List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Masatu are u suggesting Slaa ana ushahidi na can put verdict kwa hao jamaa...DREAM ON BRO!
 
Koba,

Tuliokuwa Mwembeyanga tumeambiwa ushahidi upo lakini cha kushangaza hapa anasubiriwa mtuhumiwa kwanza akafungue kesi ili mtuhuma aje kumwaga ushahidi! Kazi ipo kweli...
 
Koba,

Tuliokuwa Mwembeyanga tumeambiwa ushahidi upo lakini cha kushangaza hapa anasubiriwa mtuhumiwa kwanza akafungue kesi ili mtuhuma aje kumwaga ushahidi! Kazi ipo kweli...

Hakuna one formular au way (ambayo unapenda wewe) pekee tu itakayotumika kuwapa justice wezi wa CCM.... So far Slaa atafanya whatever the heck inafit mazingira ya Tanzania...

Wananchi wataelezwa na wataamua wenyewe cha kufanya! Na wewe unaweza kuanzisha fight yako ya wala rushwa na ukaipeleka mahakamani au bungeni kwa mdhihiri.......
 
What a ----...

umechambua nini zaidi ya kuuliza maswali tu .... CCM kwa kujipa majina makubwa .... mara mchambuzi mara nimechambua... hakuna ulichochambua hapa .....

Matusi hayatasaidia kumaliza rushwa....

Hii case haiendi bungeni wala mahakamani.... case hii ni kwa wananchi na wajichukulie sheria mkononi..... bungeni kwa kina mdhihiri wakaanzishe ngonjera kwenye issue muhimu?

Mko nani hapa?

ukimshika mwizi unafanya walichofanya polisi Arusha... unachapa risasi kama mvua. utawashangaa CCM vipi wakati wewe ni CCM?

Kama sio malumbano wewe unachofanya hapa ni nini?

Sina chakukujibu hapa mwafrika
 
Bado mnatafuta ushahidi tena katika hili au ile document hamjaisoma au mmeisoma lakini hamkuielewa?

Kwa nani mwenye jukumu la kwenda mahakama panapokuwa na tuhuma za kuhujumu uchumi wa nchi?
 
Koba,

Tuliokuwa Mwembeyanga tumeambiwa ushahidi upo lakini cha kushangaza hapa anasubiriwa mtuhumiwa kwanza akafungue kesi ili mtuhuma aje kumwaga ushahidi! Kazi ipo kweli...

Mtuhumiwa hasipofungua kesi manake hatahukumiwa na rushwa bado itaendelea kutesa. Chakushangaza, mtego wa Dr Slaa ni wa sisimizi maana ukisoma 'ushahidi' alioutoa unakuta katumia maneno ya ujanja kama "alishiriki na/au alifahidika na/au alinyamazia na /au alishauri vibaya serikali. " Practically Dr Slaa hajamshutumu yeyote ukiangalia sentense hizi...hivyo basi hao anaowasubiri waende mahakamani kabla ya yeye watakuwa wajinga, mana atatumia sentensi hizo hizo kukanusha kwamba hajawatuhumu. Kazi iko Tz.
 
Basi! Nimeamini kwamba Mgonjwa Ukimwi na Masatu ni wagonjwa wa akili. Hata kama wametumwa mambo mengine mtu mzima akitumwa kuyatetea anayakataa. Kama wamejituma basi, tujue nao ni wezi tu kama hao wanaowatetea.
 
Rais Nyerere alipokuwa akihutubia kwenye ule mkutano wa Mei Mosi 1995 alisema kitu kimoja ambacho ni kizito sana... alisema "Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kipumbavu huku akijua kuwa na wewe una akili, na wewe ukalikubali (jambo hilo) atakudharau"..
 
Katika posting yangu nimechambua ushahidi wa Dr Slaa ambao ameutoa dhidi ya watu aliowatuhumu. Na conclusion yangu ni kwamba tuhuma alizotoa ni mzito lakini ushahidi hafifu. Nilitegemea wachangiaji wenzangu waonyeshe wapi ushahidi wa Dr Slaa una strength, badala yake wachangiaji wengi wanajaribu kushawishi kwamba Dr Slaa anayajuwa mengi zaidi ya aliyoyasema. Mimi sio mtaalamu wa ndoto wala sio mpiga ramri, hivyo basi nachambua kile kilichosemwa.

Je Dr Slaa ni mjinga? Sidhani, ila kwa hili anastahili kuitwa mjinga machoni mwangu. Mwenye ushahidi wakutosha, mzalendo mpenda haki na maendeleo ya watu habembelezwi kuutoa, wala hakimbilii waandishi wa habari. Badala yake anakwenda mahakamani, na bungeni ikiwezekana. Dr Slaa hajafanya hivyo, badala yake ana-adaa wananchi wanaolia kwa kipindi kirefu juu ya rushwa.

JF tumekuwa mstari wa mbele kuipiga vita rushwa, ila kwa mshangao naona tuna double standard. Amina Chifupa (R.I.P)alipokatazwa kutoa press conference, JF kulikuwa na movement ya kushinikiza aruhusiwe. Nilitegemea JF kuwe na movement ya kumshinikiza Dr Slaa afungue kesi dhidi ya hao aliowatuhumu...tunapinga rushwa kweli JF ama tuna ibwekea tu?

Kama Dr Slaa ana ushahidi mzito zaidi ya huo alioutoa (kama wachangiaji wanavyojaribu kutuongopea)anasubiri nini kuwashitaki? Vyama kama CUF, TLP, NCCR, viko wapi wakati vina kila ushahidi dhidi ya watuhumiwa? Hivi hii sio BINGO kwa wapinzani? Nadhani Dr Slaa ameamua kutupa makengeza tuzani ukungu ni moshi.

Sasa wachangiaji wengine humu wamenichekesha, wakisema kwamba wanataka viongozi walioshutumiwa wamjibu Dr Slaa. Nadhani JF tunataka kuona malumbano badala ya suluhisho. Hatufiki tunakokusudia. Ukimshika mwizi unampeleka kwa pilato, wala hauhitaji kumhoji kama kaiba au lah, mana kama kuna possibility kwamba hajaiba basi kuna possibility kwamba sio mwizi. Na mwizi ana haki ya kukaa kimya unapomuhoji na akasubiri kwenda kujibu kwa pilato. Hasipokujibu na ukaishia kutokwenda kwa pilato haina mana kaiba, hata kama utampiga.

Kadhalika inanishangaza kuona kwamba JF tunalazimisha viongozi washutumiwa wamjibu Dr Slaa. Kana kwamba rushwa inapigwa vita kwa malumbano. By the way, nitawaona viongozi wa ccm wajinga endapo watajibu shutuma zenye ushahidi wa kuokotezea.

Again, uzalendo wa Dr Slaa sijauona katika hili. Huwezi kuitwa mpenda haki na mtetea wananchi wakati huo huo ushahidi ambao ungetoa maovu ya viongozi unauweka kibindoni, na unasubiri ubembelezwe uutoe. Huwezi kuitwa kiongozi bora kwa kuanzisha malumbano na wala rushwa kupitia waandishi wa habaru, badala ya kuwapeleka kwa pilato. Rushwa haipigwi vita kwa malumbano ya kisiasa.

Ahsante Mgonjwaukimwi,wengine tukisema humu tunaonekana kama tumetumwa.Lakini sio ndugu zanguni,mimi nafikiri kweli Dr slaa muda huu angekuwa kashabisha hodi mahakamani na sio kusubiri akina Kingunge watege Patrot zao!
 
Tatizo letu nini Watanzania? Wanaoibiwa na kuachwa hoi,sio Dr. Slaa ni sisi watanzania.

Masatu na Mgonjwa wa ukimwi,Chukua una duka na umeajiri mfanyakazi kukuuzia,lakini siku zote ni hasara tu hakuna faida.Anajitokeza msamalia akuambia bwana sisi huwa tumwona kijana wako anabeba mabox usiku toka dukani na kwenda kumuuzia yule mangi mtaa wa pili.

Utaawambia nileteeni ushahidi au Utanza kufanya utafiti? Tuchukue hukukubaliana nao ukwaambia nileteeni ushahidi nao wakaamua kukuacha kama ulivyo.Unafikiri nani anayeendelea pata hasara.

Hivi Balali au Mkapa angekuja mwembeyanga akasema jamani mimi nilipokuwa Madarakani nimeiba.Ungesema akuletee ushahidi?

Mia nafikiri Dr.Slaa na wenzake wamefanya kazi ya ziada sana tena katika mazingira magumu na hata tu kudiriki kutaja majina ambayo yalikuwa hayatajiki.

Ilikuwa sasa ni jukumu letu sisi wananchi,baada ya kuona viongozi wote waliotajwa wapo kimya, kuwalazimisha wafanye uchunguzi katika issues zote za BENKI NA MADINI. Ni dharau ya hali ya juu tunayoendelea kujijengea sisi wananchi kwa hawa viongozi majambazi,tunapowaacha na kuwakalia kimya huku tukiendelea kuwaambia akina Slaa watuletee ushahidi!!

Kuhusu suala la mahakamani.Nafikiri kuna sababu nyingi ambazo zinamfanya Dr.Slaa asiwe yeye wa kulipeleka mahakamani.

Mojawapo ni ugumu wa kumshitaki mahakamani Rais aliyeko madarakani(kwa mujibu wa katiba).Lakini ikiwa waliotuhumiwa watalipeleka mahakamani itakuwa ni rahisi sasa Dr.Slaa kuendelea nalo.
 
Wanakijiji: Barrick ilimdanganya Waziri Mkuu

na Chris Mang'era, Tarime
Tanzania Daima

WAKAZI wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa North Mara, uliopo wilayani Tarime, akiwamo Diwani wa Kata ya Kemambo, Agostino Neto Sasi, wameeleza kusikitishwa kwao na uongozi wa mgodi huo, kumpatia Waziri Mkuu, Edward Lowassa, taarifa zisizo sahihi kuwa umejenga shule 13 katika vijiji vinavyouzunguka.
"Tumesikitishwa sana na kitendo cha mgodi wa North Mara kumpatia kiongozi mkubwa wa nchi taarifa za uongo kwamba umejenga shule 13 katika vijiji vinavyouzunguka huku ukijua haujafanya kitu cha aina hiyo," alidai Sasi.

Katika mazungumzo na wanahabari mjini hapa juzi, baadhi ya wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi huo walidai taarifa yote aliyopatiwa waziri mkuu kuhusu miradi ya kijamii inayotekelezwa na mgodi huo ni ya uongo na hasa kinachowaumiza ni taarifa za madai ya ujenzi wa shule 13.

"Mimi sijawahi kushuhudia kiongozi wa nchi akidanganywa kiasi hicho… niseme tu kwamba karibu taarifa yote iliyotolewa na mgodi wa North Mara kwa waziri mkuu, kuhusu shughuli za maendeleo ya jamiii imejaa uongo.

"… ila kinachoumiza zaidi ni madai kuwa mgodi umejenga shule 13, jamani tutafika kweli kwa kudanganyana kiasi hicho?" alihoji mkazi wa Kijiji cha Kewanja, Gabriel Mwita.

Wanavijiji hao walitaja shule zilizojengwa na mgodi wa North Mara kuwa ni mbili, nazo ni Shule ya Sekondari ya Bwirege ambayo ilijengwa chini ya kiwango, kwa mujibu wa wataalamu na Shule ya Msingi Nyabichune ambayo hata hivyo, kwa sasa inakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu, hivyo kuwalazimu baadhi ya walimu kuishi kwenye stoo.

Walidai shule nyingine moja ya sekondari na 10 za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita kwa ushirikiano wa wanavijiji husika na serikali, nyingi kati ya hizo zilijengwa kabla ya mgodi huo kubinafsishwa.

Walieleza kwamba mchango uliotolewa na mgodi huo ni kugharimia ukarabati wa baadhi ya majengo ya shule hizo.

Wakizungumzia sh bilioni 42.6 ambazo mgodi wa North Mara ulidai kuzitumia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii katika vijiji hivyo hadi sasa, wananchi hao walisema hawaamini kama kuna kitu cha aina hiyo, kwa kuwa hakuna mwanakijiji aliyeshirikishwa katika matumizi hayo.

Hata hivyo, wanavijiji hao walibainisha fedha zinazotolewa na Kampuni ya Barrick kutekeleza sehemu za baadhi ya miradi ya maendeleo katika vijiji hivyo si msaada kama uongozi wa kampuni hiyo unavyodai, bali ni stahili inayopaswa kutolewa kila unapofanyika uzalishaji na mauzo ya dhahabu kulingana na mkataba uliowekwa kati ya mgodi huo na vijiji vitano ambavyo ni Matongo, Kewanja, Nyangoto, Genkuru na Kerende.

Naye mkazi wa Kijiji cha Kerende, Elia Maginga, alisema uongozi wa mgodi huyo ulijua wazi kuwa taarifa unayompatia Waziri Mkuu ni ya uongo ndio sababu uliamua kumsomea taarifa hiyo ndani ya ofisi ya kituo cha afya cha Nyamongo ambamo haikuwa rahisi kwa mwanakijiji wa kawaida kuingia na kusikiliza.

"Kama taarifa hiyo ingesomwa kwa waziri mkuu katika mkutano wa hadhara, wanavijiji tungeipinga, ili waziri agundue, lakini uongozi wa mgodi ulifahamu hilo ndiyo maana ukatumia ujanja wa kwenda kuisomea ndani ya ofisi ambamo mwanakijiji hakupata nafasi ya kuingia na kusikiliza," alisema Maginga.

Agosti 31, mwaka huu, waziri mkuu, akiwa ziarani mkoani Mara, alipata fursa ya kutembelea kituo cha afya cha Nyamongo, ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulimpatia taarifa ya shughuli na miradi mbalimbali ya kijamii iliyotekelezwa na mgodi huo katika vijiji vinavyouzunguka.

Katika taarifa hiyo, uongozi wa kampuni hiyo ulidai miongoni mwa shughuli za kijamii zilizotekelezwa na mgodi huo ujenzi wa shule 13, zikiwamo mbili za sekondari na 11 za msingi.

Mgodi huo unadai kujenga shule za sekondari za Nyamongo na Bwirege, pia shule za msingi Matongo, Nyansangero, Bung'eng'e, Nyabichune, Genkuru, Nyamwaga, Kerende, Nyangoto, Nyamongo, Kenyangi na Nyabigena.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Ama kweli mwaka huu haya madini yatapeleka watu kubaya... kudai kuwa umejenga shule wakati hujajenga?
 
TAMKO KUHUSU KAULI ZA KINGUNGE

Sisi, viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na TLP tuliokutana Equator Hotel tarehe 20 Septemba 2007 hapa Arusha tumeitafakari "Orodha ya Mafisadi"(List of Shame) na tumejadili kauli za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Siasa na Uhusiano wa Jamii-Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru alizozitoa 18 Septemba 2007 na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari Jumatano 19 Septemba 2007 na kwa pamoja tumeazimia kutoa tamko lifuatalo:

Kingunge anapotosha umma, apuuzwe; wapinzani wanatetea taifa

Tunaunga mkono uamuzi wa viongozi wetu wa kitaifa kuanika wazi kwa umma orodha ya mafisadi; hii ni kwa sababu rasilimali zinazofujwa ni za wananchi watanzania, wanaoathirika kutokana na ufisadi ni umma wa watanzania na wenye uamuzi wa mwisho wa kuwawajibisha viongozi mafisadi ni umma wa watanzania.

Kwa kuzunguka nchini kueleza yaliyotokea bungeni( hususani kusimamishwa kwa Mbunge Zitto Kabwe na kupigwa danadana kwa hoja ya kashfa ya ufisadi ndani ya Benki Kuu iliyokuwa iwasilishwe na Dr Wilbroad Slaa) wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajeti uliomalizika hivi karibuni, wabunge wa upinzani wanatimiza wajibu wao kama wawakilishi wa kweli wa wananchi.

Kwa kuzunguka nchini kueleza kuhusu ufisadi unaendelea nchini, viongozi wa upinzani wanatekeleza wajibu wao wa kisiasa wa kuwazungumzia wananchi wote wa Tanzania wanaoguswa na ufisadi bila kujali itikadi ama uanachama; ikumbukwe kuwa vyama vya siasa sio vyombo vya uchaguzi tu bali ni taasisi muhimu katika jamii katika kuchochea uwajibikaji na maendeleo. Kwa mantiki hiyo basi Waziri Kingunge anaupotosha umma anaposema kwamba ziara za viongozi wa upinzani zinatokana na ‘hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005, kambi ya upinzani kushindwa kumtetea Zitto bungeni, wivu wa kuona CCM inatekeleza ilani yake vizuri, na kwamba wanautumia vibaya mfumo wa vyama vingi'.

Tunapenda kusisitiza kuwa Viongozi wa umma wanaokiuka na/au kuvunja masharti ya katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria za Maadili ya Viongozi wa umma lazima waanikwe hadharani na kuwajibishwa na yoyote anayetoka kauli ya kubeza jitahada hizi ni vyema watanzania wakampuuza. Kama viongozi wa upinzani wanavunja sheria kwa kutoa uzushi na kufanya uchochezi kama Waziri Kingunge anavyodai kwa nini serikali haiwakamati na kuwapeleka mahakamani badala ya kutoa matamko ya kulalamika?

Kauli za Kingunge ni msimamo wa Serikali?; Ikulu itoe tamko!

Tumezijadili kauli za Waziri Kingunge na katika hatua ya sasa tusingependa kuamini kama zinawakilisha msimamo wa serikali kwa ujumla wake; hatutaki kuamini kwamba kauli hizo ni msimamo wa pamoja wa Serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri. Katika hatua ya sasa tunazichukulia kauli hizo kuwa ni maoni binafsi ya Bwana Kingunge mpaka hapo Ikulu itakapothibitisha vinginevyo; hivyo kwa tamko hili tungependa ikulu itoe ufafanuzi kuhusu kauli hizo. Lakini tunapenda pia kutoa tahadhari kwamba inawezekana kauli hizi za Bwana Kingunge amezitoa kwa nia ya kupoteza lengo tuanze kuzijadili kauli zake badala ya kujadili orodha ya mafisadi na hatma ya rasilimali za nchi yetu. Hivyo tungependa kusisitiza kuwa ikulu ijibu hoja zilizotolewa na viongozi wa upinzani ambazo zimemgusa moja kwa moja Rais na serikali.


Anayelinda ufisadi ndiye anayekwamisha maendeleo na huduma za kijamii.

Tunashangazwa na uamuzi kauli ya Kingunge kwamba uamuzi wa Viongozi wa Vyama na Wabunge wa Upinzani kuzunguka nchini ni mkakati wa kisiasa wa kuitoa serikali kwenye mstari wa kushughulikia maji, afya na barabara. Tunapenda kumbukusha Waziri Kingunge kuwa katika orodha hii ya mafisadi pekee zaidi ya shilingi trilioni 1.3(1,300,000,000,000) ambazo kama zingetumika vizuri ni wazi zingeweza kutumika kuboresha maji, umeme na barabara bila kuendelea kuwakamua zaidi wananchi masikini. Ukweli ni kuwa kwa kuendelea kulea ufisadi serikali inajitoa yenyewe kwenye mstari wa kutumia vyema kodi za wananchi na rasilimali za taifa katika kushughulikia shughuli za maendeleo na huduma za kijamii ikiwemo maji, afya na barabara. Ni ukweli pia kwamba kwa kuwawajibisha mafisadi viongozi wa upinzani wanatimiza wajibu wao wa kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa ustawi wa wananchi walio wengi.

Vyombo vya dola tayari vinayo orodha ya mafisadi vichukue hatua.

Tunashangazwa na kauli ya Waziri Kingunge ya kuhoji sababu za Viongozi wa Upinzani kushindwa kuziwasilisha kwenye vyombo vya dola tuhuma walizozitoa dhidi ya vigogo hao iwapo kweli wanao ushahidi wa kuzithibitisha. Tunashangazwa na kauli hii kwa kuwa tunaamini kabisa Waziri Kingunge anafahamu kabisa kuwa sehemu kubwa ya tuhuma hizi zipo katika Ripoti za Mkaguzi wa Serikali ikiwemo ile ya mwaka 2005/06 na kwamba vyombo vya dola vinafahamu uwepo wa tuhuma hizi lakini kwa zaidi ya miaka miwili vyombo hivyo havijachukua hatua dhidi ya vigogo waliotajwa.

Tunaamini kwamba viongozi wa upinzani walichofanya ni kuamua kushtaki kwa wenye mali walioibiwa ambao ni wananchi wote wa Tanzania ili kwa pamoja tuweze kuvitaka vyombo vya dola viweze kuchukua hatua. Tunashangazwa na kauli hii ya Waziri Kingunge ya ‘kuwahukumu' viongozi wa upinzani kwa kushindwa kupeleka ushahidi kwa kuwa kauli hii inapingana na kauli zingine ambazo zimewahi kutolewa na viongozi wa serikali kuhusu tuhuma hizo hizo.

Tunapenda kumkumbusha Waziri Kingunge kwamba tayari Spika Wa Bunge-Samuel Sitta alishasema kwamba anavipeleka polisi vielelezo vyote vya ushahidi alivyotoa Dr Slaa ili vichunguzwe. Pengine Kingunge angetoa hukumu hiyo kwa Spika kwa kushindwa kupeleka vielelezo. Pia ikumbukwe kwamba ni serikali hiyo hiyo iliyowahi kutoa taarifa kwa umma kwamba tuhuma za ufisadi ikiwemo za BOT zinachunguzwa na TAKUKURU.

Kadhalika Waziri Mkuu-Edward Lowasa alitoa kauli baadaye kwamba Serikali iliyafahamu madai ya Kashfa ya ufisadi Benki Kuu(BOT) kabla ya upinzani. Kwa upande mwingine, madai ya kutaka kushughulikia rushwa kubwa kubwa ikiwemo za kwenye mikataba yalianza kutolewa na Rais Kikwete wakati akifungua Mkutano wa Kwanza kabisa wa Bunge mwaka 2005.

Lakini baadaye ni Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba anawafahamu wala rushwa na anawapa muda wajirekebishe; tulitarajia Waziri Kingunge kama mshauri wa Rais wa masuala ya siasa angemshauri apeleke ushahidi katika vyombo vya dola na si kuwahukumu viongozi wa upinzani ambao wametoa orodha ya mafisadi na ushahidi kutoka kwenye taasisi za serikali yenyewe!. Na ni jukumu la vyombo vya dola kuchukua hatua za kufuatilia baada ya orodha ya mafisadi kuwekwa hadharani.


TAKUKURU inajipotezea imani yenyewe!

Tumeshangazwa pia na kauli ya Waziri Kingunge ya kuwalaumu viongozi wa upinzani kwa kutokuwa na imani na TAKUKURU. Kwa misingi ya kauli zao ambazo wamezitoa katika nyakati mbalimbali, viongozi wa upinzani wamekuwa wakikisisitiza kuwa TAKUKURU inajipotezea yenyewe imani kwa wananchi kutokana na taarifa zake na kwamba wamekuwa wakiipa changamoto TAKUKURU kuchukua hatua. Mathalani TAKURU kuisafisha kampuni ya RICHMOND. "….hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wa kamisheni watendaji wa serikali….uchunguzi huo umethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji na ambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara iliyosababishwa na udhaifu huo"(Mwananchi 12/5/2007). "….baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamu mwenendo wa mambo serikalini…"(Tanzania Daima 12/5/2007).

Maswali yaliyobaki mpaka hivi sasa ambayo si TAKURU wala TAKUKURU ya sasa hawajayajibu ni pamoja na: Ni kwanini Kamati ya Waziri Mkuu iliipa tenda Richmond baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kuitaka bodi yake ya sabuni kutangaza upya zabuni hiyo kwa kutimia zabuni za kimataifa? Richmond kuweza kufahamu mwenendo wa mambo ya ndani serikalini sio ishara ya rushwa ya kimadaraka? Ni kweli kama hakuna hasara iliyosababishwa na uamuzi huu wakati ambapo watanzania wamekaa bila umeme kwa miezi mingi bila kupata umeme wa dharura waliotarajia wakati wa dharura, Rais amekiri kwamba umeme ulichangia kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi na hata kuongeza mfumuko wa bei na mpaka leo bado megawatts 100 hazijatimizwa na Richmond/Dowans?

Tunapenda kumkumbusha Waziri Kingunge kwamba Mkataba wa Richmond/Dowans pekee umeligharimu taifa zaidi ya Bilioni 200 mpaka sasa ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye elimu, afya na barabara. Viongozi wa upinzani wanapohoji utendaji wa TAKUKURU wanataka ichukue hatua za haraka kushughulikia mafisadi na kuendelea kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa na si Taasisi ya Kulinda, Kusafisha ama Kutetea Rushwa !

Wasomi na asasi za kijamii wako sahihi; Kingunge amelewa madaraka Tumefadhaishwa na kauli ya Waziri Kingunge kwamba wasomi nchini wametathimini uamuzi wa Bunge wa kumsimamisha Mbunge Zitto Kabwe kwa kutanguliza jazba badala ya busara na kutilia wasiwasi uelewa wa makundi ya kijamii kuhusu mantiki ya uzalendo. Hatutaki kuamini katika hatua ya sasa kwamba huu ni msimamo wa serikali kwamba wasomi na makundi ya kijamii wametanguliza jazba na kukosa busara na uelewa katika kuijadili adhabu aliyopewa Mbunge Zitto Kabwe na hoja yake ya kutetea Rasilimali za nchi yetu hususani madini.

Tunaamini kwamba kauli hii ni maoni binafsi ya Bwana Kingunge ambayo ni ishara ya kulewa madaraka kutokana kung'ang'ania serikalini toka wakati nchi hii inapata uhuru kwani hii si mara ya kwanza kutoa kauli za kubeza-aliwahi kuibeza CHADEMA kwa kumtaja Nyerere kwenye kampeni 2005 na hivi karibuni Julai 3, 2007 aliripotiwa na vyombo vya habari akitetea msimamo wa Rais Kikwete wa kutumia nafasi yake kama rais kudhoofisha upinzani kwa kufanya kampeni za CCM katika mikutano ya kiserikali. Tunapenda kumbukusha Waziri Kingunge maneno ya Shaban Robert kwamba " elimu ilipokuwa bado kujulikana mvi zilihesabika kuwa alama ya hekima lakini fikra hizo wakati wake umeshapita haupo na wala hauji tena. Kisichobadilika ni kwamba mtu mzima bado anastahili heshima kutoka kwa mdogo" .

Ni vyema Waziri Kingunge akafahamu kwamba wasomi kama Profesa Issa Shivji na makundi ya Kijamii mathalani Mtandano wa Jinsia(TGNP), Chama cha Wanasheria wa Mazingira(LEAT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) walifanya tathmini yao kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa bila kujali itikadi. Mafisadi zaidi waendelee kutajwa; serikali ijibu hoja

Hivyo tunapongeza na tutaendelea kuunga mkono jitahada zote za vyama vya siasa, asasi za kijamii na hata watu binafsi waliowataja na watakaoendelea kuwataja viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

Kadhalika tunaunga mkono na kutoa mwito kwa vyama vya siasa, asasi za kijamii na hata watu binafsi kuendelea kuwawajibisha viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo yamesababisha taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania. Na katika haya tunataka serikali ijibu hoja na si kupuuzia na kutoa kauli za kejeli kama "hao ni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki ya kutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" . Waziri Kingunge na serikali kumbukeni kuwa watu wachache wanaweza kudanganyika katika muda mchache lakini watu wote hawewezi kudanganywa wakati wote. Watanzania wa leo na kesho si watanzania wa jana na juzi.


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa (CHADEMA)
Na Mwenyekiti wa Kikao

Godbless Lema
Katibu Mwenezi Mkoa-Arusha(TLP)
Na Msemaji wa Ushirikiano wa Vyama vya Upinzani-Arusha

Mohamed Maabad
Mwenyekiti wa Wilaya-Arusha Mjini(CUF)
Na Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Vyama vya
Upinzani-Arusha

Ened Muro
Mwakilishi-Arusha(NCCR-Mageuzi)

Amos Kibanda
Katibu Mkoa-Arusha(CHADEMA)

Calist Lazaro
Mwenyekiti wa wilaya-Arusha Mjini (TLP)
 
Basi! Nimeamini kwamba Mgonjwa Ukimwi na Masatu ni wagonjwa wa akili. Hata kama wametumwa mambo mengine mtu mzima akitumwa kuyatetea anayakataa. Kama wamejituma basi, tujue nao ni wezi tu kama hao wanaowatetea.

Hey! yamekuwa haya.........
 
Mwaka huu si mchezo naona kila kona watu wanacharuka, ndio demokrasia hiyo.
 
Back
Top Bottom