List ya Business Ideas kuhusu viwanda vidogo vidogo

List ya Business Ideas kuhusu viwanda vidogo vidogo

biashara ya home derivery , hapa unachukua oda za mahitaji ya familia mbalimbali una wasambazia mahitaji hayo bila wao kwenda sokoni au dukani kama gesi , mboga ,mchele n.k
 
Si kweli mkuu, hata Tanzania kusajili kampuni ni 24 hrs labda uniambie kuanza kufanya kazi(Operations) mpaka upate vibali vingine kutoka mamlaka mbalimbali kuhusiana na biashara yako UOTE="mdukuzi, post: 11906447, member: 194966"]nani kasdma hataki quality control na matusi ya nini,tanzania kusajili kampuni inachukua siku kadhaa ,kuna nchi jirani kampuni ndani ya masaa 24,urasimu huu una maana ya rushwa na sio quality control[/QUOTE]
Si
 
Yeah kuwa na kiwanda cha maji sio lazima chupa utengeneze mwenyewe coz ni expensive mtambo wake....unaweza. ukatengeneza kisha ukaoda vyupa vya kufungaahia ukawa unafanya sealed tu.

Hapa ni lazima uwe na matenki. makubwa na dawa ni kuyachimba chini sababu ata uvunaji wa maji ya mvua utakuwa mrahisi. Mfano wa matenki tunayoifadhia uchafu majumbani then haya yanakuwa na muinuko kidogo mpaka juu. Ungekuwa umeshafika Handeni ungenielewa kirahisi wanafanya sana hii ya kuvuna maji ya mvua na kuhifadhi.


Kuhusu treatment ya maji mimi sio mtaalam huko ila nahisi lazima uwe na mtambo fulani mdogo wa kuvuta maji ,kuyachemsha na kuyachanganya. So ishu kubwa hapa ni hiyo. mashine. Na nchi hii ina tatizo sana la mitambo midogo nilienda sido pale nikakuta mimashine ya kusaga nafaka ndio imejaa.

Kuna mtambo nilikuwa natafuta niliangaika sana sasa imebidi nijichange niuagize nje coz nilienda sido mpaka na laptop nikawaonyesha video zake na kila kitu nilidownload wakaishia kunipiga danadana si makao makuu wala vingunguti wote weupe tu.
Wanaajiri watu wasio na weledi.....fukuza weka damu mpya uangalie sido itavyobadilika. Tutakuta hadi rocket za kuendea nje ya dunia na mitambo ya nyukilia....shenzi
 
nani kasdma hataki quality control na matusi ya nini,tanzania kusajili kampuni inachukua siku kadhaa ,kuna nchi jirani kampuni ndani ya masaa 24,urasimu huu una maana ya rushwa na sio quality control
Usibishane naye huyo......mtu atayekuelewa ni yule aliyekumbana na hizo kadhia hawa watoto wa mama hawaelewi kero za wajasiliamali. Just mpotezee
 
Biashara ya kutengeneza mauwa ya plastic,
Yanahitaji ubunifu,
Ila siifahamu vizuri.
 
Ukishaona wazo Fulani limekuingia vema...waza kuanza usichelewe...pia gawa jukumu...Mimi nimewekeza ktk ushauri na uandishi wa michanganuo au proposals...Tafadhari tuwasiliane, kwakuwa mitaji shida nitafute tuandike proposal ya mradi wazo kuanza sh 150,000 hadi 350,000 kutegemea ukubwa wa mitaji...yaani milioni 1-50m. Contact 0682096669
 
b58d4bbe38b357f7400b84795d7336c9.jpg

Remember to note down. Helpful.
 
The first thing linapokuja idea ya biashara ni muhimu kuàndika.The Nobel prize winning in literature bwana sir John lous Braogas alisema"if you can't write your idea in the back of your note book,you haven't a right idea.
 
hata me nakuunga mkono biashara ya kushona nguo ni nzuri hata mimi nina wazo la kufungua kiwanda siku moja
 
Wazo langu ni juu ya kupata Mkaa kutokana na Pumba za mpunga.
Kwa kutumia machine rahisi.
Huku ninakoishi kuna miti ya kupandwa ikipasuliwa inanukia kama ubani. Tunatumia kuwashia Mkaa kwa urahisi. Je katika Ulimwengu wa ujasiriamali idea hili inaweza kuuzikana?
Wazo jingine la ujasiliamali wajuzi mtuelekeze namna ya kupanda uyoga wa bei rahisi. Je biashara ikiwini haiwezi kumtoa mtu?
Inawezekana kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba za mpunga au hata yale maranda.ila sijui kama itakua na faida.na mkaa unaotengenezwa kwa hayo mabaki unawaka kwa mda mrefu kuliko huu mkaa wa kawaida wa miti
 
Boksi za pizza.watu wamefunguka kula pizza kiwanda kidogo cha boks pizza na nembo unawekewa.mf boston pizza.

solar power energy,watu hawana umeme kinatakiwa kiwanda kidogo cha kutengeneza umeme wa Jua kwa bei nafuu.ma engineering tunao.

nepi za watoto take a way,watoto wanakunya kila wakati kifunguliwe kiwanda kidogo cha kutengeneza nepi kwa bei nafuu.

kiwanda kidogo cha kitengeneza nafaka kwa ajiri ya mifugo,yani kiwanda kinatengeneza protein zote za mifugo na nembo full pakeg bag kwa bei nafuu.

Kwa dar kiwanda kidogo cha kutengeneza miguu ya Kuku na shingo zake.kwa sababu inalipa.


Swissme:
Safi hii
 
Mawazo mazuri ila mnaishia juu juu, kuna watu wanapesa wanaweza kushawishika kuinvest wakakosa nyama....ila thread nimeipenda.

Naona idea nyingi ni za uzalishaji,unajua ni ngumu sana kuwa na biashara kubwa kwa kufanya uchuuzi wa bidhaa za mwenzako. Utaishia tu kuwa mfanyabiashara wa kati,haya mambo ya kuigana kufungua bar,barber shop,guest house,boutique utaishia kuwa mchuuzi.

Kuna biashara kama ya fenicha, vifungashio, viungo vya chakula,pedi nk.

Niliona mshikaji mmoja Kenya anatengeneza maji ya mvua anauza. Nilipenda sana idea yake sijui kibongobongo watu kama wataielewa coz jamaa yupo mtaani bado hajakua kivile ila anauza sana.
Hivi mkuu sio kwamba fenicha zinatoka taratibu sana au inaionaje hii biashara kama una A,B,C nipatie mkuu
 
waswahli wana hila, utarekebisha nyumba kwa makubaliano uikodishe kwa muda kodi mgawawane au uchukue yote, pia baadaye wanaweza kukugeuka.
Kuna mdada mtaani uku alijenga kwenye kiwanja cha mtu madarasa ya chekechea Kwa makubaliano ya kumlipa kiwanja kidogokidogo
Ee banae Dada kapandisha mpaka kwenye linta jamaa akamgeuka na hawakuandikishana popote
Kumbe yule Dada alikopa ile hela bac nasikia ilivyokuja sintofaham presha ikapanda kalazwa Hosp sijui anaendeleaje
 
Kuna mdada mtaani uku alijenga kwenye kiwanja cha mtu madarasa ya chekechea Kwa makubaliano ya kumlipa kiwanja kidogokidogo
Ee banae Dada kapandisha mpaka kwenye linta jamaa akamgeuka na hawakuandikishana popote
Kumbe yule Dada alikopa ile hela bac nasikia ilivyokuja sintofaham presha ikapanda kalazwa Hosp sijui anaendeleaje
Ni kosa sana kufanya makubaliano yasiyo na maandishi kwa mswahili.
Ni vigeugeu sana kwenye mambo ya pesa.
 
Back
Top Bottom