungufu ya kiswahili katika fani! Tumebaki kuona kiswahili kama ni jambo muhimu kuliko ufahamu. Kuna wanafunzi wengi sana wanafeli si kwa kuwa hawana uwezo wa kushika mambo akilini - baki kwa sababu hawaelewi hata wanachofundishwa.

Muulize mwalimu atakuambia ili uelewe jambo na kulishika, jambo hilo litapaswa kuelezwa katika lugha unayoifahamu zaidi. Watoto wetu wanafundishwa kwa kutumia kiingereza lakini kwa sababu ya kutokielewa - wanatumia kishwahili na lugha za kinyumbani. Anatumia muda mwingi kujaribu kuelewa badala ya kushika tu!
 
Kiingereza ni kama kijaluo tuu, mbona wachina wengi hawajui kiingereza na wako vizuri kichwani,lissu ni miongoni mwa wale wakiona mtoto mdogo wa kizungu anaongea kiingereza wanamshangaa. Nakusema "mtoto huyu ana akili sana".
 
Kati ya siku lissu ameongea ujinga na utumbo ni leo, yaani lugha iwe kigezo cha kutopata maendeleo, hapana watanzania sio wajinga kiasi hicho, swali lakujiuliza kwa nini kumekuwa na taaluma ya Tafsiri na Ukarimani. Lisu jipange upya nchi kama urusi, uchina nchi za falme za kiarabu wanatumia lugha zao na wako vizuri kiuchumi.

Daaah! Jaribu kutumia akili japo kidogo tu; Ebu fikiria mtoto anapoanza Elimu ya msingi anakuta lugha ya kufundishia ni Kiswahili mara paaah anaingia form one anakuta lugha imebadilika juu kwa juu huku huyu mtoto anang'ang'ana kujua Kiingereza hapohapo anakutana na mitihani huku hajajua lugha vizuri kwa hali kama hiyo mtoto atafeli tu mitihani maana atajikuta anatumia nguvu nyingi na muda mrefu kwa kujifunza lugha kwanza huku masomo pia yanamsubiri mara paaah anajikuta amemaliza form 4 bila kujua chochote!
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu

Umepanic mzee mwenzang maana yake ni kua nchi haina lugha maalum ya kufundishia (language of instruction) kitu ambacho kimesababisha wengi wetu hatupo competent kwenye kiswahil wala kiingereza
Kiswahil hatujui na kiingereza hatujui
Usipanic
 
Hapa mh Tundu Lissu anataka kumaanisha nini hasa wakuu hebu tusaidiane kidogo.

Amesema kingereza watu hawakijui japo wanasoma kwa muda mrefu tangu O level hadi A level lakini bado ni tatizo kwao.
Lakini pia amesema kuwa kingereza ni muhimu hususani katika suala zima la interaction with foreigners kwamba tunakosa vitu muhimu kwasababu hatujui kingereza.

Sasa hapa ningeomba mnisaidie wakuu.

Kama tatizo ni lunga ya kufindishia ambapo kwa sasa secondary inatumika kingereza na msingi ni kiswahili. Imaana ili sasa wajue kingereza Lugha ya kufundishia mashuleni iwe kingereza kuanzia chekechea hadi chuo kikuu ndipo watu watajua zaidi kingereza?

Kama jibu ni ndio hii italeta matokeo gani kwenye Lugha yetu ya kiswahili baada ya miaka 10-20 ya utekeleza wa hii sera?

Kizazi kijacho kitakuwa wazungumzaji tena wa Kiswahili Kama sasa tulivyo?

Utamaduni wetu Kama watanzania utaishia wapi?

Tukisema pia tuchague Lugha ya kiswahili ndio iwe ya kufundishia mashuleni katika ngazi zote za Elimu je hapo napo kutakuwa na matokeo gani baada ya miaka 20 ya hii sera?

Hapo sasa sio ndio idadi ya wazungumzaji wa kingereza itashuka zaidi na muingiliano wetu na mataifa ya nje utakuwa mgumu zaidi na tutapoteza fursa nyingi zaidi kuliko sasa?

Huyu aliye weka hii sera ya kuchanganya hizi Lugha kwenye Elimu yetu tutaweza kumuweka kwenye fungu hasi ama chanya ikiwa tu tutajibu hasara na faida na mifumo yote miwili Kama itatumika kwenye Elimu yetu.
 
Nenda English course..

Kwa hiyo kuwa msomi ni kujua kingereza?

Hata yule beberu wake akisikia hivi ataona aibu sana
 
..TL amesema kutakuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu lugha inayofaa kufundishia.

..Yeye hajatupa karata yake kwamba twende na Kiswahili, au twende na Kiingereza.

..ukipata muda sikiliza hawa wataalamu wa lugha na waalimu wa muda mrefu hapa chini.

Huyu jamaa kila siku ana evolves he starts to put some brain 🧠 in his speech... yuko sahihi kama Taifa inabidi tuchague moja kiswahili mwanzo mwisho kingereza kisomwe kama foreign language au English as medium of instruction through out.
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Dah mkuu umeelewa kilicho zungumzwa lakini au umetumwa tu kuja kujibu?
 
Back
Top Bottom